CCM wanunua shahada bandia za kupigia kura Moshi

mnduoeye

Senior Member
Jun 30, 2012
166
73
Ndugu wana JF,
Katika manispaa ya Moshi katika kata ya Kiborloni kutakuwa na uchaguzi mdogo baada ya Diwani wa kata hiyo ambaye pia alikuwa Naibu Meya wa Manispaa Bwana Vicent Rimoy kufariki.Uchaguzi huo utafanyika tarehe 9-2-2014.

Inavyoelekea mpaka sasa CCM wameelemewa kiasi cha kukosa kabisa wahudhuriaji kwenye mikutano yao ya hadhara.

Kama ilivy kawaida ya CCM wakaanza jitihada za kuhujumu uchaguzi ikiwa ni pamoja na kuwahadaa wapiga kura wauze shahada zao kwa sh 10,000 hadi 20.000 kutegemea na mwonekano wa mtu,jambo ambalo limelalamikiwa na Chama cha Demokrasia na maendeleo(CHADEMA).

Hata hivyo habari zimeenea tangu juzi kuwa kuna vijana wamechangamkia offer hiyo na ku -scan vitambulisho vya kupigia kura na kuwauzia CCM.

Kwa kuwa mazingira ya kuuziana ni kwenye giza na kazi hiyo inafanyika kati ya saa mbili hadi saa 4 usiku ,CCM wamejikuta wamenunua shahada zilizogushiwa na wauzaji watapiga kura kwa vitambulisho halali.

Mpango huu umeandaliwa kwa ustadi mkubwa na CHADEMA baada ya kugundua pasipo shaka kwamba CCM wananunua shahada za wapiga kura hasa nyakati za jioni na hakuna hatua zozote zinazochukuliwa dhidi yao hata ukutoa taarifa TAKUKURU hata Polisi.

Mategemeo ya wengi uchaguzi huu utawaliza sana CCM kutokana na ujanja huu waliofanyiwa huku wakiamini shahada walizo nazo ni halali.
 
Haahaaaa!CDM mmeshashinda,hiyo ya ku scan shahada na kuwauzia ccm, tuliitumia hapa Mwanza,kata ya Kirumba 2012,magamba wakaloa
 
Weka picha mkuu zipi hizo na sisi tuzione ili tujue nani muongo make siku hizi mnatunga habari kama hamana akili nzuri.
 
Hizi ni porojo nyepesi sana kwenye jamii yetu hii,
kwa sasa upeo wa watanzania upo juu sana huwezi huwezi kuwadanganya mara mbili mara tatu mpango wenu wa kupotosha tushawajua.
 
Ubunifu mzuri sana huo. Nawapongeza sana kwa ubunifu huo. Hizo ni fedha zenu mlizoibiwa na CCM heri mzile kwa staili hiyo
 
Hizi ni porojo nyepesi sana kwenye jamii yetu hii,
kwa sasa upeo wa watanzania upo juu sana huwezi huwezi kuwadanganya mara mbili mara tatu mpango wenu wa kupotosha tushawajua.

Ukiona ni porojo sina haja ya kubishana lakini ukweli uko palepale kuwa wameshalizwa na fedha imeliwa tayari na walengwa watapiga kura kama kawaida.
 
Cdm wanatafuta sababu 2, wakishindwa waanze kupiga kelele eti CCM wamenunua shahada Fanyeni siasa achen ujingaaaa.
 
Cdm wanatafuta sababu 2, wakishindwa waanze kupiga kelele eti CCM wamenunua shahada Fanyeni siasa achen ujingaaaa.

Acha wehu ccm haiwez kushinda kiborloni tena ndio makao makuu ya ndesa unaandika pumba mwizi n mwiz 2
 
Back
Top Bottom