Habari zilizonifikia hivi punde ni kwamba CCM wako mahakamani muda huu wakitafuta hati ya kimahakama kuzuia uchaguzi wa kumpata Meya wa Jiji la Dar es salaam usifanyike kama ilivyokuwa imetangazwa hapo awali, na kama barua za mialiko kwa wajumbe wa kikao hivyo zinavyoelekeza.
Aidha sababu kubwa inayotajwa CCM kukimbilia mahamakani kutafuta zuio la uchaguzi wa Meya wa Jiji inatajwa kuwa ni wao (CCM) kuendelea kutafuta mbinu ya kushinda uchaguzi huo bila kujali idadi ya wajumbe wao ni ndogo kuliko ya Ukawa.
Awali moja ya mbinu tegemeo waliyojua itawapa ushindi ni kuongeza wabunge wa viti maalum kutoka nchi jirani ya Zanzibar na wengine kutoka mikoa ya Tanzania bara, ambao kwa bahati mbaya baada ya kufuatilia hao wanaotoka mikoa mingine ilibainika michakato yao ya kusaka ubunge wa viti maalum ulianzia huko mikoani kinyume na ukweli kwamba makazi yao yako Dar es salaam. Na kwa maana hiyo wakaonekana si wajumbe halali kujumuishwa kwenye uchaguzi huu.
Kwa wale wabunge wa viti maalum kutoka nchi jirani ya Zanzibar wao ilibainika kwamba hawatakiwi kujihusisha na uchaguzi huu wa kumpata Meya, kwa kuwa wajumbe wote wataingia kama madiwani na hivyo wao hawaruhusiwi kwa kuwa suala la madiwani liko chini ya TAMISEMI, Na suala hilo si la Muungano.
Kwa kuwa mbinu hiyo chafu iliyotaka kutumiwa na CCM imekwama ,Imekwama, na kwa kuwa uchaguzi ni kesho tu kama ilivyotangazwa, basi wameona njia pekee ni kukimbilia mahakamani tena, kuzuia uchaguzi huo wa kesho usifanyike.
Kwa maoni yangu. Nawaomba CCM wakubali tu kwamba jiji liko chini ya Ukawa, ni watanzania hawa, tofauti ni itikadi tu, na kwa kuwa Tanzania iliridhia kuingia kwenye mfumo wa vyama vingi sioni sababu ya msingi kuendelea kulazimisha wakati mchakato huu ulianzia kwa wananchi kwenye uchaguzi mkuu uliopita kwa kuwachagua madiwani wengi wa ukawa.
Ni bora waachane na figisufigisu hizi za kulazimisha kuongoza jiji. ...sidhani kama mbinu hii ya kuendelea kuzuia uchaguzi kwa njia ya mahakama utawasaidia. ..labda kama wanahitaji kwenda hatua nyingine mbaya zaidi ya kumwaga damu ya watanzania kwa kutaka kuongoza jiji, labda kama wanajipanga kupata umeya kwa umafia, kwa vurugu na support ya vyombo vya dola. ...Lakini uchaguzi wa haki na huru, kwa uchaguzi wa kidemokrasia sioni CCM watashinda vipi uchaguzi na meya wa Jiji kwa kuwa uchaguzi ni namba na namba haziongopi. ..Ukawa wana wajumbe takribani 11 zaidi ya wajumbe wa ccm.
Kwa tetesi hii ya ccm kukimbilia mahakamani, nawashauri waachane na mpango huo waache demokrasia itamalaki.