CCM wahaha, wahofia Yanayotokea Misri, Libya

Kituku

JF-Expert Member
Nov 18, 2010
238
24
Ndugu wana jamii
Katika pita pita zangu kushangaa ulimwengu, nimekutana na ujumbe mahsusi katika wall ya Dr Hamis Kigwangala (mb) Nzega. (kwenye facebook)

Ukisomeka hivi::
Kuhamasisha na au hata kufikiri tu kwamba Tanzania itafika na kufaidika na maandamano na mapinduzi ya viongozi waliowekwa na umma kwa njia za kidemokrasia, ni ukosefu wa hoja, weledi na upotofu uliokithiri! Michango/mawazo ya namna hiyo tuikatae kwa nguvu zetu zote!


na hizi chini ni miongoni mwa comments zake

Dokta Hamisi Kigwangalla Tanzania ina matatizo yake lakini siamini kama yanatatulika kwa vurugu, kwa utovu wa nidhamu kwa sheria na kanuni zilizowekwa na vyombo vyetu vilivyotuongoza hadi kufikia hapa tulipo...kufikiria kuvunja amani na utulivu tulionao si sahihi na wala hatujafika na hatutofika huko kwa uwezo wa mungu inshaallah! Tuhoji, tubishane na tushindane kwa nguvu ya hoja bila kuhamasisha wala kufikiria hoja za nguvu...hazina nafasi na sote kwa pamoja tuzikemee! Leo hii walioandamana hizo nchi za huko bara arab wameanza kuzikimbia nchi zao...


Dokta Hamisi Kigwangalla Kiva, mazingira ya huko ni tofauti na ya kwetu...Tanzania hakuna mtu anayeng'ang'ania kukaa madarakani kwa mabavu...viongozi na wawakilishi wetu tunawachagua kwa sheria na taratibu tulizojiwekea! na wananchi tuna haki ya kujadili na kudai mabadiliko kwenye chochote tunachokiona hakiendi sawa - kwa ufupi 'hakuna udikteta'. sasa iweje leo tusipambane kwa nguvu ya hoja ili kurekebisha mapungufu yaliyopo na badala yake tuanze kujadili siasa za mkumbo wa vurugu na uvunjaji wa amani??? Hili ndo ninalolikataa hapa mimi!


Mimi binafsi, nimeamini kweli viongozi wetu tayari wamekuwa na hisia na imani ya woga juu ya mapinduzi yalioonyesha na yanayoendelea huko nchi za wenzetu. Inaonyesha dhahir kuwa sasa wapo viongozi tayari wameanza kupata vitumbo joto wakirefer yanayotokea Egypt, Libya, na kwengineko. SAsa kwa maelezo haya na comments hizi za Mbunge, wana jamii hamuoni hawa watu kweli wamelewa madaraka na wamekaa kwenye vyeo walivyonavyo kulinda maslahi ya o na mfumo walio nao?

Kweli, baadhi wa wabunge wamegombea nafasi zao ili tu wakajinufaishe na kutajirika kwa mamilioni ya maposho na fedha na si kwa maslahi ya umma na mustakabali wa taifa..

Wanajamii mnaonaje juu ya statements za huyu mbunge hapo juu?
 
Back
Top Bottom