Msema yote
JF-Expert Member
- Mar 19, 2013
- 448
- 301
Miaka 53 ya CCM kutumia rasilimali zetu kunufaisha watawala na kuwanufaisha wawekezaji inatosha, ni muda sasa WATANZANIA tuamke na tuikatae CCM. Tunatakiwa kutambua kuwa adui yetu ni CCM kwani ndio chama chenye sera na ilani mbovu za unyonyajii zenye kubeba wageni na kukandamiza wazawa.
Tuweke akilini kuwa kamwe hapatatokea kiongozi mzuri ndani ya CCM, miaka kumi iliyopita CCM ilimpa dhamana Mh. Jakaya Mrisho Kikwete kupeperusha bendera ya CCM kuwania urais wa jamhuri ya muungano wa TANZANIA, wananchi wengi wakawaamini ndiye chaguo la Mungu na kuanza kumbatiza majina ya kila namna yenye kumsifia, baadhi ya viombo vya habari vilimsifia sana kwa kumpampa kwa maneno mazuri ya kuvutia, mfano kuna chombo kimoja cha habari kilicho meng'enyua jina lake kwa lengo la kumsifia kwa namna hii,
K- Kiongozi
I- Imara
K- Kapatikana
W-Watanzania
E- Endelezeni
T- Taifa
E- Endelevu.
Leo sasa ni miaka 10 imeisha kila mmoja wetu ni shahidi kwa hali ilivyo nchini, hali ni mbaya kuliko maelezo hata vile viwanda alivovikuta angalau vilikuwa vinaungurumia mlima kitonga sasa havipo kabisa, kwao sifa wanayojipa ni kupeleka umeme mpaka vijijini sasa mimi najiuliza wanataka umeme uwake kwenye nyumba ya nyansi? Kwani kwa garama za ujenzi mtanzania wa kawaida hawezi mudu. Hata hivyo bado garama za umeme zipo juu kama mtanzania mmoja anaishi chini ya dola moja maana yake hawezi mudu garama za umeme huu ni utapeli mkubwa na ni kutufanya watanzania wajinga.
Baadhi ya wanawake walisema "mgombea wa CCM handsome, kijana, ana kifua kizuri, mweupe, chotara." kwa sifa hizo tu zikawafanya wao kumchagua sasa leo ni miaka kumi hizo sifa hazijasaidia chochote wanawake hao zaidi ya kudanganywa na msemo wa HAKI SAWA ukiboreshwa na kibwagizo cha "wanawake wakiwezeshwa wanaweza", huku wakiwapa wezi wenzao wa jinsia ya kike vyeo kwa lengo la kuwarubuni mama na dada zetu, baadhi ya wezi hao wa kike ni:-
Asharose Migiro – aliyeshindwa utendaji umoja wa mataifa akarudi nchini na kupewa jukumu la
uchakachuaji wa maoni ya wanachi juu ya katiba, kwa kofia ya UWAZIRI
WA KATIBA NA SHERIA.
Samia S. Hassani- alikuwa mwenyekiti msaidizi bunge la katiba akishiriki kikamilifu kufukia
shimoni rasimu ya warioba iliyokuwa na maoni ya wanachi na sasa amepewa
shukrani ya mgombea mwenza.
Anna Tibaijuka- alikuwa waziri mwenye kiburi wizara ya nyumba na makazi akajimilikisha
maeneo makubwa na kushiriki kikamilifu wizi wa pesa za umma kwa mgongo
wa ESCROW, wizi umemfanya kuwa na kiburi sana anaamini milioni kumi
ni pesa ya mboga, hayo ni matumizi mabaya sana na ni kutaka kutuaminisha
kuwa kumbe wanawake hata bajeti kupanga hawajui?
Anna Makinda- spika wa bunge la kumi aliyepewa dhamana hiyo kwa lengo mmoja tu
kudidimiza upinzani, pamoja na kupewa cheo hicho akiwa kama mwanamke
hakuna mwanamke yoyote nchini aliyenufaika na uwepo wake hapo kwani
hata hoja za muhimu zilizo hitaji upatikanaji wa madawa, ujenzi wa wodi,
uwezeshaji kiuchumi kina mama alikuwa anazipotezea kisa tu zimeletwa na
upinzani. Alitaka kutetea wezi wa ESCROW wasiadhibiwe huku akijua kuwa
pesa zile zilizo ibiwa zilitosha kujenga hospitali za wanawake na watoto zaidi ya
40 nchi nzima, Shukrani ziwaendeee wapinzani kwa kusimama kidete dhidi ya
wezi wote wa ESCROW japo mpaka leo serikali imepiga kimya
Ikumbukwe kuwa kupitia CCM vyombo vya usalama ikiwemo jeshi la polisi, usalama wa taifa, jeshi la wananchi vimepoteza mwelekeo na kusahau majukumu yake kikatiba na badala yake kushiriki na kutetea ubadhilifu unaofanywa na CCM, ni jeshi hili la polisi lilidhamiria kupiga na kuua wanafunzi wa chuo kikuu cha dodoma(UDOM) na vyuo vingine nchini waliokuwa wakidai haki zao, limeua watanzania kwa risasi za moto pasipo sababu za msingi wilayani tarime akiwemo mwanafunzi wa shule ya msingi, jeshi hili pia limetia doa na kutudhalilisha kimataifa kwa kitendo cha kupora maiti mochwari ya wilaya tarime na kuitelekeza barabarani, pia likathubutu na kufanikiwa kuwatesa na kuwaua waandishi wa habari na wanasiasa kadhaa kama Marehemu Daudi Mwangosi aliyeuawa na jeshi hili iringa, Viongozi wa Chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) na watanzania kadhaa waliouawa kwa bomu la kutupwa kwa mkono huko Arusha katika mkutano wa chama hicho, viongozi na watanzania wapenzi wa chama cha wananchi CUF wamepigwa na kudharirishwa hadharani na jeshi hilihili la polisi lililokosa weredi na kukacha majukumu yake na kugeuka jeshi la CCM linalo waua watanzania.
Kutekwa, kuuawa na kuteswa kwa wanachi mchezo unaofwanywa na usalama wa taifa kwa lengo la kuwanyamazisha watetezi wa watanzania dhidi ya wezi au vibaka wa nchi hii (CCM), watanzania kadhaa wa pande zote mbili za muungano ikiwemo tanganyika na zanzibar wameuawa, wameteswa wamelemazwa, Dr. Mvungi alivamiwa kwake na wanosemekana kuwa ni majambazi lakini walio kamatwa kwa tuhuma za kuhusika na mauaji hayo hawakuwa wahusika kwani walibambikiziwa tu kesi kama ilivo ada ya jeshi la polisi kubambikiza watu kesi mbalimbali kwa lengo la kusaidia viongozi wa CCM, kwa maana hiyo ni moja kwa moja usalama wa taifa unahusika na mauji na Dr. mvungi walichokuwa wanakihitaji ni Laptop yake iliyokuwa na taarifa maalum na nyeti zilizosheheni ubadhilifu wa serikali hii ya CCM, kuanisiwa viongozi wa wahitimu wa JKT walio hitaji ajira baada ya kuhitimu mafunzo yao na serikali hii ya CCM kuwapotezea.
Mkoani Simiyu kuna mfugaji aliyefanyiwa ukatili wa kutisha sana baada ya ng'ombe wake zaidi ya 200 kufukiwa shimoni wakiwa hai na askari wa wanyama pori kwa kushindwa kulipa kiasi cha laki moja na nusu kama faini kwa kosa la kuingiza mifungo hifadhini, waziri wa mifugo wakati huo Dr. David Mathayo alilazimika kwenda kushudia na alitoa ahadi kuwa askari hao wangechukuliwa hatua lakini mpaka leo hakuna chochote kilichofanyika huku mzee yule akiishi kwenye lindi la umaskini ulio kithiri kwa kukoswa mwelekeo.
Jeshi la wananchi nalo liingia vitani kuipigania CCM dhidi ya watanzania waishio Mkoani mtwara waliokuwa wakipinga gesi isiende Dar-es salaam kunufaisha wacheche wa CCM na wawekezaji badala yake wawekezaji wakawekeze mtwara ili wananchi wote wanufaike kwa kuanza na wana mtwara kupata ajira.
Jeshi hili la wanachi liligeuka kuwa green guard na kutesa wanamtwara wa kiume na kike kwa kuwaingiza chupa wanawake kwenye maumbile yao ya kike na kuwaingiza spoku za baiskeli wanaume kwenye maumbile yao ya kiume, Jeshi hili likatumia mbinu zake zote zilizo nazo za utesaji na hatimaye kuamua kuazima mbinu ya usalama wa taifa ya kuong'oa kucha na meno kwa bisi bisi bila ganzi, vijana wengi wa kiume walipitia mateso haya makali yasiovumilika huku wakiporwa gesi kwa kivuli cha uwekezaji.
Maisha bora kwa kila mtanzania na vijana kuwezeshwa kupata ajira ni nyimbo zilizovuma sana zilizopatikana katika albamu ya Ari mpya, Nguvu mpya na Kasi mpya. Albamu hiyo iliuza sana sokoni kwani watanzania wengi waliamini ni albamu nzuri kuwahi kutolewa na studio ya CCM, sasa ni miaka 10 nyimbo hizo hajizasaidia chochote kwani zimefanya nchi kuyumba sana na kuwa na madeni makubwa makubwa ya matrilioni.
Juzi studio hii ya CCM imekuja na albamu nyingine ya UMOJA NI USHINDI, imemtambulisha mwana sanaa wake mpya aliefuzu mafunzo mafunzo ya kuipa serikali hasara ya mabilioni baada ya kushindwa vibaya mahakamani na wachina kusu kesi ya samaki, mwanasanaa huyu anafanya sanaa ya maigizo, ameshajaribu maigizo kadhaa kama kuamuru watu wa kigamboni kutembea juu ya maji kama hawana pesa ya kivuko.
Mara baada ya kutangazwa kuwa mgombea wa chama chake mwana maigizo huyu aliapa kuwalinda na kuwatetea wana CCM na viongozi wa CCM huku akijinadi kwa kusema "Nashukuru kwa dhamana na heshima mliyonipa nawaahidi wajumbe wote na viongozi wangu wote wa CCM na wana CCM wote kuwa sitowaangusha kwa chochote kile"
sasa kwa nini watanzania tutegemee kipya chini ya utawala huu wa CCM ilihali mgombea wao kaanza kuwatukuza na kuwaona wao ndio miungu watu kuliko sisi wapiga kura kwani tayari amesha jipanga kutetea chama chake na viongozi wake dhidi ya ufisadi waliofanya kwa watanzania?
Kinachonisikitisha ni kuwa badhi ya watanzania wamesahau mateso, manyanyaso, matusi na kejeli walizopitia miaka kumi ya utawala huu wa CCM, eti leo wanaona CCM imeleta mtu mzuri kiukweli HAPANA na haitatokea CCM ikaweka mgombea mwenye kupenda watanzania na mwenye kupenda mabadiliko hiyo ni kwa sababu imefanya maovu mengi hivo kamwe haiwezi weka mtu ambae akishinda atawaadhibu kwa maovu yao, kila mtanzania anajua maovu na manyanyaso yaliofanywa na chama hiki cha mapiinduzi kilichopindua rasilimali zetu kutoka kwa wengi na kwenda kwa matumbo yao binafsi
Hakutatokea jipya chini ya utawala mwingine wa CCM endapo ikishinda, watanzania watarajie mateso mengine miaka 5 kama siyo basi 10 mpaka tuje tushtuke wezi hawa watakuwa wameiba kila kilichopo na tumebaki watupu, CCM imetudharau kwa muda mrefu sana na inajua fika watanzania wahawezi kufanya lolote kwa maana ni wapole, kwa hakika upumbavu ndio unao tuponza siyo kwamba sisi ni wapole mbona huko tarime hawataki ushenzi huu wa hawa wezi mfano. Walimfukuza mgombea wa CCM aliekuwa akiwania nafasi ya urais alipoenda huko kutafuta udhamini, wanachi wa tarime walimwambia wanataka pesa alizoiba kipindi cha richmond
Tuamke watanzania tuache kuburuzwa na hawa CCM, hii ndo nafasi pekee ya sisi kufanya maamuzi, tuwaonyeshe watu wote duniani na watawala kuwa watanzania siyo watu wa kuchezea hasa kwenye rasilimali zao na taifa lao, tusimame tuwaoneshe vyama vyote kuwa tunaweza kuwaondoa madarakani endapo hawafati malsai ya taifa, tunapaswa kuiondoa CCM, huko hakuna mzuri na ieleweke tatizo siyo mtu bali tatizo ni mfumo uliopo CCM ndo mbaya, hivo ni wakati wetu watanzania kufanya maamuzi sahii octoba kwa kuiondoa CCM, tunapaswa kupiga kura kwa wingi za kuikataaCCM kuanzia udiwani mpaka urais tuhakikishe CCM haibaki tena madarakani.
myenyekiti wao alisema sasa CCM imepata mtu atayekiunganisha chama na mipasuko, sasa watanzania tunaenda kweli kumchagua mtu aende ikulu kunusuru chama na mipasuko au tunachagua mtu atakaye tuongoza na kusimamia rasilimali zetu kwa usawa? Naamini tuna paswa kuwaweka pembeni wajinusuru na mipasuko yao huku sisi tukiweka ikulu chama/umoja wa vyama unaoweza kutuongoza na kuweka usawa katika rasilimali zetu.
TUUNGANE KWA PAMOJA OCTOBA NA MAKUNDI MBALI MBALI KAMA ;-
- KINAMAMA WALIO KAZA MATUMBO YAO KWA VITENGE NA KANGA HUKU
WAKIUGULIA MAUMIVU KWA KUZIKA WATOTO WAO WALIOUAWA NA SERIKALI
YA CCM KUPITIA POLISI HUKO VYUONI WALIPOKUWA WAKISOMA PIA FAMILIA
ZOTE ZILIZOPOTEZA WAPENDWA WAO KWA UONEVU HUU WA CCM,
- WATUMISHI MLIOITWA MBAYUWAYU NDIO WAKATI WENU KUWAONESHA NINYI
NI WATUMISHI WENYE MAAMUZI, NA SI MBAYU WAYU KWANI MBAYU WAYU HANA MAAMUZI.
- WANAFUNZI MLIOPIGWA KUTESWA, KUPEWA VILEMA VYA ULAZIMA HUU NDIO
MUDA WA KUMWONDOA MKOLONI MWEUSI ALIEWAPA ULEMAVU NA MAKOVU YASIOSAHAULIKA, JITOKEZENI KWA WINGI KUJIANDIKISHA KISHA MPIGE KURA NA KUZILINDA MPAKA TUHAKIKISHE WEZI HAWA WANATOKA MADARAKANI.
- WAFANYA BIASHARA NA WAKULIMA, PIA WAVUVI NA MADEREVA HUU NDIO
MUDA WA KUMWONDOA MKOLONI ALIETUWEKEA MGOMBEA MWIZI NA MBADHILIFU KWA KIVULI CHA UCHAPA KAZI, MGOMBEA HUYU INAELEWEKA ALIWAFANYIA NINI WAVUVI NA MADEREVA ALIPOKUWA KATIKA WIZARA ZA SEKTA YAO, NI HUYUHUYU AMEUZA NYUMBA ZA SERIKALI.
NI HUYUHUYU ANATUIBIA KWA KIVULI CHA UJENZI WA BARABARA NZURI YA KIWANGO. UPANA WA BARABARA UNATAKIWA KUWA MITA 6.7 AU 6.8 HUYU MGOMBEA WAO ALISIMAMIA UJENZI WA MITA 5.3 KWINGINE NI 5.4 VIPI HIZO 1.5 AU 5.4 PESA ZAKE ZINAENDA WAPI ZINAENDA WAPI? KWA MAANA NI TAKRIBANI TRILIONI KADHAA HASA BARABARA IKIWA YA UREFU WA KM 500 AU ZAIDI.
- WACHIMBAJI WADOGOWADOGO, MACHINGA, MAMA NTILIE NAAMINI MNA MAJIBU YA
NI NINI MLICHOKIPITIA MIAKA YOTE HIYO YA UTWALA WA CCM,
IKUMBUKWE KUWA WATANZANIA WENGI WAMEKUFA, WAMETESWA WAMELEMAZWA NA CCM KUPITIA KAULI YENYE BARAKA ZA CCM "WAPIGWE TU" ILIYOTOLEWA NDANI YA BUNGE TUKUFU NA MIZENGO PETER KAYANZA PINDA(WAZIRI MKUU).
TANZANIA NI YETU SOTE NA SI WACHACHE, HATA SIKU MOJA TUSITEGEMEE CCM ITATUOA HAPA TULIPO KWENDA MBELE ILHALI MIAKA 53 IMESHINDWA, ZAIDI INATURUDISHA TULIPOTOKA, WATANZANIA TUSIMAME TUAMUE MAENDELEO YA NCHI YETU WENYEWE KWA PAMOJA KWA KUINYIMA CCM KURA , MUDA WA MIAKA 53 UMEWASHINDA HATA TUWAPE MIAKA MINGINE 10 HAWAWEZI, ZAIDI HALI YETU ITAKUWA MBAYA KULIKO SASA, DENI LA TAIFA LITAKUWA KUBWA KULIKO SASA, IDADI YA WASIONACHO NA WALIONACHO ITAKUWA KUBWA KULIKO SASA.
NI DHAHIRI TUNA PASWA KUMWONDOA MKOLONI MWEUSI (CCM) SASA KWA MUSTAKBALI WA RASILIMALI ZETU HASA UCHUMI WETU KAMA TAIFA KWA PAMOJA.
SASA NI WAKATI WA KUIONDOA CCM.
SEMA:-
Msema Yote (Mtanzania anayeishi TANGANYIKA).

TUFIKIRI PAMOJA, TUSEME PAMOJA NA TUTENDE PAMOJA
NIMECHOKA KUUAWA, NIMECHOKA KUIBIWA, NIMECHOKA KUTESWA NA KUNYANYASWA NDANI YA
NCHI YANGU, NIMECHOKA KUITWA MPINZANI NIMECHOKA KUDHARAULIWA.
SITAKI TENA UTUMWA NDANI YA NCHI YANGU, SASA NI MIMI NA TANZANIA HAPANA CCM OCTOBA 2015.