CCM Tabora yakana vijana kumuengua Sitta | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM Tabora yakana vijana kumuengua Sitta

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Vumbi, Mar 26, 2011.

 1. V

  Vumbi Senior Member

  #1
  Mar 26, 2011
  Joined: Nov 7, 2010
  Messages: 191
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Sakata la kumuengua mlezi wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), Samuel Sitta, limeingia katika hatua mpya, baada ya Katibu wa CCM Mkoa wa Tabora, Iddy Ally, kumkana Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Tabora, Robert Kamoga, aliyetangaza uamuzi huo.

  Ally amesema hana taarifa za kuenguliwa kwa Sitta, ambaye ni Mbunge wa Urambo Mashariki na Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

  Akizungumza jana katika ofisi za UVCCM mjini Tabora, Ally alisema yeye kama Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya UVCCM, hana taarifa za kuenguliwa kwa Sitta na taarifa hizo zimemshangaza.

  Alisema taarifa hizo alizisikia kupitia vyombo vya habari, bila kujua kikao gani kilitoa tamko hilo.

  “Jumuia ya vijana inapotaka kufanya vikao, lazima nipewe taarifa na nihudhurie. Mimi kwa sababu ni mjumbe wa kamati tendaji. Jambo hilo silijui. Namsubiri Katibu wa Vijana mkoa, ambaye yupo safarini ili anipe taarifa za lini walikaa na kuamua kumsimamisha mlezi huyo,” alisema Ally.

  Alisema taratibu za maamuzi mbalimbali ndani ya chama zinaenda kwa vikao na mihitasari inakuwapo ili kuondoa utata unaoweza kujitokeza.

  Alisema anasubiri Katibu wa UVCCM Mkoa, Julius Peter, ambaye yuko safarini ili kupata maelekezo kuhusiana na taarifa hizo.

  Jumatano wiki hii, Kamoga alitangaza kuenguliwa kwa Sitta kwa madai kuwa amekidhalilisha chama kwa kusema UV-CCM mkoa wa Tabora inateswa na siasa za makundi.

  CHANZO: NIPASHE (26/03/2011)
   
 2. Mzee Wa Rubisi

  Mzee Wa Rubisi JF-Expert Member

  #2
  Mar 26, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 1,754
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  mtakulana wenyewe kwa wenyewe
   
 3. P

  Popompo JF-Expert Member

  #3
  Mar 26, 2011
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 411
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  Tatizo la UVCCM HAWANA BUSARA NA MAADILINA JUU YA YOTE NI WAKURUPUKAJI BIG TIME:crutch::hatari:
   
 4. engmtolera

  engmtolera Verified User

  #4
  Mar 26, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 5,081
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  sio busara tu pia wamepungukiwa maadili ya kiuongozi wao hudhani kuongoza ni kukurupuka na kufanya maamuzi ya kukomoana,kwa mtindo huu wao ndio wanao kipeleka chama kaburini,kwani wanadhani kuwa maamuzi yao yatakiendeleza chama kumbe ndio yanakibomowa chama

  Nacho juwa mimi Jumuia ya umoja wa vijana kabla ya kufanya kikao ni lazima mlezi wa chama uvccm awe na taarifa nikimaanisha katibu wa chama mkoa,wilaya,kata hata tawi kulingana na kikao husika kinafanyika ktk ngazi ipi ya taifa,mkoa,wilaya,kata ama tawi

  sasa kama katibu hajui nini kiliendelea inamaanisha kuwa uvccm ilifanya mambo kwa hasira kwa lengo la kumkomowa Mh sitta
  Hizo chuki zenu wana Uvccm mnakiangusha chama kinachowalea
   
 5. LINCOLINMTZA

  LINCOLINMTZA JF-Expert Member

  #5
  Mar 26, 2011
  Joined: Mar 15, 2011
  Messages: 1,640
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Tatizo si UVCCM, Tatizo ni Uongozi wa juu ambao umekamatwa na mafisadi. Hawa ni vijana ambao wanaongozwa vibaya na mafisadi. Mimi huwezi kunishawishi kwamba watu wa Pwani hasa wale wa Mkoa wa Pwani, Tanga, Mtwara na Unguja wanaweza kuongoza nchi au taasisi kubwa. Hawa ni mdebwedo kabisa. Sasa wameshikilia serikali lakini hawajui wafanye nini zaidi ya majungu tu. Mifano ipo kwa uongozi wa juu kila mtu anajua.
  Haya yote yanafanyika wakiwa wamepanga wakubwa wakifikiri ni siasa nzuri kumbe ni hewa tupu. Siwashaangi kwani hii ni kwa sababu ya asili yao, Pwani yote mdebwedo, mdebwedo, mdebweoooooooooo. Kuna wala ubwabwa wasiojua ulikotoka. Tunahitaji kuchukua nchi yetu tuwaongoze hawa watu hawawezi kazi.
   
 6. Hero

  Hero JF-Expert Member

  #6
  Mar 26, 2011
  Joined: Aug 20, 2010
  Messages: 786
  Likes Received: 137
  Trophy Points: 60
  Nakubaliana na wewe 100 %!
   
 7. TUKUTUKU

  TUKUTUKU JF-Expert Member

  #7
  Mar 26, 2011
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 11,852
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  kWELI SASA VITA VIMEPAMBA MOTO!!!
   
 8. Alwatan

  Alwatan JF-Expert Member

  #8
  Mar 26, 2011
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 409
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Hao unaowaita mdebwedo ndio waliokuwa mstari wa mbele kupigania uhuru wa nchi hii wakati wazee wako walipokua busy kitandani kuwafurahisha wakoloni huko bara. Soma historia, Shwain mkubwa we!
   
 9. Hero

  Hero JF-Expert Member

  #9
  Mar 26, 2011
  Joined: Aug 20, 2010
  Messages: 786
  Likes Received: 137
  Trophy Points: 60
  Kweli kuna kazi! Kama watu wetu ndio wanawaza kama wewe, ipo kazi:lol::lol::lol:
   
 10. MAMMAMIA

  MAMMAMIA JF-Expert Member

  #10
  Mar 26, 2011
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 3,822
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 0

  Ndio kwanza niafahamu kuwa Tabora iko Mikoa ya Pwani. Asante sana kwa kutuhabarisha.
   
 11. only83

  only83 JF-Expert Member

  #11
  Mar 26, 2011
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 5,252
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180
  Jamani hawa watu wanalengo la kututoa kwenye mada za msingi....hizo kelele zinazoedelea huko ni kutuzingua tu.....sasa hivi Katiba kimya,Umeme Kimya...kinachoendelea ni UVCCM vs Sitta nk......................
   
 12. Mo-TOWN

  Mo-TOWN JF-Expert Member

  #12
  Mar 26, 2011
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 1,629
  Likes Received: 140
  Trophy Points: 160
  The unbecoming behaviour shown by UVCCM is a result of the failure in party leadership at the top. Imagine these dayz everyone is a spokesperson for the party let alone what they communicating.
   
Loading...