CCM: Tutazindua kampeni kwa kishindo leo Arumeru

CCM: Tutazindua kampeni kwa kishindo leo Arumeru

Viol

JF-Expert Member
Joined
Dec 15, 2009
Posts
25,419
Reaction score
18,341

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimesema leo Jumatatu, Machi 12, mwaka huu kitalitikisa jimbo la Arumeru Mashariki katika uzinduzi wa kampeni zake za uchaguzi mdogo wa jimbo hilo utakaofanywa na Mwenyekiti Mstaafu wa CCM, Rais Mstaafu Benjamin Mkapa.

Mwenyekiti Mstaafu, Benjamin Mkpa alitarajiwa kuwasili Arumeru Mashariki, juzi jioni tayari kwa uzinduzi wa kampeni hizo.

Mratibu Kitaifa wa kampeni za CCM katika uchaguzi huo, Katibu wa NEC, Uchumi na Fedha Mwigulu Nchemba alisema mkutano wa uzinduzi wa kampeni hizo utafanyika Uwanja wa mpira wa Ngarasero na unatarajiwa kuhudhuriwa na maelefu ya watu kutokana na idadi kubwa ya wanachama na wapenzi wa CCM waliopo jimboni humo.

Mwigulu alisema watakaohudhuria mkutano huo wengi wanatarajiwa kutoka jimboni humo tofauti na CHADEMA ambao alidai katika mkutano wa uzinduzi wa kampeni zao jana (juzi) walisomba kwa magari mamluki kutoka Moshi, Arusha mjini na maeneo mengine nje ya jmbo hilo.

Alisema shamra shamra za mkutano huo utakaofanyika saa tisa alasiri, zitaanza mapema kwa burudani zitakazotolewa na wasanii mbalimbali mahiri wakiongozwa na Kundi la Tanzania One Thetre (TOT Plus).

Akizungumzia kuhusu CHADEMA kulalamikia Tume ya Uchaguzi kuwa haitawatendea haki kwenye uchaguzi huo, Mwigulu alisema, hata safu yao ya uonozi tangu Mwekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe hadi wabunge ikishika nafasi zote kwenye Tume hiyo CCM lazima itashinda uchaguzi wa Arumeru Mashariki utakaofanyika Aprili Mosi mwaka huu.

"Kwa Uchaguzi huu wa Arumeru Mashariki, hata Katibu Mkuu wa CHADEMA Dk. Wilborod Slaa awe Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Mbowe (Mweyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe) awe Mkurugenzi wa Uchaguzi, Zitto (Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA, Kabwe Zitto) awe Msimamizi Mkuu wa Uchaguzi na wabunge wote wa CHADEMA wawe wasimamizi wa uchaguzi huo, halafu CCM tuweke mawakala tu, naapa kikwetu CCM itashinda", alisema Mwigulu.

Alisema malalamiko ya CHADEMA dhidi ya vyombo vitakavyosimamia uchaguzi huo ni woga wa kushindwa kwa sababu wanafahamu kuwa CCM imejiimarisha vya kutosha Arumeru Mashariki na italirejesha jimbo.
 
watazindua kwa kishindo cha kuzomewa si shamrashamra!
 
watazindua kwa kishindo cha kuzomewa si shamrashamra!
Huyu dogo anajiamini sana eeh! Vifedha vyake vya dhambi ndiyo vinampa kiburi nini? Au nini chanzo ca jeuri yake? Kule Tabora aliripotiwa kufanya uzinzi na wake za watu ikaisha hivihivi, leo Meru anaropoka tu, ataangaliwa hivihivi au kuna strategy?
 
Haya magamba yakisha ibia walipa kodi wanaongea kwa nyodo Chama cha ruzuku wanategemea lile li mbunge linalofikiria kutumia masaburi mwenye jina la mnyama akawaimbie watu wa Arumeru kuwavuta labda aimbe ragge ndio watakuja
 
Kama kweli mwigulu amezungumza maneno hayo basi safari yake kisiasa haina muda mrefu itafifia kwa sababu anashindwa kutofautisha mazingira ya wananchi wenye civing na weledi wa kuchambua fikra sahihi za KIMUNGU.Nilivyoshuhudia juzi kwenye ufunguzi wa kampeni za CHADEMA NILIONA KABISA kwamba Mungu amekabidhiwa aamue juu ya Mbunge ajae wa Arumeru mashariki tofauti na majigambo ya Nchemba.NCHEMBA AKUMBUKE KAULI YA NASSARI'MUNGU AMESIKIA KILIO CHA WANA ARUMERU MASHARIKI,TULIANZA NA MUNGU,TUTAMALIZA NA MUNGU.Hivyo namalizia kwa kumtahadhalisha nchemba mbwembwe zake na hulka yake pale Arumeru zitakwisha pale Nassari atakapo tangazwa mshindi kama ilivyo tokea Tarime kwa ushindi wa Waitara na hatimae viongozi wa CCM kukimbia usiku wa manane bila kuagana.
 
hapa mtaani kwetu (MOSHI) kuna wamama viherehere wa ccm wametoweka toka alfajiri nadhani wamewahi lift ya mafuso
 
Yaani CCM imepata kiongozi wa maana sana kuisambaratisha chadema ni kama mkate kwenye chai ya rangi unavyolainika. Hiyo ndiyo siasa maneno murua yanayoleta raha kusikiliza kuliko chadema matusi na kashfa tuuuuuuuu.

Wanakera hawajijui tuu big up MWIGULU
 
Hiyo picha tuu hapo ni dalili tosha kwamba wanakazi ya ziada kushughulikia kushindwa kwao. Chadema jengeni chama chenu kwanza kisha muanze kutukana msitukane wakunga na uzazi mungalinaooo CCM OYEEEEEE
 
Yaani CCM imepata kiongozi wa maana sana kuisambaratisha chadema ni kama mkate kwenye chai ya rangi unavyolainika. Hiyo ndiyo siasa maneno murua yanayoleta raha kusikiliza kuliko chadema matusi na kashfa tuuuuuuuu.

Wanakera hawajijui tuu big up MWIGULU

Duh! Katika post zote, we ndo doa jeusi (una maoni mgando). Jenga hoja, Magamba mna jipya Arumeru?
 
Hiyo picha tuu hapo ni dalili tosha kwamba wanakazi ya ziada kushughulikia kushindwa kwao. Chadema jengeni chama chenu kwanza kisha muanze kutukana msitukane wakunga na uzazi mungalinaooo CCM OYEEEEEE
Wambie bwana.
 
Kishindo kisichokua na TIJA kwa watanzania hatukitaki!mwigulu pesa mmepata wapi?????
 
Back
Top Bottom