CCM wasambaza waraka wao, wapinga rasimu ya Katiba Mpya

Gazeti la mwananchi lina habari kuwa CCM wametoa Waraka wa Kupinga Rasimu ya Katiba Mpya kama ilivyotolewa na Tume ya Jaji Warioba.
Kama kawaida yao, wametoa sababu za kufikirika sana na zaidi ya yote zimedhihirisha kuwa wanafarijika sana kwa namna nchi inavyoendeshwa kupitia Katiba iliyopo! Inavyoonekana CCM kuna watu wachache wenye maamuzi ambao pia ni wavivu wa kufikiri ndiyo maana wameibuka na tamthiliya hizi zilizopitwa na wakati!

Waraka huo unaeleza kuwa kutokana na ukubwa wa eneo la uchumi wa Tanzania Bara ni wazi kwamba itachangia zaidi kwenye uendeshaji wa Serikali ya Muungano na kwamba jambo hilo linaweza kutoa mwanya kwa Serikali ya Tanzania Bara kuiburuza Serikali ya Muungano na Serikali ya Zanzibar.

Kiuchumi, mwongozo huo unaeleza kwamba Serikali ya Jamhuri ya Muungano itakuwa tegemezi kwa Serikali zinazounda muungano hasa Serikali ya Bara ambayo itakuwa na uchumi mkubwa.

“Urasimu wa kibiashara na umilikaji ardhi utaongezeka kwa sababu biashara, ardhi na umilikaji mali wa aina nyingine si mambo ya muungano, pia gharama za uendeshaji wa Serikali uliopo ni mkubwa na kuwepo kwa Serikali tatu itakuwa gharama zaidi,” unaeleza.

Kijamii, unaeleza kwamba Serikali tatu zitahatarisha amani, utulivu na utangamo wa kitaifa kwani watu wa pande mbili za muungano wamekuwa na uhusiano na mwingiliano kwa miaka mingi.

Katika sehemu ya faida za muundo wa Serikali mbili, mwongozo huo unafafanua kwamba muundo unaotumika sasa unawawezesha Wazanzibari kumiliki ardhi na rasilimali nyingine zilizopo Tanzania Bara kama raia wa Tanzania, ingawa ardhi na rasilimali nyingine za kiuchumi si masuala ya Muungano.

Katika mfumo wa kiutendaji kama ulivyoanishwa katika Ibara ya 67 hadi 101 ya rasimu hiyo, mwongozo huo unaeleza kuwa kutakuwa na mgongano wa viongozi pale ambapo Serikali hizo tatu zitakuwa chini ya uongozi wa vyama tofauti vya siasa au wagombea binafsi.

“Rasimu haijabainisha vyema mipaka ya uhusiano na ushirikiano kati ya Jamhuri ya Muungano na nchi au taasisi za nje kwa upande mmoja, kati ya Serikali ya Tanzania Bara na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na taasisi za nje.

“Hali hii inaweza kuleta mgongano kati ya Serikali hizi tatu, muundo wa Serikali hizi umeondoa nafasi ya Waziri Mkuu kuteuliwa kutoka miongoni mwa wabunge, lengo la Katiba iliyopo kutaka mawaziri wateuliwe kutoka miongoni mwa wabunge ni kuwafanya kuwajibika moja kwa moja bungeni ili Bunge liweze kuisimamia Serikali,” unaeleza.

Hii ni mara ya pili kwa CCM kutoa mwongozo wa aina hiyo, kwani katika awamu ya kwanza ya kutoa maoni, chama hicho kiliandaa mwongozo wake uliojielekeza kwenye mambo makuu ya msingi na yenye masilahi pekee kwa taifa.

Hata hivyo, kati ya mambo hayo ni mawili tu ndiyo yaliyopo katika rasimu hiyo ambayo ni dola kutokuwa na dini rasmi pamoja na ukomo wa idadi ya wabunge.

Mambo ambayo yalitolewa maoni na chama hicho na kutokuingizwa katika Rasimu ya Katiba ni kuendelea kwa mfumo wa Serikali mbili, rais kupatikana kwa wingi wa kura, mawaziri kutokutoka nje ya Bunge, wajumbe wa NEC kuthibitishwa na Bunge.

Nyingine ni kutokuwepo kwa mgombea binafsi, kuendelea kwa viti maalumu bungeni pamoja na kutokuhojiwa kwa matokeo ya urais mahakamani.

Soma zaidi kwenye link hii: CCM wasambaza waraka wao, wapinga rasimu ya Katiba Mpya - Kitaifa - mwananchi.co.tz

Sasa ni nini kisichoeleweka hapo kuhusu gharama za uendeshaji. Wengine wana argue kwa kuwa hawajui hata gharama za kutunza familia.
 
Uhai wa magamba upo kwenye jinamizi la muungano wa serekali mbili,ukiupangua muungano huo yanakata roho.
 
Our Motherland Tanganyika is back , LIWALO NA LIWE ! Poor Magamba !
 
Wana haki ya kutoa maoni yao. Sidhani kama tunaweza kuwahukumu kwa kutokubaliana na mapendekezo ya Tume ya Katiba.

yale sio mapendekezo ya TUME YA KATIBA , ni mapendekezo ya Umma wa Watanzania muache kujidai mnafikiri kwa niaba ya wenzenu. shame.
 
Hakuna watu walio na mawazo finyu na tegemezi kama Viongozi wa CCM. Inabidi vi2 vingne wa2mie akili, hv wanaposema gharama wana2mia akili ya kutoka kwa nani wakati wao wenyewe wanaibebesha serikali mzigo mkubwa kwa kukumbatia mafisadi, kufungua kesi dhidi ya wapinzani zinazoigharim serikali, kuunda vyeo visivyo na tija serikalini, kusaini mikataba feki na kushindwa kutoza kodi kwenye madini nk. Hivi hawa wanaposema serikali tatu ni gharama inamaana hata tume ya kuratibu mabadiliko ya katiba kwao inaonekana tayari ni mwiba? Subirini Chadema ishike hatamu ndo mtafaham ukidondokea pua unakuwaje.
 
Gazeti la mwananchi lina habari kuwa CCM wametoa Waraka wa Kupinga Rasimu ya Katiba Mpya kama ilivyotolewa na Tume ya Jaji Warioba.
Kama kawaida yao, wametoa sababu za kufikirika sana na zaidi ya yote zimedhihirisha kuwa wanafarijika sana kwa namna nchi inavyoendeshwa kupitia Katiba iliyopo! Inavyoonekana CCM kuna watu wachache wenye maamuzi ambao pia ni wavivu wa kufikiri ndiyo maana wameibuka na tamthiliya hizi zilizopitwa na wakati!

Waraka huo unaeleza kuwa kutokana na ukubwa wa eneo la uchumi wa Tanzania Bara ni wazi kwamba itachangia zaidi kwenye uendeshaji wa Serikali ya Muungano na kwamba jambo hilo linaweza kutoa mwanya kwa Serikali ya Tanzania Bara kuiburuza Serikali ya Muungano na Serikali ya Zanzibar.

Kiuchumi, mwongozo huo unaeleza kwamba Serikali ya Jamhuri ya Muungano itakuwa tegemezi kwa Serikali zinazounda muungano hasa Serikali ya Bara ambayo itakuwa na uchumi mkubwa.

“Urasimu wa kibiashara na umilikaji ardhi utaongezeka kwa sababu biashara, ardhi na umilikaji mali wa aina nyingine si mambo ya muungano, pia gharama za uendeshaji wa Serikali uliopo ni mkubwa na kuwepo kwa Serikali tatu itakuwa gharama zaidi,” unaeleza.

Kijamii, unaeleza kwamba Serikali tatu zitahatarisha amani, utulivu na utangamo wa kitaifa kwani watu wa pande mbili za muungano wamekuwa na uhusiano na mwingiliano kwa miaka mingi.

Katika sehemu ya faida za muundo wa Serikali mbili, mwongozo huo unafafanua kwamba muundo unaotumika sasa unawawezesha Wazanzibari kumiliki ardhi na rasilimali nyingine zilizopo Tanzania Bara kama raia wa Tanzania, ingawa ardhi na rasilimali nyingine za kiuchumi si masuala ya Muungano.

Katika mfumo wa kiutendaji kama ulivyoanishwa katika Ibara ya 67 hadi 101 ya rasimu hiyo, mwongozo huo unaeleza kuwa kutakuwa na mgongano wa viongozi pale ambapo Serikali hizo tatu zitakuwa chini ya uongozi wa vyama tofauti vya siasa au wagombea binafsi.

“Rasimu haijabainisha vyema mipaka ya uhusiano na ushirikiano kati ya Jamhuri ya Muungano na nchi au taasisi za nje kwa upande mmoja, kati ya Serikali ya Tanzania Bara na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na taasisi za nje.

“Hali hii inaweza kuleta mgongano kati ya Serikali hizi tatu, muundo wa Serikali hizi umeondoa nafasi ya Waziri Mkuu kuteuliwa kutoka miongoni mwa wabunge, lengo la Katiba iliyopo kutaka mawaziri wateuliwe kutoka miongoni mwa wabunge ni kuwafanya kuwajibika moja kwa moja bungeni ili Bunge liweze kuisimamia Serikali,” unaeleza.

Hii ni mara ya pili kwa CCM kutoa mwongozo wa aina hiyo, kwani katika awamu ya kwanza ya kutoa maoni, chama hicho kiliandaa mwongozo wake uliojielekeza kwenye mambo makuu ya msingi na yenye masilahi pekee kwa taifa.

Hata hivyo, kati ya mambo hayo ni mawili tu ndiyo yaliyopo katika rasimu hiyo ambayo ni dola kutokuwa na dini rasmi pamoja na ukomo wa idadi ya wabunge.

Mambo ambayo yalitolewa maoni na chama hicho na kutokuingizwa katika Rasimu ya Katiba ni kuendelea kwa mfumo wa Serikali mbili, rais kupatikana kwa wingi wa kura, mawaziri kutokutoka nje ya Bunge, wajumbe wa NEC kuthibitishwa na Bunge.

Nyingine ni kutokuwepo kwa mgombea binafsi, kuendelea kwa viti maalumu bungeni pamoja na kutokuhojiwa kwa matokeo ya urais mahakamani.

Soma zaidi kwenye link hii: CCM wasambaza waraka wao, wapinga rasimu ya Katiba Mpya - Kitaifa - mwananchi.co.tz

Poor CCM,

Hoja hazina mashiko kabisa na wala hata hazisisimui, imekula kwao, na haya mapendekezo yana Propaganda ndani yake uksoma between lines wanaongelea zaidi Tanzania kupata hasara ili wapate uungwaji mkono wa Wananchi. Goodness, Nawashauri tena, katika suala la Muungano CHADEMA na Taasisi nyingine zikomalie kwamba liamuliwe kwa Wananchi wa Zanzibar kupiga kura kivyao na Sisi Watanganyika tupige kivyetu sharti kila upande ukubaliane la sivyo, ngoma ni Serikali tatu.

Naendelea kushauri kwamba, kama issue ni kuwa na Marais watatu, Tanganyika iwe na Waziri Mkuu Mtendaji na Zanzibar hali kadhalika. CCM wanachekesha eti vyama tofauti na hiyo ndo raha maana kila Chama kitataka kufanya vema ili uchaguzi utakaofuata wapate sehemu zote. CHADEMA jiandaeni kuchukua Tanganyika na Serikali ndogo ya Tanzania maana Zanzibar ngoma bado, lolote laweza kutokea kati ya CUF na CCM ingawa CUF wana nafasi kubwa kwa sababu ya kete ya Muungano...Habari ndo hiyo CCM imekula kwenu, jiandae kuwa wapinzani 2015..CHADEMA piga jalamba mpira uwanjani
 
hii nchi si ya ccm bwana, ipo siku tutakata vichwa vyao hawa wadhalimu pale uwanja wa taifa ili iwe fundisho kwa wengine.
siku yenu inakuja na tutafunga mipaka ya nchi hii msipate pa kukimbilia, njinga sana nyinyi
 
Gazeti la mwananchi lina habari kuwa CCM wametoa Waraka wa Kupinga Rasimu ya Katiba Mpya kama ilivyotolewa na Tume ya Jaji Warioba.
Kama kawaida yao, wametoa sababu za kufikirika sana na zaidi ya yote zimedhihirisha kuwa wanafarijika sana kwa namna nchi inavyoendeshwa kupitia Katiba iliyopo! Inavyoonekana CCM kuna watu wachache wenye maamuzi ambao pia ni wavivu wa kufikiri ndiyo maana wameibuka na tamthiliya hizi zilizopitwa na wakati!

Waraka huo unaeleza kuwa kutokana na ukubwa wa eneo la uchumi wa Tanzania Bara ni wazi kwamba itachangia zaidi kwenye uendeshaji wa Serikali ya Muungano na kwamba jambo hilo linaweza kutoa mwanya kwa Serikali ya Tanzania Bara kuiburuza Serikali ya Muungano na Serikali ya Zanzibar.

Kiuchumi, mwongozo huo unaeleza kwamba Serikali ya Jamhuri ya Muungano itakuwa tegemezi kwa Serikali zinazounda muungano hasa Serikali ya Bara ambayo itakuwa na uchumi mkubwa.

“Urasimu wa kibiashara na umilikaji ardhi utaongezeka kwa sababu biashara, ardhi na umilikaji mali wa aina nyingine si mambo ya muungano, pia gharama za uendeshaji wa Serikali uliopo ni mkubwa na kuwepo kwa Serikali tatu itakuwa gharama zaidi,” unaeleza.

Kijamii, unaeleza kwamba Serikali tatu zitahatarisha amani, utulivu na utangamo wa kitaifa kwani watu wa pande mbili za muungano wamekuwa na uhusiano na mwingiliano kwa miaka mingi.

Katika sehemu ya faida za muundo wa Serikali mbili, mwongozo huo unafafanua kwamba muundo unaotumika sasa unawawezesha Wazanzibari kumiliki ardhi na rasilimali nyingine zilizopo Tanzania Bara kama raia wa Tanzania, ingawa ardhi na rasilimali nyingine za kiuchumi si masuala ya Muungano.

Katika mfumo wa kiutendaji kama ulivyoanishwa katika Ibara ya 67 hadi 101 ya rasimu hiyo, mwongozo huo unaeleza kuwa kutakuwa na mgongano wa viongozi pale ambapo Serikali hizo tatu zitakuwa chini ya uongozi wa vyama tofauti vya siasa au wagombea binafsi.

“Rasimu haijabainisha vyema mipaka ya uhusiano na ushirikiano kati ya Jamhuri ya Muungano na nchi au taasisi za nje kwa upande mmoja, kati ya Serikali ya Tanzania Bara na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na taasisi za nje.

“Hali hii inaweza kuleta mgongano kati ya Serikali hizi tatu, muundo wa Serikali hizi umeondoa nafasi ya Waziri Mkuu kuteuliwa kutoka miongoni mwa wabunge, lengo la Katiba iliyopo kutaka mawaziri wateuliwe kutoka miongoni mwa wabunge ni kuwafanya kuwajibika moja kwa moja bungeni ili Bunge liweze kuisimamia Serikali,” unaeleza.

Hii ni mara ya pili kwa CCM kutoa mwongozo wa aina hiyo, kwani katika awamu ya kwanza ya kutoa maoni, chama hicho kiliandaa mwongozo wake uliojielekeza kwenye mambo makuu ya msingi na yenye masilahi pekee kwa taifa.

Hata hivyo, kati ya mambo hayo ni mawili tu ndiyo yaliyopo katika rasimu hiyo ambayo ni dola kutokuwa na dini rasmi pamoja na ukomo wa idadi ya wabunge.

Mambo ambayo yalitolewa maoni na chama hicho na kutokuingizwa katika Rasimu ya Katiba ni kuendelea kwa mfumo wa Serikali mbili, rais kupatikana kwa wingi wa kura, mawaziri kutokutoka nje ya Bunge, wajumbe wa NEC kuthibitishwa na Bunge.

Nyingine ni kutokuwepo kwa mgombea binafsi, kuendelea kwa viti maalumu bungeni pamoja na kutokuhojiwa kwa matokeo ya urais mahakamani.

Soma zaidi kwenye link hii: CCM wasambaza waraka wao, wapinga rasimu ya Katiba Mpya - Kitaifa - mwananchi.co.tz[/QUOTE

"Mimi hofu yangu ni kwamba chama cha mapinduzi kinakundi kubwa katika vikao vya maamuzi(very popular),sitatizama sana uchangiaji wa watanzani(umma) katika mchakato wa mabadiliko ya katiba,wanananchi ambao sauti zao sichochote kwa serikali ya chama chamapinduzi,tukianzia mabaraza ya mabadiliko ya kila wilaya na Bunge maalumu la kikatiba.Mapendekezo yanayopendekezwa na chama cha mapinduzi kwa asilimia 90% yatafikiwa kwa ukweli huu wa wakilishi wa CCM huvutwa na mitizamo ya chama kuliko ya yale ambayo nikero kwa wananchi.Kwa taswira hii kunaumuhimu wakulitazama sakata hili kwa mtazamo unaostahili kwa mfano tulipokubali mfumo wa vyama vingi vya siasa asilimia 80% ya watanzania walitaka tuendelea na mfumo wa chama kimoja cha siasa.lakini kwa shinikizo la Banki ya dunia,shirika la fedha la dunia(IMF),kusambaratika umoja wa Soviet,kuongozeka kwa elimu ya uraia kwa wananchi,serikali ya chama cha mapinduzi ilisalimu amri kwa umma wa watanzania.watanzania hatutakuwa radhi kuona matakwa ya watanzania yanakandamizwa na taasisi dhaifu.
 
1+1=2, not 3

1-1=0 not 1, kwa hesabu zako na Nyerere Zanzibar-Tanganyika=Hakuna taifa. Kuanzia leo tumia hesabu za kigreat thinker, yani ukiunganisha/jumlisha TNK na/+ ZNZ=TZ yani nchi moja na ukitengenisha Tz unapata Znz na Tnk. Kwa iyo nyie wanzibar kuweni wapole Znz itatoa 5 regions ambayo itakuwa miongoni ya mikoa 30 ya Tz ukijumlisha 25 ya Tanganyika!!
 
Ma ccm hovyo kabisa wanaona ni sawa mzanzibar kumiliki ardhi bara ila mtanganyika marufuku zanzibar,muungano wa govt 2 umefeli msiturudishe nyuma
 
Waraka huo unaeleza kuwa kutokana na ukubwa wa eneo la uchumi wa Tanzania Bara ni wazi kwamba itachangia zaidi kwenye uendeshaji wa Serikali ya Muungano na kwamba jambo hilo linaweza kutoa mwanya kwa Serikali ya Tanzania Bara kuiburuza Serikali ya Muungano na Serikali ya Zanzibar.

Kwani kwasasa Zanzibar haiburuzwi?
 
Back
Top Bottom