Baada ya CCM kufikiri wamemaliza nguvu za upinzani waliodhani ndio wakosoaji pekee, limeibuka wimbi la watumishi wa Mungu na viongozi wa dini na makanisa mbalimbali kumkosoa Rais waziwazi kwa utendaji wake.
Baada ya kuona hivyo, vijana wa CCM na serikali yake kwa kutumiwa au kujituma wenyewe wameanzisha vita na kanisa, wanawabeza na kuwajibu viongozi wa dini kama vile wanamjibu Mbowe, wanawaita viongozi wa dini ni vibaraka wa mafisadi, vibaraka wa wazungu, wezi wa mali ya umma n.k n.k.
CCM wameamua kupambana na kanisa kama vile wanapambana na CHADEMA au CUF. Niwaeleze CCM kuwa hii vita mliyoianzisha si lelemama ni kubwa kuliko wanavyodhania inaweza kukisambalatisha chama chenu na serikali yake, hebu chungulieni kwa majirani zetu Congo mpate kujifunza yanayotokea.
Kanisa ni tofauti na chama cha siasa, msitegemee Rais atakuja kupiga marufuku mikutano ya dini kama alivyopiga marufuku mikutano ya vyama vya siasa hadi 2020. Msitegemee Rais atayafuta makanisa kama alivyosema atahakikisha kufikia 2020 hakutakuwa na chama cha upinzani. Anachoweza ni kuwasumbua baadhi ya viongozi wake lakini si kanisa.
Nguvu ya kanisa ni kubwa kuliko nguvu ya chama cha siasa kanisa lina nguvu kuliko hata serikali (anayebisha nitampa mifano). Kanisa lina waumini wa itikadi zote na wananchi wa vyama vyote wa ngazi zote na wa matabaka yote mijini na vijijini. Kanisa kama Roman Catholic na KKKT ni matawi tu yako duniani kote, kwahiyo kulia-attack kanisa la RC Tanzania ni ku attack makanisa yote ya Roman Catholics.
Nimalizie kwa kuwaonya vijana wa CCM na CCM yenyewe wasicheze na imani za watu, viongozi wa dini waheshimiwe na kanisa lazima liheshimiwe.