CCM wamkemea January Makamba

CCM wamkemea January Makamba

BAK

JF-Expert Member
Joined
Feb 11, 2007
Posts
124,769
Reaction score
288,283
CCM wamkemea January Makamba

08/07/2014 | Posted by Mwandishi Wetu

KAULI ya Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba, ya kuwataka wazee waachane na mbio za urais 2015 kwa madai kuwa ni zamu ya vijana, imeelezwa kuwa ni ya kibaguzi na matusi.

Chama Cha Mapinduzi (CCM), Wilaya ya Shinyanga mjini, kupitia kwa Katibu Mwenezi, Charles Shigino, kimesema kuwa kauli hiyo ya Makamba inaleta siasa za ubaguzi ndani ya chama.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Shigino alisema kuwa CCM inapiga vita suala la ubaguzi wa aina yoyote ile kwa binadamu, na kwamba kauli ya Makamba inaweza kuleta hatari kwa mustakabali wa chama.

Kwa mujibu wa Shigino, kauli ya Makamba ambaye pia ni mbunge wa Bumbuli, ni ya kuwabagua wazee kuwa fikra zao hazifai na kuongeza kwamba ni sawa na kuwatusi, hivyo anapaswa kuwaomba radhi.

“Tunamwomba Makamba atambue kuwa ujana sio kigezo cha kuiongoza jamii ya Kitanzania na hasa katika nafasi nyeti ya urais. Ni bora akajifunza kutoka kwa wazee waliokwishawahi kuiongoza nchi.

“Kama kweli Makamba ana nia ya urais, ni bora akajipa muda wa kujifunza na kupata uzoefu wa kutosha wa nafasi hiyo, kwani Watanzania wanajua bila ubishi kuwa ndani ya CCM hana muda wa zaidi ya mwaka na nusu katika uongozi,” alisema.

Shigino aliongeza kuwa Makamba ni kijana mdogo kisiasa, ambaye anatakiwa kwenda kujifunza kutoka kwa wazee waliopo ndani ya CCM, ambao amekuwa akiwadharau.

Wakati huo huo, Gordon Kalulunga anaripoti kutoka Mbeya, kuwa tatizo kubwa kwa baadhi ya vijana wa chama hicho (UVCCM), wanatumika vibaya na wagombea na kukisemea chama bila utaratibu.

Katibu wa Siasa na Uenezi wa CCM, Mkoa wa Mbeya, Bashiru Madodi, aliyasema hayo katika Ukumbi wa CCM Mkoa wa Mbeya juzi, wakati wa Baraza Kuu la UVCCM mkoa, ambalo lilifanyika kwa mujibu wa kanuni za umoja huo kwa ajili ya maandalizi ya kumwapisha Kamanda wa Vijana Mkoa wa Mbeya, Yona Sonelo na makamanda wa wilaya tisa za mkoa huo.

Akionekana kama anamjibu Katibu wa Hamasa wa UVCCM Taifa, Paul Makonda, ambaye hivi karibuni ametoa tamko kuwa Waziri Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa hafai kuwania nafasi ya Rais wa Tanzania, Madodi alisema inashangaza vijana kwenda mbio na kutoa matamko ambayo yanapaswa yatolewe na vikao vya chama kwanza.

Alisema kuwa vijana wengi wanatembea na wanaotaka madaraka kutokana na kuwa ndio tegemeo la taifa, kwa sababu wanaweza kukimbia huku na kule.
“Ni kipindi kigumu sana kwenu, wakati wetu kina Guninita waliwahi kufutwa uongozi kutokana na tabia zinazofanana na vijana wa leo. Mnatoa matamko bila hata vikao vya chama kutoa maamuzi,” alisema huku akishangiliwa.

Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji UVCCM Mkoa wa Mbeya kutoka Wilaya ya Momba, Hassan Nyalile, aliiambia Tanzania Daima kuwa anaunga mkono kauli ya Madodi akisema ni ya kiungozi, na kuongeza kwamba Makonda anatakiwa kujirekebisha na kurudi kwenye majukumu yake.

“Makonda anatakiwa atafsiri vema kauli ya Madodi na kurejea kwenye misingi ya kanuni ili aweze kufanya vema kazi za jumuiya yake ya watoto, badala ya kila wakati kuinuka na kutoa matamko ambayo yanaashiria yupo na kiongozi mmoja mfukoni kutafuta nafasi ya rais mwaka 2015,” alisema.
Makonda ambaye alikuwepo kwenye baraza hilo, ndiye aliyeanza kueleza kuwa vijana wapo ndani ya mifuko ya wanasiasa wakubwa, ndiyo maana inafikia mahali chama hakiwaamini.

Alisisitiza kuwa kuna baadhi wanaomtuhumu kuwa yeye anatumwa na kundi la watu kutoa matamko, jambo ambalo si la kweli, bali anaongozwa na akili zake mwenyewe na kwamba madhara ya magenge ni kujitafutia riziki binafsi.
 
Sidhani kama ni bahati mbaya au hajui afanyalo!!!!
 
Ilikua zamu ya 'wanawake' wakamtupa nje ya ulingo mtu anayefaa kua speaker...sasa eti zamu ya 'vijana' ili wamtupe nje ya ulingo mtu anayefaa kua rais. Mbaya sana kijana anayejinadi ni bomu.
 
watavurugana sana
 
ma'ccm yanacheza na akili za watanganyika sana.
 
Ccm hakuna jipya,wote ni ukoo wa panya na kambale kila mtu anaweza fanyalolote atakalo.
 
Ilikua zamu ya 'wanawake' wakamtupa nje ya ulingo mtu anayefaa kua speaker...sasa eti zamu ya 'vijana' ili wamtupe nje ya ulingo mtu anayefaa kua rais. Mbaya sana kijana anayejinadi ni bomu.

Kama ilivyo vigumu Serikali kuhamia Dodoma ndivyo ilivyo vigumu kwa J.Makamba Kuwa Rais na wakijichanganya tu wakampa nafasi January Makamba watambue Kuwa Upinzani wataingia ikulu kiulaini .
 
Huyu bwana Makamba baba yake alipokuwa anaongoza akiwa na umri mkubwa kwanini hajasema lolote. He's hypocritical individual and residue for this country.
 
Njia rahisi ya kupitia kuelekea ikulu ni hii January Makamba ,wapinzani wanaombea usiku na mchana ili apitishwe watumie fursa hiyo kuichukua Nchi kiwepesi na kwa speed ya 120, Mtu pekee ndani ya ccm mwenye uwezo wa kushinda kwa kishindo ni E.L pekee wengine labda wategemee miujiza.
 
Umeona eeh!!!! Juzi juzi aliadhibiwa huyu pamoja na akina Membe, Sumaye na Lowassa. Ngoja tusubiri tuone adhabu yake mpya baada ya kukiuka masharti ya MACCM ambayo aliwekewa.

ma'ccm yanacheza na akili za watanganyika sana.
 
Very good in deed,Makamba km km JK na anayeishi maisha ya JK yaliyochokwa na watz, na sifa alizojipa ni kuonyesha kuwa atafanya anayofanya JK.Makmaba Dini yake na walichojenga ktk nchi kuwagawa watz kwa minajili ya dini,sidhani km atawashawishi sana watz.
 
GONGO is talking now!

Teh teh teh teh!
 
Vijana ndo wengi kwa taifa letu, lakini kumpa kura mtu/mgombea kwa sifa tu ya ujana haifai! Tunayona leo kwa jk!
 
Kama ilivyo vigumu Serikali kuhamia Dodoma ndivyo ilivyo vigumu kwa J.Makamba Kuwa Rais na wakijichanganya tu wakampa nafasi January Makamba watambue Kuwa Upinzani wataingia ikulu kiulaini .

CCM kwa ujuzi wa kuiba kura sintashangaa akishinda.
 
Kama ilivyo vigumu Serikali kuhamia Dodoma ndivyo ilivyo vigumu kwa J.Makamba Kuwa Rais na wakijichanganya tu wakampa nafasi January Makamba watambue Kuwa Upinzani wataingia ikulu kiulaini .

Mkuu hakuna chaguo litakalo inusuru CCM hata wachague nani 2015 ni rahisi kwa Ngamia kupenya kwenye tundu la sindano kuliko CCM kuingia tena Ikulu " MAY BE OVER OUR DIED BODIES"
 
Pyuu!
kama bata kanya.
kachukue posho yako Ufipa.
 
Back
Top Bottom