CCM Waipinga kauli ya makinda - Arumeru | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM Waipinga kauli ya makinda - Arumeru

Discussion in 'Chaguzi Ndogo' started by usininukuu, Mar 19, 2012.

 1. usininukuu

  usininukuu JF-Expert Member

  #1
  Mar 19, 2012
  Joined: Aug 8, 2011
  Messages: 380
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  WANANCHI wa Jimbo la Arumeru Mashariki, wameombwa kumchagua mgombea Ubunge wa Jimbo hilo kupitia CCM, Sioi Sumari ili kumfuta machozi yaliyotokana na kifo cha baba yake mzazi, Jeremiah Sumari ambaye alikuwa Mbunge wa Jimbo hilo.

  Mbali na hilo wananchi hao wameelezwa kuwa kwa kufanya hivyo, watakuwa wamejipatia baraka kwa Mungu kwani watamwezesha Sioi kupata mshahara utakaomwezesha kuendesha familia aliyoachiwa na baba yake.

  Mwito huo ulitolewa juzi katika Kijiji cha Migadini, Kata ya Mororoni na Mbunge wa Mtera(CCM), Livingstone Lusinde alipokuwa akimnadi mgombea huyo katika kampeni za uchaguzi mdogo zinazoendelea jimboni humo.
  Source; Gazeti la majira

  My take;
  Kauli hii ya Lusinde inapingana na hoja iliyotolewa na makinda kuwa "Ubunge sasa umekuwa ni sehemu ya UMASIKINI WA KUTUPWA" hali iliyowafanya wabunge wengi kufikilia kujiuzulu.
   
 2. Emmani

  Emmani JF-Expert Member

  #2
  Mar 19, 2012
  Joined: Jan 27, 2012
  Messages: 525
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Taifa liko kwenye 'roundabout' Kauli gongana tutazipata nyingi tu kipindi hiki! ooh! ubunge ni umaskini mara mchagueni apate mshahara wa kuilea familia!. Wakati wabunge wa CCM zaidi ya nusu wanataka kujiuzulu, SIOI anatumia hadi rushwa kwenda huko bungeni!!
   
 3. K

  Kuntakint JF-Expert Member

  #3
  Mar 20, 2012
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 1,112
  Likes Received: 470
  Trophy Points: 180
  Ata mimi nilifiwa na dadangu kwani nilionewa huruma na nani wa kunisaidia. Huyo Sioi aonewe huruma wa nini wakati wanaishi Uingereza kwa kodi ya watanzania. Sioi na mkewe wanapesa gani ya kuweza kununua nyumba uingereza kama sio pesa za watanzania ndio zinatumwa kwa ujanja wa kulipia shule na alizochota Lowasa. Sioi ni mkwe wa Lowasa sasa Lowasa leo anagawa mamilioni za watanzania kila kona ndio atashindwa kumtunza mkwewe na mtoto wake. Huyo Lusinde achane na siasa za mwaka 47. aende akapunguze tumbo lilijaa mafuta ya ufisadi
   
Loading...