MAHANJU
JF-Expert Member
- Aug 26, 2014
- 5,252
- 8,003
Endapo CCM wakawapigia kura wagombea wa ACT yaani Ktila Mkumbo na Albert Msando, pia Wakampigia mgombea kupitia CUF/LIPUMBA kuwapata wabunge EALA wapinzani kwa ujumla wanatakiwa kuwachukulia hawa kama maadui wakubwa wa mabadiliko nchini.
Sio tatizo wagombea wa ACT/CUF-Lipumba kuchaguliwa kuwakilisha EALA kupitia upinzani,wote ni wanasiasa wazuri wasiokua na shaka kwenye siasa zao lakini itakua ni jambo ambalo sio la kawaida Chama kikuu cha upinzani Kama CHADEMA kukosa uwakilishi kabisa ikizingatia kua kua uwakilishi wao bungeni ni wabunge zaidi ya 18%,kama ni hivyo basi kila chama cha cha upinzani kingetoa angalau mbunge mmoja.
Busara iliyokua imetumiwa na spika wa bunge kwa kuangalia uwiano wa uwakilishi kwenye bunge la muungano ni kubwa mno na ilikua ni ya kiuungwana. Zitto Kabwe alilipinga jambo hili makusudi kabisa huku akijua fika kua CCM hawako tayari kumpigia kura mbunge wa CHADEMA ikiwa tu kwenye uchaguzi wa TLS ambao haukua wa kisiasa walionesha misimamo yao wazi,anaona ni bora hata ACT yake isiyokua na mwakilishi kwa bunge la muungano au kumpigia kura Mnyaa mfuasi wa LIPUMBA ambaye ni kirusi cha mgogoro ndani ya Chama hicho na kuendelea kuinufaisha CCM.
Zitto Kabwe atambue kwamba hata CHADEMA wakikosa uwakilishi EALA hawatapoteza kitu chichote zaidi ya kuwafanya wajipamge zaidi, Zitto Kabwe atambue kuungwa mkono kwao na CCM sio bure, anaweza kufurahia hivi sasa lakini kwa baadae itamgharimu sana kwenye ustawi wake wa kisiasa, Zitto Kabwe atambue kua alishaanza kuonesha nia ya kushirikiana na wenzake ili kumng'oa mkoloni mweusi ambao kitendo hiki kinaweza kumfanya ashtukiwe na wenzake.
ACT bado ni Chama kichanga sana ambacho kimsingi hakiwezi kusimama peke yake kwenye uchaguzi wowote kikafanikiwa, bado ni chama kichamga sana kwenye rasirimali za aina zote kufikia kutwa chama kikuu cha upinzani.Wala wabunge wawili wa uwakilishi EALA kupitia ACT hawawezi kua na impact yeyote kukibeba chama.
Kwa sasa CHADEMA kimekua taasisi kubwa na imara ambayo inazo rasirimali za kutosha za kila aina kupambana na CCM kwa nguvu zote,Mh Zitto Kabwe asitumie uhasimu ulipo kati ya CCM na CHADEMA/CUF-halisi kujinufaisha kiubinafsi badala yake aangalie manufaa ya kisiasa ya baadae kwa chama chake.
Ushirikiano utakaooneshwa na wabunge wa CCM juu ya ACT/CUF-lipumba ndioyo reflection halisi ya uchaguzi mkuu 2020 na hivyo ndivyo Mwenyekiti wa CCM taifa anavyopenda iwe.Wawakilishi wa ACT/CUF-lipumba wanaweza kupita kwa kishindo sio kwa sababu kwa kukubalika kwao bali ni kwa sababu maalum.
Ndio kila chama kina haki ya kua na wagombea EALA Lakini chama kikubwa Cha upinzani kama CHADEMA kukosa uwakilishi itakua ni kituko cha mwaka na itakua ni ushabiki usiokua na tija kwa taifa.
CCM ni chama dola na chenye baraza la mawaziri wanaoiwakilisha serikali na pia wana waziri anayeiwakilisha serikali EAC, lakini UKAWA ndio wenye baraza la mawaziri kivuli ambao pia wanaisimamia na kuishsuri serikali ambapo kama wanalo jambo la kusema juu ya EAC kama upinzani wanatakiwa kuwapa wabunge wao kuliwasilisha na kulisema.