CCM wanategemea kura za nani kushinda uchaguzi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM wanategemea kura za nani kushinda uchaguzi?

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by MANI, Aug 17, 2010.

 1. MANI

  MANI Platinum Member

  #1
  Aug 17, 2010
  Joined: Feb 22, 2010
  Messages: 6,409
  Likes Received: 1,862
  Trophy Points: 280
  Jamani Waungwana wezangu mimi nashindwa kuelewa matamshi ya viongozi wakuu wa CCM kuelekea uchaguzi mbona hayaendani na chama kinachotegemea sanduku la kura kupata ushindi. Mwenyekiti wao alisema hahitaji kura za wafanyakazi kwa hiyo hawezi kuwaongezea mshahara hata kama hawatampigia kura, jana makamu mwenyekiti wao amesema wale wote ambao wanaona hawakutendewa vyema kwenye mchakato wa kupitishwa kuwania nafasi mbalimbali za uongozi wanaweza kuondoka pamoja na wafuasi wao. Sasa kama chama kinachoingia kwenye ushindani wa kura kinaanza kuwakataa wapiga kura kwamba hakina haja nao je wenzetu wana mbinu gani nyingine wanazotumia kushinda!
   
 2. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #2
  Aug 17, 2010
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,632
  Trophy Points: 280

  Mkuu CCM wantegemea kura za maruani
   
 3. b

  blackpepper JF-Expert Member

  #3
  Aug 17, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 382
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  hawa wanahitaji kususiwa na wapiga kura wote mwaka huu
   
 4. M

  MC JF-Expert Member

  #4
  Aug 17, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 751
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  Kama ulisoma enzi zile, kipindi cha mwalimu, enzi zile hata Kiranja Mkuu wa Shule ya Msingi anaongoza kwa busara na uwajibikaji kuliko viongozi wetu wengi wa sasa, nadhani utakumbuka hadithi ya 'Sizitaki Mbichi hizi'
   
 5. Mlachake

  Mlachake JF-Expert Member

  #5
  Aug 17, 2010
  Joined: Oct 13, 2009
  Messages: 2,920
  Likes Received: 619
  Trophy Points: 280
  Hawa jamaa wamekosa utashi. ila ipo siku.
  wanakiburi sana. tena sana. unajua kwanini?
  system ya utawala wa sasa.
  ukianzia yule mjumbe wa nyumba Kumi ni sisiemu.
  kuibadilisha hii itatuchukua muda kaka.
  kwahiyo wana uwezo wa kuropoka lolote lile kwasababu wana uhakika na kura.
   
 6. M

  MzeePunch JF-Expert Member

  #6
  Aug 17, 2010
  Joined: Jun 8, 2009
  Messages: 1,412
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Wallah safari hii wataumbuka. Ngoja akina Slaa, Zitto, Mbowe, Marando, Tundu Lissu na wengine waanze kumwaga 'sumu' huko vijijini.
   
 7. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #7
  Aug 17, 2010
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,823
  Likes Received: 10,120
  Trophy Points: 280
  za sheikh yahaya
   
 8. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #8
  Aug 17, 2010
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  ccm inategemea kura aina ifuatayo kushinda.
  1. Kura za wizi.
  hapa wanajiandalia kucheza na ballots, wataiba ili kuwezesha kura zao zitoshe, hapa watawatumia wakuu wa wilaya, wakuu wa mikoa na makada wezi wazoefu kama kina Kingunge na makada wenzao.

  2.kura za wasio piga kura.
  hili ni kundi kubwa la wapenda mageuzi wasio piga kura, wengi wao wako miji mikuu, hasa Dar es salaam , Morogoro , Mwanza na mikoa mingine mikubwa, kwao kupiga kuraa ni jukumu la wajinga, wasio soma, na wala wasio na kazi, wao wako busy kila siku, wanadhani ukombozi ni jukumu la kundi fulani la watu.

  3. kura za Wazee na waoga wa mageuzi.
  hawa ni wale watu wanaogopa mageuzi, wanaminishwa kuchagua chama tofauti na ccm ni kumkana JK Nyerere,RIP.
  WANAONYESHWA FILAMU ZA VITA BURUNDI NA RWANDA , huku wakiaminishwa kupitia Channel 10, TBC, Uhuru FM, Daily News, uhuru na Mzalendo kuwa , wapinzani ni chanzo cha vita.

  4.Kura za wasomi mamluki.
  hawa walikuwepo hata uchaguzi wa mwaka 2005, wengi wao walikwenda kula pilau pale Diamond Jubelee, wakihadiwa kulipiwa ada kwa 100%, wakatoka pale wameshiba wakiimba ccm nambari one, Nguvu mpaya kazi mpaya.
  hawa ni wajinga ingawa wapo vyuo vya elimu ya juu, elimu yao haijawasaidia kuondokana na ujinga, hata wakuchanganua ujinga mwepesi kama huo.

  5.Kura za waarabu, Wahindi na foreigner.
  hawa ni wengi sana, kuna wasomali kemkem wanaishi kiholela hapa Tz, wako Tanga, wako Temeke DSM, WAKO kILIMANJARO NA aRUSHA,
  KUNAwahindi, WAO na familia zao, wamenufaika na utawala legelege wa ccm, wanafuja mali zataifa hili kama vichaa, wengi hawana uraia wa TZ, ingawa wana vitambulisho vya kupigia kura, wengi wamechanga mamilioni kusaidia kampeni za kina makamba na ccm yao, ni waoga wamageuzi, wanaogopa kupata mtawala mfuata sheria, maana watakua hatarini kunaswa na mkono wa sheria.

  kufikia hapo ccm itakua na kura millioni 4. hizi wanazo tayari, wanatafutia za kujazia , kutegemea na kazi ya kampeni na mvuto wa mgombea wao kama anao bado, na mvuto wa wabunge kama kina Mwakyembe, kuweza kumpatia kura za wanaKyela Kikwete.
   
 9. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #9
  Aug 17, 2010
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,823
  Likes Received: 10,120
  Trophy Points: 280
  na kura za wafu..si mliona wale waliopiga kura juzi kwenye kura za maoni
   
 10. MANI

  MANI Platinum Member

  #10
  Aug 17, 2010
  Joined: Feb 22, 2010
  Messages: 6,409
  Likes Received: 1,862
  Trophy Points: 280
  2.kura za wasio piga kura.
  hili ni kundi kubwa la wapenda mageuzi wasio piga kura, wengi wao wako miji mikuu, hasa Dar es salaam , Morogoro , Mwanza na mikoa mingine mikubwa, kwao kupiga kuraa ni jukumu la wajinga, wasio soma, na wala wasio na kazi, wao wako busy kila siku, wanadhani ukombozi ni jukumu la kundi fulani la watu.


  Ndugu yangu Nguvumali ulichokisema hapa kimeniuma sana kwa kuwa ni kweli nadhani kuna swala kama hili amelileta mkuu Mwanakijiji sasa sisi tunaojua umuhimu wa kupiga kura nadhani ni wajibu wetu mwaka huu kuwaamsha hawa ili mapinduzi ya kweli yawepo.
   
 11. mfianchi

  mfianchi JF-Expert Member

  #11
  Aug 17, 2010
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 7,948
  Likes Received: 1,505
  Trophy Points: 280
  Pia waseme hata wale wanachama waliowapigia kura wale wanaolalamika pia waondoke ,hawana haja nao au sio
   
 12. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #12
  Aug 17, 2010
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  katika ujumla wake, upinzani unahitaji kuendelea kuelimisha umma , juu ya umuhimu wa kupiga kura, na kuelezea namna kura moja ilivyo na thamani, J2 Niliona kipindi kimoja kizuri EATV kikihamasisha vijana kupiga kupiga kura.
  kidogo kidogo vijana wataamka, watambukizana tabia, Nilikua Kenya wakati wa kura za maoni amini usiamini , kule watu wako proud kupiga kura, hakuna anaetamani kukosa,
  ELIMU BILA KIKOMO JUU YA UMUHIMU WA KUPIGA KURA ITALIOKOA TAIFA.
   
 13. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #13
  Aug 17, 2010
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Aina nyingine ya kura ni. Kuwadiscourage watu kupiga kura katika maeneo yenye upinzani mkali kwa kuchelewesha vifaaa na kufungua vituo late, halafu zoezi kwenda mwendo wa jongoo. Mtu atakayepiga kura itabidi asimame kwenye msitari masaa matatu mpaka manne.
   
 14. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #14
  Aug 17, 2010
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  asante sana, hizo ni kura zingine , tena wanazitumia sana kwenye maeneo yenye upinzani mkali, kumbuka Ubungo 2005, kumbuka uchaguzi wa DSM mwaka 1995, ni mbinu yao, wanajitengeneza ghost vote, kisha wanatangaza kufutwa uchaguzi , iliwahi kutokea ZNZ, KISHA CUF wakasusa.
   
 15. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #15
  Aug 17, 2010
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,604
  Likes Received: 4,730
  Trophy Points: 280
  Kura za wizi. Hawa wezi ,majambazi ,mafisadi, mashetani...................
   
 16. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #16
  Aug 17, 2010
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  sema tena kwa sauti
   
Loading...