Walianza akina Nape tangu kwenye mabaraza kutetea Serikali mbili, akina Mwigulu na makada wengine ndani ya CCM wamediriki kusema wazi kuwa wanaotetea Serikali tatu wajiandae kuihama nchi na kuwa wananchi watakaotetea Serikali tatu wajiandae kulipa kodi ya kichwa; hata Mkuu wa Nchi Mhe. Kikwete alitamka wazi kuwa Serikali tatu itakuja labda baada ya yeye kuondoka madarakani;
Iweje leo baada makada wa CCM kujikanyaga wenyewe kwa kauli zao watu wanataka kuhamisha mjadala mzima na lawama kwa WAKRISTU na kwa MUADHAMA KARDINALI PENGO. Ina maana wao CCM na watawala kwa ujumla hawana wanachosimamia ila ni kusubiri kuangalia watu fulani wanataka nini ili waweze kudandia?. Kama ni suala la Ukristu; KIKWETE, SHEIN, BILALI, SHIVJI na wawakilishi wote wa CCM kutoka Zanzibar ni Wakristu?
Tufike mahali tutumie akili zetu tulizopewa na maulana kwa busara hata kama ni finyu na sio kila mara tuwe tunatafuta sababu na visingizio kwa minajili ya kuficha udhaifu na ujinga uliotujaa vichwani mwetu.