VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,140
- 18,007
Hapa Lumumba,ofisi ndogo za CCM Dar, sasa ni vikao mfululizo. Kamati mbalimbali zinaundwa na kupewa majukumu mbalimbali lakini yenye lengo moja:kuiadhibu Mtwara. Kwanini waandamane kupinga kuisafirisha gesi toka huko Mtwara hadi Dar es Salaam? Kwanini wamsaliti Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa nchi? Wapo Wajumbe wenzangu wanawaita Mtwara wahaini na wasaliti.
CCM imeapa kuidhibu Mtwara. Wanakamati tumepewa kazi ya kutafuta adhabu mujarabu na kuishauri Serikali. Nitakuja kuwaambia adhabu husika baada ya Kikao cha Jumatatu. Hali ni tete hapa Lumumba.Tutaonana siku hiyo.Jadilini lakini mjue hivyo
Wenu,
VUTA-NKUVUTE aka Mzee Tupatupa
listen to JaH LIVE song - by Bob MarleyUkiona mbwa anabwekea ndege wapitao angani ujue huna mbwa hapo ni mjinga tu.
Mchawi wa ccm ni ccm yenyewe
aidha Watanzania hatujui siasa, ama tuliowapa dhamana za uongozi wa siasa hawajui wajibu wao. Maana hizi vuta-nikuvute zimekuwa mara zinatutupa huku, mara zinatutupa kule kiasi kwamba Watanzania tumesahau kupambana na maadui wa maendeleo yetu.
Ona kwa mfano hii taarifa ya VUTA NIKUVUTE aka Mzee Tupatupa inaonesha Chama kinachoongoza serikali hakina mpango wa kuhakikisha Wanasayansi wa Tanzania wanaenda Mwezini achilia mbali kuhakikisha neno "umasikini" linakuwa historia, kwa mujibu wa taarifa hii CCM inajiwinda kuwaadhibu wananchi masikini wanaohoji namna watakavyo faidika na rasilimali zao za asili, sio tu ni aibu wanaMtwara kuogelea kwenye lindi la umasikini kwenye serikali inayojigamba kuongoza kwa ufanisi, bali ni kinyaa kwa serikali inayojiita makini kuwatishia wananchi wake yenyewe. Haya mambo yanaashiria udhaifu mahali fulani, kama sio kwa wananchi, basi kwa serikali ama kwa chama kinachoongoza serikali.
Umenena mkuu!
Hii serikali imeshasahau ya kwamba cheo ni dhamana!
Wamejisahau ya kuwa wapo madarakani kutokana na kura za hao hao wanaotaka kuwaadibisha.
Watanzania amkeni, ccm haiko kwa ajili yenu.
Ondoeni uozo huu muone angalau harufu ya mabadiliko.
Mpira uko kwetu wana Mtwara na watanzania wote!
Haitakuwa rahisi lakini hatuna budi kuanza.
Hata TANU ilipoleta uhuru kuna waliotia mashaka kama ingewezekana, lakini sauti ya yule, mimi na wewe ikamtoa mkoloni.
Mungu Ibariki Tanzania na watu wake!
lakini sauti ya yule, mimi na wewe ikamtoa mkoloni.