Daudi Mchambuzi
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 62,188
- 128,284
Body guard wa mgombea wa ccm kata ya Themi ajulikanaye kwa jina la Antony Mrema a.k.a Blair Kichwa kubwa amepoteza uvumilivu wa kisiasa na kumvamia kada wa Chadema ajulikanaye kwa jina la Emanuel Paul a.k.a Rasta ambaye ni kaka yake wa damu.
Kizazaa hichi kimetokea hapa Themi maeneo ya Fire madukani ambapo mgombea wa udiwani wa kata ya Themi CCM mheshimiwa Victor akiwa anakatiza maeneo hayo akiwa na Body guard wake kwa jina 'Blair Kichwa Kubwa' walikuta kundi kubwa la vijana wa CHADEMA Themi wakipanga mikakati ya kuomba kura nyumba kwa nyumba, gafla Body guard huyo wa CCM alianza kutoa maneno ya matusi dhidi ya vijana wa CHADEMA na Mheshimiwa Victor ambaye ni mgombea wa udiwani kata ya themi kwa tiketi ya CCM aliondoka upesi na kuingia ktk ofisi ya ccm zilizokua karibu na kumuacha Body Guard wake akiendelea kuchana picha za chadema na ndipo kada maarufu wa CDM almaarufu kama Rasta aliingilia kati zoezi hilo na kumkataza green guard huyo 'Kichwa Kubwa' kuacha kuchana posters kwasababu majibu yatapatikana tarehe 16 baada ya kupiga kura. Rasta alizidi kumjazibisha kada uyo wa ccm kwa kumwambia maneno haya yafuatayo:
Nanukuu "Najua jana mkutano wenu wa Mwigulu Nchemba umebuma usituletee hasira kwenye matangazo ya CHADEMA na dozi yenu itajulikana kwenye box la kura"
Green Guard huyo alishindwa kuvumilia na kuamua kumkamata kada wa CDM 'rastaman' na kumtandika makofi na kumvuta rasta zake kumalizia jazba zilizomzidi.
Watu wazima tuliamua kuingilia kati na kumsihi rasta aondoke eneo la tukio kwasababu ni dhahiri makada wote wa CCM hapa Themi wamepanic na wameamua kupiga watu hovyo.
My take:
CCM kata ya Themi, Tawi la Fire mnazidi kupoteza hata hizo kura 2 mlizokua mzipate.
Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums

Last edited by a moderator: