Mfikirishi
JF-Expert Member
- Jan 16, 2012
- 11,397
- 13,722
Gazeti la mwananchi lina habari kuwa CCM wametoa Waraka wa Kupinga Rasimu ya Katiba Mpya kama ilivyotolewa na Tume ya Jaji Warioba.
Kama kawaida yao, wametoa sababu za kufikirika sana na zaidi ya yote zimedhihirisha kuwa wanafarijika sana kwa namna nchi inavyoendeshwa kupitia Katiba iliyopo! Inavyoonekana CCM kuna watu wachache wenye maamuzi ambao pia ni wavivu wa kufikiri ndiyo maana wameibuka na tamthiliya hizi zilizopitwa na wakati!
Waraka huo unaeleza kuwa kutokana na ukubwa wa eneo la uchumi wa Tanzania Bara ni wazi kwamba itachangia zaidi kwenye uendeshaji wa Serikali ya Muungano na kwamba jambo hilo linaweza kutoa mwanya kwa Serikali ya Tanzania Bara kuiburuza Serikali ya Muungano na Serikali ya Zanzibar.
Kiuchumi, mwongozo huo unaeleza kwamba Serikali ya Jamhuri ya Muungano itakuwa tegemezi kwa Serikali zinazounda muungano hasa Serikali ya Bara ambayo itakuwa na uchumi mkubwa.
"Urasimu wa kibiashara na umilikaji ardhi utaongezeka kwa sababu biashara, ardhi na umilikaji mali wa aina nyingine si mambo ya muungano, pia gharama za uendeshaji wa Serikali uliopo ni mkubwa na kuwepo kwa Serikali tatu itakuwa gharama zaidi," unaeleza.
Kijamii, unaeleza kwamba Serikali tatu zitahatarisha amani, utulivu na utangamo wa kitaifa kwani watu wa pande mbili za muungano wamekuwa na uhusiano na mwingiliano kwa miaka mingi.
Katika sehemu ya faida za muundo wa Serikali mbili, mwongozo huo unafafanua kwamba muundo unaotumika sasa unawawezesha Wazanzibari kumiliki ardhi na rasilimali nyingine zilizopo Tanzania Bara kama raia wa Tanzania, ingawa ardhi na rasilimali nyingine za kiuchumi si masuala ya Muungano.
Katika mfumo wa kiutendaji kama ulivyoanishwa katika Ibara ya 67 hadi 101 ya rasimu hiyo, mwongozo huo unaeleza kuwa kutakuwa na mgongano wa viongozi pale ambapo Serikali hizo tatu zitakuwa chini ya uongozi wa vyama tofauti vya siasa au wagombea binafsi.
"Rasimu haijabainisha vyema mipaka ya uhusiano na ushirikiano kati ya Jamhuri ya Muungano na nchi au taasisi za nje kwa upande mmoja, kati ya Serikali ya Tanzania Bara na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na taasisi za nje.
"Hali hii inaweza kuleta mgongano kati ya Serikali hizi tatu, muundo wa Serikali hizi umeondoa nafasi ya Waziri Mkuu kuteuliwa kutoka miongoni mwa wabunge, lengo la Katiba iliyopo kutaka mawaziri wateuliwe kutoka miongoni mwa wabunge ni kuwafanya kuwajibika moja kwa moja bungeni ili Bunge liweze kuisimamia Serikali," unaeleza.
Hii ni mara ya pili kwa CCM kutoa mwongozo wa aina hiyo, kwani katika awamu ya kwanza ya kutoa maoni, chama hicho kiliandaa mwongozo wake uliojielekeza kwenye mambo makuu ya msingi na yenye masilahi pekee kwa taifa.
Hata hivyo, kati ya mambo hayo ni mawili tu ndiyo yaliyopo katika rasimu hiyo ambayo ni dola kutokuwa na dini rasmi pamoja na ukomo wa idadi ya wabunge.
Mambo ambayo yalitolewa maoni na chama hicho na kutokuingizwa katika Rasimu ya Katiba ni kuendelea kwa mfumo wa Serikali mbili, rais kupatikana kwa wingi wa kura, mawaziri kutokutoka nje ya Bunge, wajumbe wa NEC kuthibitishwa na Bunge.
Nyingine ni kutokuwepo kwa mgombea binafsi, kuendelea kwa viti maalumu bungeni pamoja na kutokuhojiwa kwa matokeo ya urais mahakamani.
Soma zaidi kwenye link hii: CCM wasambaza waraka wao, wapinga rasimu ya Katiba Mpya - Kitaifa - mwananchi.co.tz