Ni jambo la wazi kabisa kwa sasa kuwa kwa vyovyote vile itakavyokuwa Edward Lowassa ana nafasi kubwa sana kuwa mgombea urais wa CCM 2015.
Lowassa ambaye huenda ndiye mtu anayejulikana na watanzania wengi zaidi kama ni mwanaCCM mchafu(Fisadi) zaidi lakini Lowassa ndiye mwanaCCM mwenye nguvu zaidi ndani na nje ya CCM kwa sasa.
Binafsi mpaka sasa sioni namna yoyote kwa chama changu cha mapinduzi kama kinaweza kuepusha Lowassa asiwe mgombea urais wa CCM 2015.
Mikakati mbali mbali ya makusudi ndani ya serikali na CCM imefanyika tena kwa juhudi kubwa ili kumdhibiti Lowassa kisiasa kuanzia kushinikiza kujiuzuru kwake uwaziri mkuu kwa kashfa ya Ufisadi mpaka mkakati wa kujivua gamba na kuteua mara mbili secretariety mpya ya CCM lakini bado havikusaidia kitu.
Karibu kila kada mwandamizi ndani ya CCM imeshachoka kumdhibiti Lowassa na wapambe wake kisiasa na kwa sasa karibu kila kada wa CCM ambaye hampendi Lowassa ameanza kumwogopa sana au kujipendekeza. Mfano rahisi kabisa ni Nape Nnauye ambaye anaogopa kabisa kutaja hata neno Lowassa au Fisadi hadharani kwa sasa na Mwigulu Nchemba ambaye tayari 'ametangaza' kuwa yuko pamoja na Lowassa bega kwa bega katika mbio za urais.
Wakati Lowassa akizidi kuchanja mbuga katika mbio zake za urais kisiasa kupitia makundi mbalimbali ya kijamii na kidini, kambi zingine hasimu za urais ndani ya CCM zimechoka sana na wamebaki kulalamika, kunung'ung'unika na kuhangaika tu.
Kuanzia kambi ya Samweli Sitta, Benard Membe, Fredrick Sumaye nk. kwa sasa wanasubiri miujiza ya kisiasa pekee ndani ya CCM ili waweze kumshinda Lowassa.
Swali, CCM tumeshindwa kumdhibiti Lowassa?