Elections 2010 CCM waanza rasmi?

Naona kwa nyuma Ridhiwani anawakilisha!

Anajiandaa kurithi dynasty!

Wow nilikuwa sijamwona

ajmoo8.jpg
 
..unajua kwenye nchi iliyojaa umasikini kama Tanzania, ni kufuru kwa chama tawala kufuja mapesa yote hayo kwa ajili ya kampeni

..CCM wamedai wana uhakika wa ushindi sasa haya matumizi makubwa-makubwa ya kampeni ni kwa faida ya nani?
 
Mie afya ya huyu mgombea ni mashaka matupu

Ndugu yangu huo wsi wasi wa watu tulio wengi! Ipo siku ataanguka kwenye midahalo ya kimataifa kama DAVOS kwenye world economic forum ama kwenye vikao vya UN. Aibu itarudi kwa watanzania
 
..unajua kwenye nchi iliyojaa umasikini kama Tanzania, ni kufuru kwa chama tawala kufuja mapesa yote hayo kwa ajili ya kampeni

..CCM wamedai wana uhakika wa ushindi sasa haya matumizi makubwa-makubwa ya kampeni ni kwa faida ya nani?
Nilikuta wamebandika makaratasi yao kwenye ukuta wa nyumba yangu,nikauliza nani kafanya hii kazi,jibu lilikuwa ni vijana walikuwa na kiongozi wa serikali za mitaa,nikamwendea huyo kiongozi na nikamwambia kwakuwa ninamuheshimu naomba tuongozane akatoe uchafu wake,alitii na kutoa.Ujinga mtupu,mabango mpk kwenye Public toilets!
 
Ndugu yangu huo wsi wasi wa watu tulio wengi! Ipo siku ataanguka kwenye midahalo ya kimataifa kama DAVOS kwenye world economic forum ama kwenye vikao vya UN. Aibu itarudi kwa watanzania

Mimi nadhani ni vema akianguka huko,tutapata coverage nzuri tu ya tukio zima,maana hakutakuwa na Tido wala Marine Hassan wa kukwepesha camera!
 
ni kwasababu hawakuandika KUANGUKA KWA KIONGOZI WA CHADEMA........!?

Kwani MAkani anagombea urais ,pili ana miaka mingapi?
Mkwere kagonjwa ww miaka hamsini kazaa una unadondoka mara mia kwa mwaka
 
Watatumia kila hila lakini siku moja watajuta kuzaliwa. Sauti ya wengi ni sauti ya Mungu, kuna siku dhuluma na ulaghai wao utajipambanua na watalia na kusaga meno. Siku hiyo yaja na haiko mbali sana
 
Mimi nilinunu magazeti ya Tdaima, Mwananchi, NIpashe na Habarileo maeneo ya Morocco kwenye Trafic lights lakini muuzaji hajanipa hivyo vicover page vya CCM
 
Mie afya ya huyu mgombea ni mashaka matupu

Eeee, nadhani kuna kila sababu ya kuangalia jambo hilo, kweli afya ya mgombea haifurahishi, hivi ndio kwanza kampeni zimeanza, tuna miezi 2 iliyoshiba, mgombea anaonekana yuko hoi? Hivi kuna mtabiri alisema uchaguzi unaweza usifanyiek mwaka huu, mh yetu macho
 
Gazeti zima liko covered na hilo tangazo... Ukinunua gazeti linakuwa ndani. Sasa, ndo hapo ninaposema kuwa wauzaji walio wengi ndo wameangusha mpango huu, baadhi wanauza kama ilivyotakiwa lakini wengi wameondoa na kuweka kando! HabariLeo, Mtanzania, Majira, Nipashe, Jambo Leo, etc

Nipashe nao??? Kwa kweli hapo Mengi anatia kichefuchefu. Mwanzoni alikuwa anajitahidi sana kuwa fair katika kuandika habari za vyama vyote. Kama na yeye amekubali kununuliwa na mafisadi basi bila shaka na yeye ni fisadi. Na mpango wake wa kuwaita wengine ni mafisadi papa unaonekana ni useless.
 
Mkuu, binafsi siwalaumu CCM... Hata chembe, wamepata opportunity na wameitumia. Sasa, wenye matatizo (njaa?) nadhani ni wenye magazeti kuruhusu gazeti kuwa covered na tangazo kwa tamaa ya fedha.

That's my concern

Mkulu Invizibo,

Nakuunga mkono kutokuwalaumu CCM. Kwani Chadema, CUF, n.k. wangelikuwa na uwezo wa kumudu kununua (kama ulivyosema) nafasi ya matangazo vile CCM wamefanya; nawo wangelifanya hivyo!

Lakini siungi mkono hoja yako kwamba, wenye magazeti wasiruhu upokeaji wa matangazo kwa vile tu ni ya CCM. Iwapo sheria za kibiashara na sheria za nchi (za uchaguzi) zinaruhusu magazeti hayo kuweka matangazo, basi sioni makosa ya wenye magazeti. Iwapo yamepewa fedha taslimu kutangaza chama fulani, hiyo kwao ni fursa ya kibiashara. Matangazo ni matangazo, ilhali hayakiuki maadili na sheria zilizopo.

Wakulaumiwa hapa ni sisi wanajamii tutakao nunua magazeti eti tu kwa vile kuna mabango ya CCM.

Lakini kama ulivyoelezea kwenye bandiko lako, nimefurahishwa sana kuona kuwa kuna Watanzania wengi wenye msimamo na kuelewa kuwa nchi hii inahitaji mabadiliko...hata kudiriki kunyofoa kurasa hizo kutoka kwenye magazeti. Usemi wa Watanzania si mabwege tena umejidhihirisha!!

Jambo moja ambalo naona ni la muhimu kukumbukwa hapa ni kwamba; walau safari hii CCM (kwa issue za mabango magazetini) wamegharimika kupitia channels zinazojulikana. Maana matangazo hayo yamelipiwa, na hivyo yanastahili kukatwa kodi na magazeti kukatwa kodi ya mapato. Hivyo hela "za wananchi za kampeni" zinarudishwa kwenye hazina yao ya Taifa walau kwa kiwango kidogo. Kuliko kutumika kwa jinsi vile wanavojulikana... i.e. kuhonga watu binafsi na hivyo kukosesha mwanya wa kodi!!
 
Mkuu,

Wauzaji magazeti wengi wamezitoa hizo covers, nadhani hili pia CCM wakiligundua wataona kuwa wametumia hela bure kwani wauzaji wamewaangusha.

Wakuu ilikua ni janja ya kuzuia makombora ya Chadema yaliorushwa Jangwani, lakini haikuwa dawa moto uliwaka na ujumbe ulifika
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom