Kuna kila dalili ccm wamechanganyikiwa, mara wanasema Tume ya uchaguzi inaipendelea ukawa, wanakuja kupiga Kampeni pale ambapo wametoka wenyewe. Lakini kubwa zaidi ni hii ya kukosa ubunifu na kuanza kutumia slogan ya mabadiliko, wanasema magufuli ni mabadiliko na mabadiliko ni magufuli!! Ama!! Hii slogan si ilianzishwa na mbowe wakati mgombea wa uraisi wa chadema Edward Lowassa alipokuwa anaongea na kina mama. Tena akawafundisha na namna ya kujibu kwa vitendo?! Kwa hali hii inaonyesha wazi kuwa ccm wamekosa sera na ubunifu. Na mwaka huu wataenda kushindwa vibaya kwenye uchaguzi.
Wapi Nipe Ninawe