CCM wanagawa fedha kwa vijana ili kuwarubuni wajiunge na chama hicho na kuwashawishi wawaunge mkono kwenye uchaguzi wa serikali za mtaa Mbezi Makabe.Harakati na mipango yao dhalimu wameanza kuifanya kitambo. Waliitisha mkutano wa dharula wiki moja iliyopita,mkutano ulidoda. Jana wakasambaza ujumbe kwa vijana kwamba wakutane jioni kwa mjumbe na kada wa Chadema kamanda Rama,almaarufu Ba'Dula.Walisema kada huyo anagawa fedha za Chadema.Vijana wakamfuata ili kuhoji kulikoni Chadema kugawa fedha! Sio utamaduni wa Chadema kufanya mambo ya kifirauni! Vijana wakiwa hapo kwa Ba'Dula wakaambiwa mwenyewe hayupo na wala hajui jambo hilo.
Ndipo mara wakaona gari la kada wa CCM ndg Sharifu linawasili hapo.Akatelemka ndg yake Ba'Dula. Vijana walipoona hivyo wakatawanyika.Baadaye,ilikuja julikana kwamba CCM wamekuwa wakigawa fedha kwa vijana tangu wiki iliyopita ili kuwavuta vijana wajiunge na kwenda kwenye mikutano ya chama chao.Mbinu hizo zimekwama.Kwa hiyo,wakaona watumie mbinu ya kuwaita vijana kwa kada wa Chadema kwamba ingerahisisha kuwapata vijana. Hilo limekwama maana Ba'Dula aliwajulisha vijana kwamba hakuwepo nyumbani muda ule na wala hakujua kinachoendelea akawataka vijana kutawanyika wasijihusishe na uzandiki huo wa kifisadi.Hali kwa jumla ni mbaya sana kwa CCM katika eneo la Mbezi Makabe. Vijana wengi wameikataa CCM.
Katika uchaguzi mkuu wa 2010 mgombea udiwani kwa tiketi ya CCM aliambulia kura 30 kati ya kura elfu kadha za mgombea udiwani wa Chadema kwa kura zilizopigwa katika kituo cha Shule ya Msingi Makabe.UKAWA huko Msumi.Wakati huo huo, katika eneo la Msumi CCM wamewafuata wafuasi wa CUF wakiwashawishi kwa fedha na kwa ahadi nyingi, huku wakitumia sera zao za ukanda na udini kwamba wasikubali Chadema kusimamisha mgombea kwa kiti cha mwenyekiti wa mtaa wa Msumi. Wanatumia mbinu hizo ili kuwagawa wananchi katika uchaguzi ujao.Njama hizi zimejulikana kwa sasa viongozi wa CUF na Chadema wanalifuatilia jambo hili kwa ukaribu.
Huko Msumi hali ya CCM nako ni tete, CUF na Chadema ni vyama vinavyokubalika zaidi eneo hilo.