Kessy Wa Kilimanjaro
JF-Expert Member
- Jan 23, 2016
- 327
- 208
Tangia uhuru wa Tanzania tumepewa msaada wa zaidi ya mabilioni ya dolla za kimarekani ili kujenga nchi yetu. Je hiyo hela imeenda kwenye kujenga barabara ambazo magari yanaanguka kwenye mashimo kila siku, au kwenye kununua madawati ambayo yanakosekana, au hiyo hela imeenda kwenye kununua vitanda muimbili, au imeenda kwenye kukuza elimu ambayo kwenye kusoma tuko namba 82 kati ya 112, au hiyo hela imeenda kwenye kusaidia vijiji ambavyo bado vinaishi kwenye nyumba za matope.
Lakini ambacho kinashangaza ni kwamba bado hawa wanasiasa na viongozi wana hamu ya kupendekeza sera ambazo zinazidi kuwafukuza wafanya biashara, kufanya uwekezaji wa wamaskini kwenye biashara uwe mgumu, kuongeza kodi, kuongeza wizara, kuongeza sheria kwenye uwekezaji, kuongeza leseni zinazohitajika kuanzisha biashara, kuongeza vikwazo kwenye mabenki na maisha ya watu binafsi.
hivi kweli hawa viongozi wetu wanajidai kama hawajui madhara ya wanachofanya?
Ukweli ni kwamba wanajua na wanafanya maksudi. Sababu ni kwamba wanapenda urahisi wa hela za misaada. Hela za misaada zinakuja pale kukiwa na shida. Sasa fikiria, hawa viongozi wangetumia mbinu ambazo wanajua zinaleta mazao na zimeonyesha kuleta maendeleo kwenye nchi zingine, na wangejenga uchumi kwenye kiwango cha kupunguza umaskini mpaka wale wanaotuma misaada wakaona hamna haja tena, si watakuwa wanajiharibia utajiri wao wenyewe. Misaada ingeanza kupungua na wao wangeshindwa kuiiba na kuificha kwenye account swiss bank account zao. Kama hamniamini waulizeni viongozi wenu kwanini tusiache kuchukua misaada utaona watakavyo badilika sura kama umewatukana.