Ccm wahofia kupoteza viti maalumu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ccm wahofia kupoteza viti maalumu

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by KIDUNDULIMA, Sep 20, 2010.

 1. K

  KIDUNDULIMA JF-Expert Member

  #1
  Sep 20, 2010
  Joined: Aug 18, 2010
  Messages: 775
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 45
  Moja ya vitu vinavyo waumuza kichwa wapanga mikakati ya ushindi wa CCM ni kupoteza viti maalumu. Viti maalumu hutolewa kwa uwiano wa kura anazopata mgombea urais. Hivyo basi kama mgombea wa CCM (Kikwete) ataambulia 40% ya kura zote (hata viti maalumu atapewa hivyo hivyo) na inamaana kuwa asilimia 60% ya viti maalumu vitakwenda kwa wapinzani. Hivyo msishangae CCM wakihaha kutumia mabilioni kwa ajili ya kampeni, kubandika picha kila mtaa, kuongeza ratiba na helikopta kwa mgombea wao wa urais, kusomba watu kwa ajili ya mikutano ta kampeni, kumchafua Dr Slaa, na kutumia propaganda kuwa afya na elimu haviwezi kutolewa bure kwa kuwa pesa za kufanya hivyo hazipo. Kwa maana anguko kuu linawasubiri

  Chadema tuendeleze mpambano. Hakuna kulala mpaka kieleweke
   
 2. m

  mwita ke mwita JF-Expert Member

  #2
  Sep 20, 2010
  Joined: Aug 13, 2010
  Messages: 5,491
  Likes Received: 1,220
  Trophy Points: 280
  mimi silali mpaka kiama
   
 3. M

  Mkulima JF-Expert Member

  #3
  Sep 20, 2010
  Joined: Feb 4, 2007
  Messages: 698
  Likes Received: 113
  Trophy Points: 60
  Hii sio sahihi kabisa. Mchanganuo wa kupata wabunge wa viti maalumu ni kama ifuatavyo:

  Kulingana na Ibara Na. 66 na 78 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya 1977 Vyama vya Siasa vitapendekeza kwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi majina ya wanawake ambao Tume inaweza kuwatangaza kuwa Wabunge kama ikiridhika kwamba wana sifa zinazostahili.

  Tume inatakiwa kutangaza majina ya wanawake kwa idadi isiyopungua asilimia 30 ya Wabunge wote kwa ajili ya viti maalumu kwa wanawake. Mgawanyo huo utazingatia uwiano wa kura ambazo kila chama kimepata katika uchaguzi wa Bunge. Endapo mgombea ubunge amepita bila kupingwa, kura za mgombea Urais wa chama cha mbunge zitachukuliwa kuwa ndizo kura halali za mbunge huyo. Kama hakina mgombea Urais, asilimia 51 ya idadi ya wapiga kura walioandikishwa zitachukuliwa kuwa ndizo kura halali za mbunge wa chama husika. Hata hivyo, chama kinaweza kupata nafasi ya viti maalumu cha mbunge mwanamke endapo kimepata 5% ya kura zote halali za uchaguzi wa wabunge.
   
 4. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #4
  Sep 20, 2010
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,899
  Likes Received: 12,035
  Trophy Points: 280
  Pamoja na sahihisho lako lakini hofu bado iko palepale ya kupoteza viti vingi maalumu tofauti na 2005.
   
 5. BornTown

  BornTown JF-Expert Member

  #5
  Sep 20, 2010
  Joined: May 7, 2008
  Messages: 1,716
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Hii ni PRESHA INAPANDA PRESHA INASHUKA!!!! :becky::becky::becky:
   
 6. B

  ByaseL JF-Expert Member

  #6
  Sep 20, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 2,223
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Tatizo la vijana wengi siku hiyo 31 Oktoba 2010 watakuwa na hangover hawataenda vituoni kupiga kura mwishowe tunaishia kulalamika kwenye Forum!
   
Loading...