Dah ccmCCM sio chama cha kisiasa ni kikundi tu cha MATAPELI na WALAGHAI!
Wakuu, CCM sina hamu nao, Maji hakuna, Umeme bei juu tena unapatikana kwa shida, Shule za kayumba walimu hakuna, vitabu hakuna, Nikiumwa hospitali hazina dawa, Mchele bei juu, Sukari bei juu, Usafiri ni balaa, Vifaa vya ujenzi bei juu siwezi kununua - - naombeni ushauri watanzania wenzangu wapi pa kukimbilia!! nimedata mwenzenu.
acha uongo umepatawapi simu,bundle na umecharge na kitugani kamasio umeme!!!!!!.
watu wanauza kuku na kununua petrol ya Riziwani kisha kuwasha generator ili wacharge sim.
chezea ccm weye....maisha bora kwa kikwete na watu wa pwani wengine hali mbaya usipime mkuu.
maisha Bora kwa kila mtanzania yamewezekana maana hata mimi ni muuza kuku wa kienyeji na nimefanikiwa kuwa na banda langu zuri na solar power Mkuu.
jeykey hoyeeeeeeeeee!
WAMA wangemsaidia huyu dogo aisee.
wanakijiji wametofautiana hali Mkuu kutokana na vipaumbele katika kilimo Mkuu mimi nilikopa finca kama laki7 tukiwa na kikundi chetu cha wauza kuku Hapa handeni nashukuru mambo yalienda vema kabisa nimelipa mkopo na sasa ninakuku wa kutosha ninawafuga kienyeji nina mbuzi pia wakutosha kuendeshea maisha.
Kumbe wa karibia na pwani?, vipi wale mbuzi wachinjwao kabuku bado wapo? maana sijaenda Tanga siku nyingi mkuu.
ndio soko letu kubwa Mkuu, ila nimejifunza
kitu kama serkali ingetumia elimu ya
vipaumbele vya aina ya kilimo basi ingefaa
iangalie maeneo mbalimbali na tabia zake hii
ingesaidia wakulima wengi na wafugaji.
panga biashara yako onyesha jitihada yako na
kakope ikibidi kukuza biashara yako.
mkuu sijakupinga si kwamba nakubaliana na hoja zako la.
-Tabora/mbeya wanalima tumbaku sana, nakuthibitishia kupitia hiyo mikopo serikali imeshindwa kuwasimamia wakulima wanakatwa na kuibiwa sana na vyama husika au wafanya bishara.
-Mtwara na korosho yale yale.............na hili nimaeneo takribani yote. nimepita maneo mbalimbali naongea nilichokiona.
-Mwanza na shinyanga mpaka singida wanalima pamba, lakini makato na ujanjaujanja mwingine umepelekea kuuwa zao hilo
hiyo mikopo unayoisema inawatesa sana wananchi kwasababu serikali yako imelala na wakulima wanaibiwa mno.