CCM wamekabwa kila kona, hawana mpya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM wamekabwa kila kona, hawana mpya

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Kidatu, Oct 11, 2010.

 1. K

  Kidatu JF-Expert Member

  #1
  Oct 11, 2010
  Joined: Jun 11, 2008
  Messages: 1,491
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Slaa: Watanzania ipuzeeni CCM
  • Asema imeonyesha dalili za kufa

  na Mwandishi wetu


  [​IMG] MGOMBEA urais kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa, amewataka Watanzania kupuuza ujumbe mfupi wa maneno (sms) unaosambazwa kupitia simu mikononi kuwa ni ujanja wa Chama cha Mapinduzi (CCM), baada ya kuona kimekabwa koo kila kona.
  Akihutubia mamia ya wananchi katika mkutano wake wa kampeni uliofanyika katika kijiji cha Kalinzi, Dk. Slaa alisema CCM imekabwa koo kila idara hivyo imelazimika kutuma ujumbe kuwahadaa Watanzania ili waamini uongo unaosambazwa.
  “Nimesikia wanasambaza ujumbe kwenye simu za mikononi wanasema mimi ni mropokaji… nawaambia Watanzania wenzagu, wapuuzeni CCM hii ni dalili tosha kwamba tumewakamata kila kona wanahaha kujinasua…hizi ni porojo za CCM; zinaonyesha wazi sasa wameanza kutapata kama mtu anayetaka kufa, imeonyesha sasa ni kama inapumulia mashine,” alisema Dk. Slaa.
  Alisema kutokana na hali hiyo, CCM imekuwa bingwa wa kumzushia mambo mbalimbali ambayo hayana ukweli wowote mbele ya jamii.
  Akizungumzia suala la yeye kuambiwa anataka kwenda Ikulu kwa njia ya kumwaga damu, Dk. Slaa alisema amekuwa mbunge wa jimbo la Karatu kwa kipindi cha miaka 15 bila kumwaga damu ni kitu ambacho hakiwezekani hata siku moja.
  “Nimekuwa mbunge wa Karatu kwa kipindi cha miaka 15, sikumwaga damu… sasa hiyo damu itatoka wapi? Kwa vile tumefanikiwa kuwabana wanahangaika kujinasua,” alisema Dk. Slaa.
  Alisema pamoja na yeye kuitwa mropokaji, anakubali kwa vile uropokaji huo umezaa matunda kipindi chote alichokuwa bungeni.
  “Wananiita mropokaji, mimi nasema sawa nimeropoka na matunda yangu yameonekana, niliwataja watu kama Basil Mramba, Gray Mgonja na Daniel Yona mbona wamefikishwa mahakamani? “Kama nisingefanya hivi wangeendelea kutafuna fedha za walipa kodi wa nchi hii….nawaambieni jamani hata wakati ule nilimtaja Rais Jakaya Kikwete mbona hawajanikamata kama ulikuwa uongo?” alihoji Dk. Slaa na kushangiliwa na maelfu ya wananchi.
  Akimnadi mgombea ubunge wa jimbo la Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe, Dk. Slaa alimmwagia sifa kutokana na shughuli za maendeleo alizozifanya jimboni kwake.
  Akihutubia mikutano ya kampeni eneo la Kagunga, Dk. Slaa alimmwagia sifa mbunge huyo anayetetea nafasi yake katika uchaguzi mkuu ujao kuwa ni jembe linalorahisisha kazi ya mkulima, kutokana na alivyoshirikiana na wananchi kutatua kero na matatizo yanayolikabili jimbo lake na mkoa wa Kigoma kwa ujumla.
  “Zitto amejipambanua kama mbunge anayejua majukumu na wajibu wake kwa wapiga kura, amekuwa akiisukuma kweli kweli serikali kutekeleza miradi ya maendeleo kwenye jimbo lake na pale alipoona serikali inasuasua alitumia uwezo wake binafsi kama alivyofanya katika mradi wa umeme Kagunga kwa kuzungumza na serikali ya Burundi ili mpate umeme kutoka huko …nimepata taarifa kuwa mazungumzo yamefikia pazuri,” alisema Dk. Slaa.
  “Huyu ni mbunge na mgombea unayemnadi kifua mbele siyo kama wengine ambao ukifika majimboni mwao unaogopa na kujifikiria utaanzia wapi kuwanadi,” alisema Dk. Slaa.
  Aliwahakikishia wakazi wa kijiji hicho kuwa wataondokana na adha ya kutegemea mawasiliano ya simu za mkononi kutoka mitandao ya nchi jirani ya Burundi.
  Miradi mingine iliyofanikishwa kijijini hapo kwa msukumo wa Zitto ni ujenzi wa bandari ya kisasa inayoziunganisha nchi za Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) na Tanzania. Dk. Slaa alirejea ahadi yake ya elimu bure hadi kidato cha Sita ili kuwapa uwezo watoto wa Tanzania kuhimili ushindani katika soko la ajira la Afrika Mashariki na kutoa mfano wa watoto wa nchi jirani ya Burundi wanavyoweza kuongea kwa ufasaha lugha ya Kifaransa tofauti na wa hapa nchini ambao baadhi yao wanaohitimu elimu ya msingi bila kuwa na uwezo wa kuongea Kiswahili ambayo ni lugha ya taifa.  My take: Ni kweli kabisa CCM hawana sera tena, wameshikwa pabaya, wanatapatapa. Pressure inapanda, pressure inashuka. CCM iko ICU

  [​IMG]


  juu[​IMG] [​IMG]
   
 2. hashycool

  hashycool JF-Expert Member

  #2
  Oct 11, 2010
  Joined: Oct 2, 2010
  Messages: 5,899
  Likes Received: 442
  Trophy Points: 180
  "You cannot fight against the future. Time is on our side." CHADEMA
   
 3. K

  King kingo JF-Expert Member

  #3
  Oct 11, 2010
  Joined: Sep 6, 2010
  Messages: 401
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  CCM wanapumulia mashine na mashine yenyewe itazimika sasa hivi kwa maana hiyo itakufa soon
   
Loading...