maganjwa
JF-Expert Member
- Sep 11, 2012
- 2,806
- 2,349
Shughuli ya kubadili vifungu vya sheria pamoja na minongono ya chini kwa chini ya kubadili katiba ikichagizwa na baadhi ya wabunge pamoja na spika siyo ya kupuuzwa. Waswahili walisema lisemwalo lipo kama halipo linakuja.
Mimi nasema hilo iko wazi kabisa na maandalizi imeanza leo Dodoma kuwaingiza watu wasio na sifa kisheria kuwa wanasheria wa kiwango cha mawakili hayo yote yanafanywa kumlenga nani? Kuna watu wanalengwa na kwa sababu za kisheria hawawezi kuwa mawakili kwa hiyo siku wakishamaliza yao, hao watu watakuwa viongozi wakubwa serikalini na kazi yao ni kufuata maelekezo ya aliyewasaidia kuwa pale.
Haiingii akilini kutoa upendeleo kwa jambo la kisheria ambalo limewekwa ili kuwa na weledi katika fani ya sheria kwa hiyo shughuli hii inayoendelea dodoma inanajisi tasnia ya sheria Tanzania.
Baada ya hapo kuna kazi kubwa inakuja Novemba ya kuwa na bunge la chama kimoja cha siasa CCM na ndipo itakapofanyika jambo kubwa la kihistoria. Watu wanajaribu kubisha bisha lakini mimi nawauliza watanzania walishakataa nini wakashinda.
Mkinipa jibu kwa swali langu hilo wanayowaza yanaweza kufeli. Kwangu mimi kama sio kutania na wamedhamiria kweli basi imepita siku nyingi sana sheria hiyo ya kumpa mkulu zaidi ya miaka kumi.