Allen Kilewella
JF-Expert Member
- Sep 30, 2011
- 20,387
- 38,663
Kila wakati naona kama kuna kusakamwa fulani kwa wachaga walioko kwenye siasa za nchi hii hasa wakiwa Kwenye vyama vya Upinzani. Mwaka 1995 wakati Mrema akiwa katika Ubora wake, CCM ilikuwa inawaambia wananchi kwamba kirefu cha NCCR ni "National Chagga Convention Republic" Maelezo ambayo hata kwa kiswahliil hayatafisiriki! Walikuwa wakisema "Mkimchagua Mrema hii nchi itatawaliwa na wachaga"
Wananchi wakaambiwa kwamba NCCR-Mageuzi ni chama cha wachaga na ndiyo maana kwenye Nembo ya chama hicho kuna mlima wa Kilimanjaro. Hoja ya kijinga kabisa lakini ikashupaliwa na CCM. Kwenye mkoa wowote ule hata kama kiongozi wa NCCR -Mageuzi mchaga ni mmoja tu mkoa mzima ikawa ndiyo nongwa ya kuambiwa hicho chama ni cha wachaga!
Wakati NCCR - Mageuzi inapoitwa ya "Wachaga" CHADEMA ilikuwepo na ilikuwa haishambuliwi hata kama Mwenyekiti wake Muanzilishi ni Mchaga, Mzee Edwin Mtei. CHADEMA baadaye ikaongozwa na Msukuma na Muislam Marehemu Bob Nyange Makani. Wakati CHADEMA ikiongozwa na Makani haikuitwa ya Waislamu wala ya Wasukuma!! Kwa sababu haikuwa ni tishio kwa CCM na wanaofaidika nayo. Wakati huo waliokuwa wanashambuliwa kwa "Upemba" na "Uislamu" wa chama chao walikuwa ni CUF.
Baadaye Freeman Aikaeli Mbowe akachaguliwa kuwa Mwenyekiti wa CHADEMA. Pale alipochaguliwa tu, CHADEMA haikuitwa ya wachaga, ila alipoanza ziara ya kukijenga chama hicho Mwaka 2004 na baadaye kugombea Urais Mwaka 2005, ndipo tulipoanza kuambiwa kwamba CHADEMA ni chama cha wachaga. Hata watu kama kina Mnyika nao wakaitwa wachaga!
Picha inayojengwa na wanaoeneza Propaganda hiyo ya kijinga ambao wengi wao ni watu wa CCM, ni kwamba watu wa Kaskazini hasa wachaga hawafai kuwa viongozi wa nchi hii, kwa kuwa ni watu wa hatari sana na ni wabinafsi. Propaganda hizi zinatofautiana vipi na zile za Wahutu wa Misimamo mikali chini ya kundi lao la "Interahamwe" dhidi ya watutsi na wahutu wenye msimamo wa wastani?
Wakati CCM inasema watu wa Kaskazini ni hatari yenyewe inao viongozi wa ngazi ya taifa toka huko huko Kaskazini. Mchaga anayefaa kuwa kiongozi ni yule tu aliye CCM? Kwani dhambi ya wachaga wasioitaka CCM ni nin? Ni wakati gani watu wa Kaskazini wanapokuwa siyo "Hatari" dhidi ya watu toka maeneo mengine ya nchi hii?
CCM IWAACHE WACHAGA WAISHI KWA AMANI KATIKA NCHI YAO HALALI KAMA MAKABILA MENGINE YANAVYOISHI!!