Ccm wanatumikia wananchi au wapo kupeana vyeo!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ccm wanatumikia wananchi au wapo kupeana vyeo!!!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Expedito Mduda, Nov 11, 2010.

 1. Expedito Mduda

  Expedito Mduda JF-Expert Member

  #1
  Nov 11, 2010
  Joined: Sep 22, 2009
  Messages: 368
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  Jamani nahisi kila mmoja wetu ni shahidi wa kazi ya bunge iliyofanyika na bunge lililopita chini ya mheshimiwa Samuel Sitta.
  Bunge lililopita lilifanya kazi nzuri na hasa ile ya kuruhusu mijadala motomoto kwa maslahi ya taifa letu. Ni bunge ambalo liliwafanya watu waelewe maana ya ufisadi. Bunge hilo lilikuwa la kiwango cha juu kiasi chake. Mheshimiwa sana Sitta hakukipendelea chama chochote na wala hakuwa mnafiki.
  CCM baada ya kuona Sitta aliwatumikia wananchi kwa mafanikio hayo na kwa kuwa majadiliano hayo yaliyoruhusiwa na Sitta yalikuwa yanawaumbua mafisadi, wameamua kumuweka mtu wao atakayesaidia kuficha uovu unaofanywa na hao mafisadi.
  Tanzania amini msiamini imeingiliwa na mdudu mtu anatafuna huku na huko alimradi tu kuhakikisha wachache wanaokula nchi hii wanaendelea kula bila pingamizi lolote.
  NNakumbuka huyu mtu wanayeteka kumweka anayeitwa Anne Makinda ndiye aliyempinga Dr. Slaa alipopendekeza mishahara ya wabunge ipunguzwe na nakumbuka alicheka kwa kebehi sana tu! Huyu mama anayewekwa ni kwa maslahi ya nani: Mafisadi au wananchi? Wanataka bunge liwe linajadili maslahi ya mafisadi badala ya kujadili mambo yanayohusu mastakabali wa taifa letu na kuwafichua mafisadi. Wamamchagua mtu aliyesema hata mishahara ya wabunge ikipunguzwa hakuna kitakachoongezeka kwa mfanyakazi wa chini. Huyu hesabu hiyo aliitoa wapi jamani!
  Eti wanataka kulinyamazisha bunge! mimi naomba sana wabunge wenye uchungu na nchi yetu wamtupilie mbali huyo mama maana hana hoja yoyote kama tulivyoona wakati ule akiwa naibu spika. Sisi Watanzania wenye nchi yetu tunaomba mchague spika atakaye ruhusu mijadala motomoto ili kulinusuru taifa letu na uporaji unaofanywa na mafisadi hawa wasio na aibu kabisa.
  Suala la jinsia si hoja kabisa! Hapa tunataka mtu anayeweza kuliongoza bunge lijadili mambo ya msingi ya taifa letu. Awe mwanamke au mwanaume sawa lakini awe na uwezo huo.
  Kwa kuwa wenzetu wa CCM tayari wamempendekeza mtu asiye na uwezo tunaohitaji, sisi tumchague mtu mwingine mwenye uwezo huo.
  Jamani maslahi ya taifa mbele ubinafsi shimoni. Tunawaomba wabunge wote wenye nia ya kuwatumikia wananchi kwa moyo wao wote wawe CCM au CHADEMA au CUF, chagua mtu mwenye uwezo wa kuwaongoza mjadili mambo muhimu na yale ya kufichua mafisadi popote walipo.
   
 2. Expedito Mduda

  Expedito Mduda JF-Expert Member

  #2
  Nov 11, 2010
  Joined: Sep 22, 2009
  Messages: 368
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  Watanzania tuone kama si Wadanganyika!! Anna Makinda ndiye spika wa wabunge wenu mliowachagu badala ya muungwana Samuel Sitta baba wa viwango!
  MNASEMAJE?
   
 3. Mwanamageuko

  Mwanamageuko JF-Expert Member

  #3
  Nov 11, 2010
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 3,796
  Likes Received: 1,294
  Trophy Points: 280
  Labda Anne, Anna au Kate wana kiwango kuliko cha mzee wa Urambo :smile-big:
   
 4. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #4
  Nov 11, 2010
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,603
  Likes Received: 4,709
  Trophy Points: 280
  CCM ni maharamia na manyang'au wanagawana nyara.MLALAHOI YOYOTE ANAYEWAUNGA MKONO CCM LAZIME APIMWE AKILI.
   
 5. Ehud

  Ehud JF-Expert Member

  #5
  Nov 11, 2010
  Joined: Feb 12, 2008
  Messages: 2,696
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  CCM wanatumikisha wananchi siyo wanatumikia wananchi
  :A S angry:
   
Loading...