VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,140
- 18,007
Washauri wote nguli na wa idara mbali mbali za kichama tunahitajika Lumumba Dar es Salaam 'kubuni' mbinu mpya za kupambana na changamoto za vyama vya upinzani, wanaharakati na wananchi kwa ujumla. Kuanzia Jumatatu, Lumumba itagubikwa na vikao vya hapa na pale. Tuna mambo mengi jadilifu. Tuna mzigo mkubwa kwasasa. Tumeambiwa Bungeni mambo yameshatulia na sasa turejee Dar es Salaam 'kukilinda' chama kisera na kiutekelezaji. Tutatoka vipi? Kaeni chonjo! VUTA-NKUVUTE aka Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam(sasa Dodoma)