Wamefanya vizuri kumpa nafasi ajieleze kama analojema la kuwaeleza, labda angeweza kutamka la muhimu kama vile RPC ameshasimamishwa kazi na atachukuliwa hatua isheria nk. baada ya hapo hunda wangempa nafasi jukwaani. Lakini alipoonyesha kuwa ni yale yale ya kulaghai wananchi wakampa mkono wa kwaheri. Wametumia busara pale.
Pia hawakukosea hata chembe kumkaribisha Dr. Rewitama kuongea, kama ulivyosema ni rafiki yao, hata wewe kwenye msiba wa mtu wako wa karibu atakaeongea pale msibani ni rafiki yako wa karibu au jirani yako aliye na ushirikiano na mwenye busara.
Nimelipenda bango moja walilobeba waandishi, liliandikwa "Kalamu inaweza kuwa hatari kuliko bunduki"; Sijui kama ulilisoma wewe? Ni ujumbe mzito, mwenye akili atatafakari!