CCM, Wanawaza kuboa upinzani si kuleta maendeleo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM, Wanawaza kuboa upinzani si kuleta maendeleo

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Big Dady, Aug 31, 2010.

 1. B

  Big Dady Member

  #1
  Aug 31, 2010
  Joined: Nov 10, 2009
  Messages: 59
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ''CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimeibomoa ngome ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Wilaya ya Mbeya Vijijini baada kuvuna wanachama 367 na viongozi saba wa chama akiwemo katibu wake wa wilaya.

  Ngome hiyo ya Chadema ilivunjwa baada ya mgombea urais wa CCM, Jakaya Kikwete kuwapokea wanachama hao akiwemo Katibu wa Chadema Mkoa wa Mbeya Ipyana Seme katika mkutano wa kampeni uliofanyika eneo la Mbalizi Mbeya Vijijini jana.

  Awali akiongea kabla ya kukamkaribisha Rais Kikwete, Katibu wa CCM Mkoa wa Mbeya, Verena Shumbusho alisema katika kipindi hicho cha kampeni, wamefanikiwa kubomoa ngome ya Chadema Jimbo la Mbeya Vijijini ambayo imekuwa ikiiumiza kichwa CCM.

  Alisema CCM imefanya kazi kubwa kuhakikisha ngome hiyo inavunjwa kwa kuhakikisha wanamnyakua mwanzilishi wa Chadema Wilaya ya Mbeya Vijijini.''

  Source: Mwananchi leo

  Hizi ndio siasa za kitanzania ambazo kila wakati CCM inawaza kubomoa ngome za wapinzani. Sijaona siasa za kijinga kama hizi, kweli katibu mzima wa CCM Mkoa anajisifu eti ''CCM imefanya kazi kubwa... xxnzy. Kweli demokrasia itajengwa hapa nchini?. Badala ya katibu huyo kueleza CCM Mkoa imewanyia nini wananchi alichoona cha maana ni kubomoa upinzani. Hayo ndio maendeleo? Hao waliohama sana sana wamatafuta fadhila sasa, wapewe u katibu nanihii wilayani, n.k. Poleni sana na njaa zenu.
   
Loading...