CCM wapanga kuhujumu CHADEMA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM wapanga kuhujumu CHADEMA

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by sweke34, Jun 11, 2011.

 1. s

  sweke34 JF-Expert Member

  #1
  Jun 11, 2011
  Joined: Sep 28, 2010
  Messages: 2,533
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  MKAKATI wa makusudi umesukwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) ili kudhoofisha jitihada za kisiasa za Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), MwanaHALISI limeelezwa.
  Mkakati unalenga kuzuia viongozi wakuu wa CHADEMA kufanya kazi za kisiasa na hata za kibunge; kwa kuwapotezea muda katika malumbano na polisi, serikali na mahakama.
  Taarifa zinasema katika mpango huo, CCM na serikali yake wamepanga kuwakamata na kuwafungulia kesi viongozi wakuu wa chama hicho ili kuzima moto uliowashwa na chama hicho mijini na vijijini.
  MwanaHALISI limeelezwa na kiongozi mmoja wa ngazi ya juu wa serikali kuwa hata kuzuiliwa kwa Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe kwenye Kituo Kikuu cha Polisi (Central) jijini Dar es Salaam kwa maelezo ya kutekeleza amri ya mahakama, ni sehemu ya utekelezaji wa mkakati huo.
  Mbowe aliwekwa rumande jijini Dar es Salaam kwa siku mbili mfululizo, kati ya Jumamosi na Jumatatu asubuhi, baada ya mwenyewe kujipeleka kituoni.
  Ilipofika usiku wa manane Jumapili, Mbowe alipelekwa uwanja wa ndege wa Mwalimu Nyerere Dar es Salaam na kupakiwa kwenye ndege kubwa ya jeshi chini ya ulinzi mkali wa viongozi wa Polisi mkoani kwa safari ya mjini Arusha.
  Tayari mpaka sasa, wabunge zaidi 10 wa chama hicho wameshakamatwa na kufunguliwa kesi mahakamani au polisi.
  Ukimuondoa Mbowe, viongozi waliokamatwa na kufikishwa mahakamani au polisi, ni Godbless Lema (mbunge wa Arusha Mjini), Philemon Ndesamburo (Moshi Mjini) na Joseph Selasini (Rombo).
  Wengine ni Meshack Opurukwa (Meatu), Tundu Lissu (Singida Mashariki), Esther Matiko (Viti Maalum) na Zitto Kabwe (Kigoma Kaskazini).
  Mbali na wabunge, viongozi wengine wa chama hicho wanakabiliwa na lundo la kesi mahakamani.
  Hao ni pamoja na Dk. Willibrod Slaa, katibu mkuu wa chama hicho, mwenyekiti wa mkoa wa Arusha, Samson Mwigamba na kiongozi wa ngazi ya juu katika Baraza la Vijana la CHADEMA (BAVICHA), Dadi Igogo.
  “Nakwambia kijana, yote haya yanafanyika kwa madhumuni ya kuidhoofisha CHADEMA. Haiwezekani kwamba mtu amejisalimisha polisi mwenyewe, azuiliwe kwa kisingizio cha kutekeleza amri ya mahakama,” ameeleza mtoa taarifa.
  Amesema kukamatwa na kuwekwa rumande kwa Mbowe kumefanyika ili “kumdhalilisha yeye binafsi na kuwatisha wanachama na wafuasi wa chama chake.”
  Amesema, “Mkakati huu umelenga kuwajenga wanachama woga na kuwafanya viongozi waliofunguliwa kesi kushindwa kutimiza majukumu yao kwa kuwa hadi uchaguzi mkuu unafika wanakuwa bize na kesi na hivyo wanashindwa kufanya kazi zao za kisiasa.”
  Kukamatwa kwa Mbowe kumekuja wiki moja baada ya Jaji Mkuu wa Tanzania Bara, Othman Chande kuhudhuria semina elekezi iliyoitishwa na serikali mjini Dodoma.
  Haijafahamika mara moja kama kamatakamata hiyo inatokana na semina hiyo au imekuja kwa “bahati mbaya.”
  Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Arusha, Charles Magessa ndiye aliyetoa amri ya kutaka Mbowe akamatwe kwa madai kuwa, si yeye wala mdhamini wake, waliofika mahakamani kueleza kilichowasibu siku kesi yake ilipotajwa tena.
  Tangu Januari mwaka huu, Mbowe na viongozi wenzake kadhaa walishitakiwa kwa tuhuma za kufanya maandamano bila kibali cha polisi.
  Gazeti hili limeelezwa na vyanzo vya uhakika kuwa Hakimu Magesa awali alikubaliana na hoja zilizotolewa mahakamani na mdhamini wa Mbowe ambaye alieleza kuwa alikuwa mgonjwa na si kweli kuwa hajawahi kufika mahakamani kwa muda mrefu.
  Baada ya maelezo ya mdhamini wa Mbowe, hakimu Magessa alikubali kufuta hati ya kumkamata Mbowe na aliridhia haja ya Mbowe pamoja na wabunge wengine wanaoshitakiwa pamoja kuruhusiwa kushiriki vikao vya bunge.
  Lakini katika hali ya kushangaza, jioni ya siku hiyo, hakimu Magessa alitoa uamuzi wa kukamatwa kwa mwanasiasa huyo mwenye ushawishi mkubwa.
  Taarifa zinasema ni baadhi ya maofisa wa mahakama waliopeleka taarifa za amri ya kumkamata Mbowe kwa wakili wake, Method Kimomogoro.
  Mara baada ya wakili Method kujulishwa kuwa hakimu Magessa ameendelea na msimamo wake wa kutaka Mbowe akamatwe, haraka alirudi mahakamani ambako inadaiwa alikuta hakimu ameshaondoka kazini.
  Taarifa zinasema hakimu alikwenda Babati kwenye harusi.
  Wakili Method ameelezwa kukutana na msajili wa mahakama. Naye msajili inaelezwa alipitia jalada la mwenendo wa kesi na kukuta, pamoja na kuwapo maelezo ya kutosha ya mdhamini wa Mbowe, hakimu Magessa bado aliamuru Mbowe akamatwe.
  “Baada ya kuona hivyo, msajili wa mahakama aliamua kuwasiliana na hakimu kwa simu yake ya mkononi na kumweleza kuwa alikuwa hajafuta amri inayomtaka Mbowe akamatwe. Akatakiwa kumuagiza hakimu kiongozi aliyepo kufuta amri hiyo ili kuondoa usumbufu kwa mhusika,” anasema mtoa taarifa.
  Hata hivyo, mtoa taarifa anamnukuu hakimu akisema, “Nitakuja kushughulikia mwenyewe Jumatatu.”
  “Unajua yule hakimu alifuta hati ya kukamatwa Mbowe. Lakini hakutoa uamuzi kimaandishi. Hivyo ikatolewa amri Mbowe akamatwe,” ameeleza ofisa huyo wa mahakama mjini Arusha.
  Maelezo ya ofisa huyo wa mahakama yanafanana na yale yaliyotolewa na wakili Method, kwamba hakimu Magessa alijichanganya katika uamuzi wake.
  Mbowe alijipeleka mwenyewe polisi Jumamosi jioni na kuwa na mashauriano yaliyodumu kwa saa kadhaa kati yake, viongozi wa jeshi la polisi na wanasheria wa chama hicho, Mabere Marando na Lissu.
  Hata hivyo, baada ya makubaliano ya jinsi atakavyokwenda Arusha, imeelezwa kuwa aligeuziwa kibao na kushikiliwa hadi juzi Jumatatu alipofikishwa mahakamani mjini Arusha.
  Katika mashauriano hayo, viongozi wa polisi walikuwa wamekubaliana na maombi ya mawakili wa CHADEMA kuwa Mbowe aende mwenyewe mahakamani Jumatatu asubuhi, lakini kwa sharti kwamba aripoti katika kituo hicho cha polisi na kisha ataruhusiwa kuondoka.
  Wakili Marando amethibitisha kuwa kabla ya Mbowe kwenda kujisalimisha, kulifanyika majadiliano marefu kati yao na viongozi wa polisi; majadiliano yaliyolenga kutafuta njia mwafaka ya kumfanya kiongozi wao kufika Arusha bila bughudha.
  “Ni kweli tulikwenda polisi kufanya majadiliano ya jinsi mwenyekiti wetu atakavyofika Arusha. Tulifanya hivyo kwa nia njema. Hatukutaka mwenyekiti wetu kwenda kienyeji ili asije kukamatwa uwanja wa ndege au njiani wakati anakwenda Arusha na kisha ikatafsiriwa kuwa alikuwa anataka kukimbia,” ameeleza Marando.
  Anasema, “Tulipokuwa katika majadiliano hayo, ndipo polisi wakaeleza kuwa makubaliano hayo hayawezi kufanyika bila mheshimiwa Mbowe kufika ili aonekane ameripoti polisi. Na sisi hatukuwa na pingamizi; tukafanya kama tulivyokubaliana.”
  Habari zinasema baadaye, polisi wakionekana kama waliopokea amri kutoka juu, waligeuka na kumueleza Mbowe kuwa yuko chini ya ulinzi, jambo ambalo wakili Marando anasema linaonekana lilifanywa kwa shinikizo kutoka nje ya jeshi la polisi.
  Akizungumzia kukamatwa kwa Mbowe, Dk. Slaa alituhumu mbele ya waandishi wa habari, Jumapili iliyopita kuwa Rais Kikwete na chama chake wamesimama nyuma ya matukio yote ya kukamatwa kwa viongozi wa CHADEMA.
  Alionya kuwa chama chake kimechoka kunyanyaswa na kusema, “Hakuna wa kuzima moto tuliowasha.”

  Source: Mwanahalisi
   
 2. Mwanakili90

  Mwanakili90 JF-Expert Member

  #2
  Jun 11, 2011
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 1,571
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  mbowe Kama maNDELA,WE MFuNGENI TU,MANA MNACHOZUIA aSIKISEME MBONA TUMESHAJUA.
   
 3. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #3
  Jun 11, 2011
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  Mpanga mikakati mwenyewe ndio huyu bwana mabembea , hawataweza, na wakijaribu wataumia, CDM tunapepea mbele kwa mbele.
  [​IMG]
   
 4. s

  siraji Member

  #4
  Jun 11, 2011
  Joined: Mar 13, 2010
  Messages: 47
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nadhani CCM haina haja ya kupambana na chama ambacho watanzania huwa wanakikataa katika chaguzi zilizopita.Hoja nyingine zimekaa kipropaganda sana kiasi kwamba hata mtoto mdogo anatambua kuwa makala hiyo juu ni ya ushabiki tu.Haiwezekani watu wakavunja sheria serikali ikakaa kimya tu ikiwakodolea macho.Hapo itakuwa haitimizi wajibu wake.CDM iliapa kuona nchi hii haitawaliki na ndicho kinachofanyika sasa kwa kuwatumia wananchi ili watimize malengo yao.Hii nchi ina serikali ambayo wajibu wake wa kwanza is to maintain peace and order, bila kujali mkubwa au mdogo, bila kujali una kinga au huna kinga, bila kujali ww ni mbunge au waziri.Ukiiba au ukivunja sheria yoyote ile basi inabidi uchukuliwe hatua.Rais Kikwete na seriksli yake amekua akifanya hivyo kwa kuwafikisha mahakamani hata wabunge wake wa CCM mfano Mramba na Chenge na wengine wengi tu akiwemo marehemu Ditopile n.k.Viongozi wa cdm wanaokamatwa hawafuatwi majumbani mwao au misikitini au makanisani bali hukamatwa katika eneo la tukio.Tuache kulalama kusikokuwa na mantiki, tulinde amani yetu kwa gharama yoyote ile.
   
 5. Hmaster

  Hmaster JF-Expert Member

  #5
  Jun 11, 2011
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 347
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Umeona utumie wino wa kijani ili tujue wazi kwamba wewe ni mkereketwa wa Chama Cha Magamba si ndiyo? Sasa mimi ninaandika kwa wino mwekundu na kukueleza wewe na magamba wenzako kwamba moto uliowashwa na CHADEMA ni balaa. Kila jambo tunalitazama kwa makini sana, tukihisi tu linakiuka haki tunakwenda barabarani haraka sana. Mmezoea siasa laini nyie magamba!
   
 6. Mr.Professional

  Mr.Professional JF-Expert Member

  #6
  Jun 11, 2011
  Joined: Oct 4, 2010
  Messages: 1,602
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Sio rahisi kuzuia mvua isinyeshe na chadema ni kama mvua tukiamua kunyesha tunanyesha. washakuja na hoja lukuki kama CDM ni chama cha wachaga ila cha ajabu hata mie nisie mchaga ni mwanachama halali wa CDM. wakaja na hoja ya Udini lkn nayo naona wameshindwa kwani wao ndio wadini namba 1. Sasa huu mpango mkakati wa kutumia polisi na mahakama mbona tunautambua lkn mwisho wa siku tutashinda. Njia ya ukombozi ni lazima iwe na mabonde, mashimo, miba na kila aina ya vikwazo ili hao wanaoutaka ukombozi wakate tamaa.
   
 7. m

  moshijeff Senior Member

  #7
  Jun 11, 2011
  Joined: May 31, 2011
  Messages: 102
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Walimfunga Nelson Mandela, Wakamfunga na Jomo Kenyata lakini Uhuru ukapatikana. nawaambia MAGAMBA MAVI kuwa waelewe, GEREZA, Mahakama na polisi Havijawahi kuzuia UHURU Mahali popote pale duniani, kwa CDM ni kama wametia PETROL kwenye moto unaowaka wakizani utazima mda sio mrefu.hii wametuhamasisha zaidi. so CCM kuweni makini sana coz njia mnazopitia tunaziona tutawapiga tikitaka mpotelee mbali maskini wa fikra wakubwa nyie kaleni kitabu kwanza muondoe huo utapia Elimu mlionao
   
 8. Rweye

  Rweye JF-Expert Member

  #8
  Jun 11, 2011
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 15,047
  Likes Received: 3,080
  Trophy Points: 280
  CDM haimtegemei mtu mm1 hata akifungwa mbowe naamini Mbowe atakuwa ni sauti ya mwana aliae nyikani,walioko nje tutapambana mpaka tone la mwisho (till the last drop of our blood)

  Mpango huu tushaujua na siyo hatari tena make adui usiyemjua ni hatari kuliko yule unayemjua,kwa vile tushajua uadui huu na sraa zao,CDM tunaandaa kinga (shield) na kamwe CCM haitudhuru tena,CHADEMA ni jeshi kubwa
   
 9. S

  SEAL Team 6 JF-Expert Member

  #9
  Jun 11, 2011
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 655
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hilo linajulikana tangu awali pale polisi walipotekeleza mauaji ya Arusha, huo pia ulikuwa ni mpango mahususi wa kuidhoofisha Chadema. Tunashukuru MwanaHalisi kwa kutufumbua akili, pia tutegemee Wabunge wengine zaidi kukamatwa. Ngoja tusubiri tuone kama Wabunge wa Chadema Akina Zitto waliokataa posho watakamatwa!.
   
 10. jouneGwalu

  jouneGwalu JF-Expert Member

  #10
  Jun 11, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,680
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  Hili la posho za watumishi wote serikalini linawatosha sana, hadi walimalize hili kazi wanayo,
  Kuikabili CDM ni kazi inayohitaji chama /watu waliotayari kujitoa muhanga mara 2 zaidi ya wao CDM,
  Haya hapo CCM wana nani wa kujitoa muhanga kwa ajiri ya chama na akitokea je atakuwa na maslahi kwa umma???
  Kwishaaaa CCM
   
 11. Filipo

  Filipo JF-Expert Member

  #11
  Jun 11, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 9,330
  Likes Received: 210
  Trophy Points: 160
  Pole sana!
  ukitoka kitandani, i mean ukiamka utaiona dunia.
   
 12. Dume la Mende

  Dume la Mende JF-Expert Member

  #12
  Jun 11, 2011
  Joined: Mar 23, 2011
  Messages: 419
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  CHADEMA nyambinyambi
   
 13. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #13
  Jun 11, 2011
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Labda tuone Mr Six kama atajitoa, kuungana na CDM
   
 14. F

  FJM JF-Expert Member

  #14
  Jun 11, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  @Siraji, tuanze na Mramba. Serikali ya Kikwete imemfungilia mashitaka Mramba kwa kile ilichosema 'matumizi mabaya ya madara' yaliyosababisha hasara kwa taifa. Wakati wa campaign za uchaguzi mkuu 2010 Kikwete huyo huyo ambaye serikali yake imepfungilia mashitaka Mramba, alienda Rombo kuwaomba wananchi wampe kura Mramba! Kwa maneno mengine Kikwete anasema ana tatizo na Mramba kwa sababu anatumia madaraka vibaya, wakati huo huo Kikwete anawaambie wananchi wampe Mramba 'madaraka' (ubunge nao ni madaraka)! Nimeeleza hili ili uone just how ridiculous is your argument.

  Haya, turudi kwenye hii hoja "Haiwezekani watu wakavunja sheria serikali ikakaa kimya tu ikiwakodolea macho" -
  You are kidding me right? EPA, Richmond, IPTL, Kagoda, Rada na ndugu na jamaa wote wanaofanana na haya - utasema hakuna sheria iliyovunjwa hapo? Serikali ilikuwa wapi? Mbowe amefanya nini kikubwa kushinda EPA mpaka alale central na kusafirishwa usiku usiku tena kwa ulinzi mkali?
   
 15. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #15
  Jun 11, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,608
  Likes Received: 82,182
  Trophy Points: 280
  CCM wapanga kuhujumu CHADEMA[HR][/HR]
  [​IMG]
  Na Alfred Lucas - Imechapwa 08 June 2011

  [​IMG][​IMG] [​IMG]

  MKAKATI wa makusudi umesukwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) ili kudhoofisha jitihada za kisiasa za Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), MwanaHALISI limeelezwa.
  Mkakati unalenga kuzuia viongozi wakuu wa CHADEMA kufanya kazi za kisiasa na hata za kibunge; kwa kuwapotezea muda katika malumbano na polisi, serikali na mahakama.
  Taarifa zinasema katika mpango huo, CCM na serikali yake wamepanga kuwakamata na kuwafungulia kesi viongozi wakuu wa chama hicho ili kuzima moto uliowashwa na chama hicho mijini na vijijini.

  MwanaHALISI limeelezwa na kiongozi mmoja wa ngazi ya juu wa serikali kuwa hata kuzuiliwa kwa Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe kwenye Kituo Kikuu cha Polisi (Central) jijini Dar es Salaam kwa maelezo ya kutekeleza amri ya mahakama, ni sehemu ya utekelezaji wa mkakati huo.

  Mbowe aliwekwa rumande jijini Dar es Salaam kwa siku mbili mfululizo, kati ya Jumamosi na Jumatatu asubuhi, baada ya mwenyewe kujipeleka kituoni.
  Ilipofika usiku wa manane Jumapili, Mbowe alipelekwa uwanja wa ndege wa Mwalimu Nyerere Dar es Salaam na kupakiwa kwenye ndege kubwa ya jeshi chini ya ulinzi mkali wa viongozi wa Polisi mkoani kwa safari ya mjini Arusha.

  Tayari mpaka sasa, wabunge zaidi 10 wa chama hicho wameshakamatwa na kufunguliwa kesi mahakamani au polisi.
  Ukimuondoa Mbowe, viongozi waliokamatwa na kufikishwa mahakamani au polisi, ni Godbless Lema (mbunge wa Arusha Mjini), Philemon Ndesamburo (Moshi Mjini) na Joseph Selasini (Rombo).
  Wengine ni Meshack Opurukwa (Meatu), Tundu Lissu (Singida Mashariki), Esther Matiko (Viti Maalum) na Zitto Kabwe (Kigoma Kaskazini).
  Mbali na wabunge, viongozi wengine wa chama hicho wanakabiliwa na lundo la kesi mahakamani.
  Hao ni pamoja na Dk. Willibrod Slaa, katibu mkuu wa chama hicho, mwenyekiti wa mkoa wa Arusha, Samson Mwigamba na kiongozi wa ngazi ya juu katika Baraza la Vijana la CHADEMA (BAVICHA), Dadi Igogo.

  "Nakwambia kijana, yote haya yanafanyika kwa madhumuni ya kuidhoofisha CHADEMA. Haiwezekani kwamba mtu amejisalimisha polisi mwenyewe, azuiliwe kwa kisingizio cha kutekeleza amri ya mahakama," ameeleza mtoa taarifa.

  Amesema kukamatwa na kuwekwa rumande kwa Mbowe kumefanyika ili "kumdhalilisha yeye binafsi na kuwatisha wanachama na wafuasi wa chama chake."

  Amesema, "Mkakati huu umelenga kuwajenga wanachama woga na kuwafanya viongozi waliofunguliwa kesi kushindwa kutimiza majukumu yao kwa kuwa hadi uchaguzi mkuu unafika wanakuwa bize na kesi na hivyo wanashindwa kufanya kazi zao za kisiasa."
  Kukamatwa kwa Mbowe kumekuja wiki moja baada ya Jaji Mkuu wa Tanzania Bara, Othman Chande kuhudhuria semina elekezi iliyoitishwa na serikali mjini Dodoma.

  Haijafahamika mara moja kama kamatakamata hiyo inatokana na semina hiyo au imekuja kwa "bahati mbaya."
  Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Arusha, Charles Magessa ndiye aliyetoa amri ya kutaka Mbowe akamatwe kwa madai kuwa, si yeye wala mdhamini wake, waliofika mahakamani kueleza kilichowasibu siku kesi yake ilipotajwa tena.

  Tangu Januari mwaka huu, Mbowe na viongozi wenzake kadhaa walishitakiwa kwa tuhuma za kufanya maandamano bila kibali cha polisi.
  Gazeti hili limeelezwa na vyanzo vya uhakika kuwa Hakimu Magesa awali alikubaliana na hoja zilizotolewa mahakamani na mdhamini wa Mbowe ambaye alieleza kuwa alikuwa mgonjwa na si kweli kuwa hajawahi kufika mahakamani kwa muda mrefu.

  Baada ya maelezo ya mdhamini wa Mbowe, hakimu Magessa alikubali kufuta hati ya kumkamata Mbowe na aliridhia haja ya Mbowe pamoja na wabunge wengine wanaoshitakiwa pamoja kuruhusiwa kushiriki vikao vya bunge.

  Lakini katika hali ya kushangaza, jioni ya siku hiyo, hakimu Magessa alitoa uamuzi wa kukamatwa kwa mwanasiasa huyo mwenye ushawishi mkubwa.
  Taarifa zinasema ni baadhi ya maofisa wa mahakama waliopeleka taarifa za amri ya kumkamata Mbowe kwa wakili wake, Method Kimomogoro.

  Mara baada ya wakili Method kujulishwa kuwa hakimu Magessa ameendelea na msimamo wake wa kutaka Mbowe akamatwe, haraka alirudi mahakamani ambako inadaiwa alikuta hakimu ameshaondoka kazini.

  Taarifa zinasema hakimu alikwenda Babati kwenye harusi.
  Wakili Method ameelezwa kukutana na msajili wa mahakama. Naye msajili inaelezwa alipitia jalada la mwenendo wa kesi na kukuta, pamoja na kuwapo maelezo ya kutosha ya mdhamini wa Mbowe, hakimu Magessa bado aliamuru Mbowe akamatwe.

  "Baada ya kuona hivyo, msajili wa mahakama aliamua kuwasiliana na hakimu kwa simu yake ya mkononi na kumweleza kuwa alikuwa hajafuta amri inayomtaka Mbowe akamatwe. Akatakiwa kumuagiza hakimu kiongozi aliyepo kufuta amri hiyo ili kuondoa usumbufu kwa mhusika," anasema mtoa taarifa.
  Hata hivyo, mtoa taarifa anamnukuu hakimu akisema, "Nitakuja kushughulikia mwenyewe Jumatatu."

  "Unajua yule hakimu alifuta hati ya kukamatwa Mbowe. Lakini hakutoa uamuzi kimaandishi. Hivyo ikatolewa amri Mbowe akamatwe," ameeleza ofisa huyo wa mahakama mjini Arusha.
  Maelezo ya ofisa huyo wa mahakama yanafanana na yale yaliyotolewa na wakili Method, kwamba hakimu Magessa alijichanganya katika uamuzi wake.

  Mbowe alijipeleka mwenyewe polisi Jumamosi jioni na kuwa na mashauriano yaliyodumu kwa saa kadhaa kati yake, viongozi wa jeshi la polisi na wanasheria wa chama hicho, Mabere Marando na Lissu.

  Hata hivyo, baada ya makubaliano ya jinsi atakavyokwenda Arusha, imeelezwa kuwa aligeuziwa kibao na kushikiliwa hadi juzi Jumatatu alipofikishwa mahakamani mjini Arusha.
  Katika mashauriano hayo, viongozi wa polisi walikuwa wamekubaliana na maombi ya mawakili wa CHADEMA kuwa Mbowe aende mwenyewe mahakamani Jumatatu asubuhi, lakini kwa sharti kwamba aripoti katika kituo hicho cha polisi na kisha ataruhusiwa kuondoka.

  Wakili Marando amethibitisha kuwa kabla ya Mbowe kwenda kujisalimisha, kulifanyika majadiliano marefu kati yao na viongozi wa polisi; majadiliano yaliyolenga kutafuta njia mwafaka ya kumfanya kiongozi wao kufika Arusha bila bughudha.

  "Ni kweli tulikwenda polisi kufanya majadiliano ya jinsi mwenyekiti wetu atakavyofika Arusha. Tulifanya hivyo kwa nia njema. Hatukutaka mwenyekiti wetu kwenda kienyeji ili asije kukamatwa uwanja wa ndege au njiani wakati anakwenda Arusha na kisha ikatafsiriwa kuwa alikuwa anataka kukimbia," ameeleza Marando.

  Anasema, "Tulipokuwa katika majadiliano hayo, ndipo polisi wakaeleza kuwa makubaliano hayo hayawezi kufanyika bila mheshimiwa Mbowe kufika ili aonekane ameripoti polisi. Na sisi hatukuwa na pingamizi; tukafanya kama tulivyokubaliana."

  Habari zinasema baadaye, polisi wakionekana kama waliopokea amri kutoka juu, waligeuka na kumueleza Mbowe kuwa yuko chini ya ulinzi, jambo ambalo wakili Marando anasema linaonekana lilifanywa kwa shinikizo kutoka nje ya jeshi la polisi.

  Akizungumzia kukamatwa kwa Mbowe, Dk. Slaa alituhumu mbele ya waandishi wa habari, Jumapili iliyopita kuwa Rais Kikwete na chama chake wamesimama nyuma ya matukio yote ya kukamatwa kwa viongozi wa CHADEMA.
  Alionya kuwa chama chake kimechoka kunyanyaswa na kusema, "Hakuna wa kuzima moto tuliowasha."
   
 16. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #16
  Jun 11, 2011
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,238
  Likes Received: 3,673
  Trophy Points: 280
  Muda wao umekwisha hawa CCM a.k.a mafisadi,hakuna anaeweza kushindana na wakati!
   
 17. Mohamedi Mtoi

  Mohamedi Mtoi R I P

  #17
  Jun 11, 2011
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 3,326
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 0
  Hujma za ccm kwa chadema zitashindwa maana wananchi wana uelewa juu ya hiki kinacho endelea. Chadema na viongozi wote kwa ujumla wana taswira ya ukombozi, wakombozi wengi barani Afrika walianzia mahabusu, mahakamani na jela lakini baadae wakaja kukomboa mataifa yao.
  Ccm wasijidanganye wanachowafanyia viongozi wa Cdm kinawapa faida kwa wananchi kuliko wanavyofikiri.
   
 18. M

  Mwanaweja JF-Expert Member

  #18
  Jun 11, 2011
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 3,576
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  hawataweza wanawaongezea umaarufuu tu hakuna mtanzania mabaye bado yuko kwenye UHURU na zidumu fikira za mwenyekiti. tulishatoka huko hata wakiwafunga tutatokea wengine tutaendeleza mamapambano kama kawida. nguo ikichakaa hata ufanyeje kung'ara ni issue.
   
 19. NewDawnTz

  NewDawnTz JF-Expert Member

  #19
  Jun 11, 2011
  Joined: Nov 15, 2010
  Messages: 1,675
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  :A S clock:
  Why shouldnt they invest much kuhakikisha bibi yangu kijijini anasogezewa huduma karibu za afya?

  Washenzi wakubwa hawa, i wish i could shoot deia xxxx
   
Loading...