Mkuu tpaul,
Kwangu mimi,nadhani huu ni ukweli kabisa,ni suala la muda tu,maana mambo yanayofanywa na CCM kwa sasa ni kama wamechanganyikiwa, au sijui laana ya yule kiongozi wa dhehebu fulani la dini nchini imewafikia?..
La pili,ilikuweka rekodi sawia,Mkuu wa mkoa wa Dodoma ni Dr.Rehema Nchimbi,huyo bi Mwasha ni wa Tabora
Asante.
Kuna taarifa za chini chini kwamba serikali ya CCM imeuagiza uongozi wa TBC kusitisha kurusha matangazo ya moja kwa moja kutoka bungeni Dodoma ili kuwanyima fursa wananchi kufuatilia mjadala wa utunzi wa katiba utakaoanza ngwe ya pili kesho Jumanne. Lengo kubwa ni kuwafanya wananchi wasijue kinachoendelea ndani ya ukumbi wa bunge. Imeazimiwa kwamba TBC Taifa (RTD) warekodi kipindi hicho na kukihariri kwa kadri watakavyoona inafaa na kisha kukirusha kupitia redioni saa 4 usiku.
Aidha wamekipiga marufuku kituo cha Stat TV kurusha mjadala huo moja kwa moja kama walivyokuwa wakifanya katika ngwe ya kwanza. Mkuu wa mkoa wa Dodoma Bi Rehema Nchimbi na wakuu wengine wa mikoa wameagizwa kuwazuia watu kujadili katiba hiyo katika mji wa Dodoma na mikoa mingine kwa kisingizio cha kuwavuruga wajumbe watakaoukuwa wakijadiliana bungeni. Baadhi ya vyombo vya habari, hasa vya binafsi, vimepigwa marufuku kusogelea ukumbi wa bunge wakati mijadala itakapokuwa ikiendelea. Wameelekezwa wasubiri mjadala ukiisha watakuwa wanapewa taarifa na katibu wa bunge mara moja kwa kila siku.
Ndugu zangu, huu ni udikteta. Naona sasa CCM inakaribia kabisa kuiingiza nchi hii katika machafuko. TBC inaendeshwa kwa kodi za umma. Sasa iweje wananchi wazuiwe kupata habari na kufuatilia michango ya utunzi wa katiba mpya? Hili jambo halikubaliki hata kidogo. Kama kuna mtu mwenye taarifa kamili juu ya hujuma hizi naomba atujuze. Kama ni kweli CCM wameamua kuwanyanyasa wananchi namna hii, nchi hii sasa itakuwa imegeuza kuwa ya kidikteta.
:israel:
Mkuu tpaul,
Kwangu mimi,nadhani huu ni ukweli kabisa,ni suala la muda tu,maana mambo yanayofanywa na CCM kwa sasa ni kama wamechanganyikiwa, au sijui laana ya yule kiongozi wa dhehebu fulani la dini nchini imewafikia?..
La pili,ilikuweka rekodi sawia,Mkuu wa mkoa wa Dodoma ni Dr.Rehema Nchimbi,huyo bi Mwasha ni wa Tabora
Asante.
Unategemea nini kutoka Serikali dhalimu iliyojaa wahuni ? wamejiona hawana hoja sasa ni kauli za kibabe tu huku wakiwa wamejificha mgongoni mwa vyombo vya dola. Hii ni katiba ya Watanzania kwanini wanachojadili kifanywe siri? Wanajua watafanya madudu ambayo Watanzania tukiyaona live kamwe hatuwezi kukubali uhuni na uharamia wao. Sasa ndio wameamua kufanya kila kitu nyuma ya pazia huku wakilipana mabiioni ya posho kutoka kwenye pesa za walipa kodi. Wafanye tu walitakalo lakini pesa za walipa kodi wasiziguse. Kuendelea kulipana shilingi laki tatu kwa siku huku wakijua fika kwamba wanachokifanya hakitakubalika na Watanzania walio wengi ni ufisadi na wizi wa mchana kweupe.
Sawa hili ni zoezi zuri tupate katiba yetu nzuri ukawa wasituharibie nchi.
Sawa hili ni zoezi zuri tupate katiba yetu nzuri ukawa wasituharibie nchi.
Taarifa haina chanzo watu wanaijadili kama ni kweli!!