CCM Should start acting like "Chama Tawala", no other way around...!

Elly B

JF-Expert Member
Jan 11, 2011
1,194
906
Ndugu wana JF,

Katika kupitia makala ,nilikutana na mada hii ambayo nimeona inabeba ukweli usiotakiwa kupuuzwa......

KATIKA mfumo wa demokrasia ya vyama vingi, kazi ya chama tawala na vyama vya upinzani zinatofautiana sana. Kazi kubwa ya chama tawala ni kuisimamia serikali yake itekeleze yale iliyoahidi kwa wananchi wakati wa kampeni za uchaguzi na kuhakikisha kwamba mambo yaliyomo katika ilani yake ya uchaguzi yanaingia katika mfumo wa kisheria na sera za nchi.

Kwa hiyo katika majukwaa ya kisiasa chama tawala hujitahidi kuonyesha kwamba wanatekeleza waliyoahidi na huonyesha kwamba kweli mambo yanaenda vizuri kuliko kabla hakijaingia madarakani. Kwa hiyo, kazi ya chama tawala baada ya uchaguzi ni kutenda kwa sababu wana nyenzo za kutendea kazi, yaani serikali.

Kupitia utekelezaji wa mambo mbalimbali yaliyopo katika ilani yake, chama tawala hujitahidi kuonyesha mafanikio na kujenga hoja ya kuwafanya wananchi waliokichagua kuendelea kujivunia na kufurahia chaguo lao, wakati huo huo kikionyesha kwamba kama wangechagua wapinzani mambo yangekuwa mabaya.

Kwa hivyo, kazi ya chama tawala ni kusimamia utekelezaji na huhukumiwa kwa vitendo vya serikali yake. Chama tawala wakati wote huhakikisha kuwa harakati za vyama vya upinzani haziwatoi nje ya mstari wa kutekeleza sera zake.

Chama cha upinzani, kwa upande mwingine, kazi yake kubwa ni kuweka wazi udhaifu wa chama kinachotawala kwa kuonyesha wananchi kwamba mambo hayaendi kama walivyoahidiwa na kwa hivyo, walidanganywa.

Kwa kifupi, ni kazi ya chama cha upinzani kuwafanya wananchi wajutie kukichagua chama kilichopo madarakani na kuwajengea uelewa, ufahamu na ujasiri wa kukitoa chama tawala katika uchaguzi mwingine utakaofuatia. Chama cha Upinzani hujitahidi kuonyesha kwamba kama wangechaguliwa wao mambo yangekuwa mazuri zaidi kuliko ilivyo sasa.

Kwa hivyo, kazi ya chama cha upinzani ni kuuza maneno na huhukumiwa kwa maneno wanayoyasema. Wakati wote wakisubiri uchaguzi mwingine chama cha upinzani hujitahidi kupita huku na kule kuonyesha udhaifu wa serikali iliyopo na kuonyesha kwamba, kina sera na mipango bora zaidi ya kuipeleka nchi mbele zaidi.

Ni kazi ya chama cha upinzani kuhakikisha kwamba chama tawala kinatoka nje ya mstari na kuanza kuhangaika kujitetea. Dalili za mafanikio ya chama cha upinzani ni pale ambapo unaona chama tawala kinaanza kulialia na kujitetea.

Kama wewe ni mgeni katika nchi hii na kama uliingia nchini kwa mara ya kwanza siku ambapo CCM walifanya mkutano pale Jangwani (Jumamosi ya Juni 9, 2012), ungeamini kwamba chama hiki tawala ama ndio kwanza kilikuwa kimeingia madarakani kwa mara ya kwanza au kilikuwa kinaomba ridhaa ya kuchaguliwa.

Mawaziri waliendeleza kasumba sugu ndani ya CCM ya kumwaga ahadi ambazo wanajua hazitekelezeki. Mwakyembe anautangazia umma kwamba anaomba apewe miezi mitatu tu ili aweze kumaliza matatizo yaliyopo katika Wizara ya Uchukuzi.

Mwakyembe anataka tuamini kwamba suluhu ya matatizo ya sekta ya uchukuzi anayo mtu mmoja tu anayeitwa Waziri, na kwamba mawaziri wote waliopita katika wizara hii walishindwa kutatua matatizo yale isipokuwa sasa tumepata ‘mwarobaini' na mambo yatakuwa mazuri. Anataka tuamini kwamba, Mwakyembe ndiyo wizara na wizara ndiyo Mwakyembe!

Mwakyembe anaelewa vizuri kwamba ujenzi wa reli katika nchi hii umekwamishwa na serikali kushindwa kuwekeza fedha za kutosha katika sekta hii, na sote tumesikia taarifa kwamba katika mwaka wa fedha unaoisha ni chini ya asilimia 40 tu ya fedha iliyotengwa kwa ajili ya kuendeleza miundombinu ya reli ndiyo iliyotolewa na hazina.

Sasa Mwakyembe ana miujiza gani ya kutatua matatizo ya wizara hii katika miezi mitatu aliyoomba apewe? Mwakyembe na mawaziri wengine wapya wanaelekea kuamini kwamba ili waonekane wanachapa kazi ni lazima wafukuze watu kazi na watangaze kwa sauti kubwa kwamba tumewafukuza!

Tunarudia tena kuwaasa kwamba matatizo ya kiutawala katika nchi yetu na nchi nyingine kadhaa za kiafrika ni ya kimfumo na hayawezi kutatuliwa kwa kufukuza wafanyakazi tu. Tatizo letu ni kwamba tumekuwa tukifanya bidii ya kuimarisha watu badala ya kuimarisha mifumo ya kuwadhibiti viongozi.

Matokeo yake kiongozi mmoja anaweza akaja na jambo jema lakini likafa mara yeye atakapoondoka katika wizara husika. Na bahati mbaya mawaziri wa CCM hawakai muda wa kutosha katika wizara moja kabla hawajanyang'anywa uwaziri au kuhamishiwa wizara nyingine.

Tunamkumbusha Mwakyembe kwamba miezi mitatu aliyoomba itaisha mwezi wa tisa mwaka huu, na tutawaomba wabunge wamkumbushe kutoa taarifa yake katika Bunge la Novemba.

Mawaziri na viongozi wengine wa CCM walijikita katika kukipiga vijembe chama kikuu cha upinzani nchini, CHADEMA. Kimsingi wengi walikuwa wanajitetea na kulialia. Kwamba ugumu wa maisha umesababishwa na kupanda kwa gharama za mafuta duniani kote na kwamba CCM haipaswi kulaumiwa kwa hilo ni utetezi usio na maana yeyote.

Hakuna mtu anayesema kwamba ni lazima utatue matatizo uliyosababisha wewe tu. Matatizo ni matatizo tu, na unapokuwa kiongozi yakupasa kujua kwamba upo hapo ulipo kwa ajili ya kushughulikia matatizo, sio kujitetea.

Kuilaumu CHADEMA kwa kuibua matatizo yaliyopo na kuonyesha udhaifu wa serikali iliyopo ni kujaribu kuwazuia wasifanye kazi yao ya kuwa chama cha upinzani. Ni muhimu kusisitiza hapa pia kwamba kazi ya chama cha upinzani sio kuisaidia serikali ijirekebishe.
Chama cha Upinzani kikiamua kufanya kazi ya kuirekebisha serikali maana yake ni kwamba kimeamua kuendelea kuwa chama cha upinzani milele. Kazi ya kuirekebisha serikali ni kazi ya taasisi za kiraia (NGOs) ambazo hazina malengo ya kutawala. Na isitoshe serikali ina vyombo tele vya kuishauri na kuirekebisha.

CCM wanapouza maneno na kulalamika barabarani badala ya kuisimamia serikali yao itekeleze ahadi zake ni kuzidi kupoteza mwelekeo, na kimsingi wanafanya kazi ya upinzani.

Kuendelea kutoa ahadi wakati upo madarakani ni kutokuelewa kazi za chama tawala. Ndiyo maana sasa tunauliza, CCM inapoamua kufanya kazi ya upinzani, nani atafanya kazi ya chama tawala?

*makala hii ni kutoka Raia Mwema

Binafsi nadhani wananchi wanahitaji mabadiliko(they deserve it) . Wanahitaji mabadiliko ya kiuchumi, kimfumo, kiutawala na hata kifikra. Kuendekeza malumbano badala ya kuprovide solution ni dalili ya kuzidiwa majukumu. Nadhani ni muda wa CCM kuanza kuonyesha utekelezaji wa kile walichoahidi na si vinginevyo.
 
Mkuu wana miaka miwili imebaki.
Wamekuwa madarakani kwa miaka mingapi?
Ndo waanze leo?
Hata wao wamechoka wanasubiri tu miwili iishe liwalo na liwe
 
Siyo kwamba waanze kujifunza namna ya kuhoji utendaji wa serikali iliyoko Madaraki?
 
Siyo kwamba waanze kujifunza namna ya kuhoji utendaji wa serikali iliyoko Madaraki?[/QUOTE


Na haswa ndiyo maana ya dhana ya kuisimamia serikali yao. instead na wao wanalalamika viwanjani na kulaumu wapinzai. Wanajibu vijembe kwa vijembe badala ya vitendo. Sasa nani anatawala na nani mpinzani. Nini maana ya kuwa naserikali na resources kama all you can afford ni maneno?
 
Mkuu wana miaka miwili imebaki.
Wamekuwa madarakani kwa miaka mingapi?
Ndo waanze leo?
Hata wao wamechoka wanasubiri tu miwili iishe liwalo na liwe

Kwenye la kuchoka hilo ni wazi kabisa. otherwise they need to do some critical thinking and show the difference.
 
Mimi nadhani sasa niwakati wa wananchi kutambua nini maana ya maendeleo katika nchi na mtu mmoja mmoja kwa ujumla, pia kwa kulitambua hilo ni hakikaka wanaweza kuangalia chama tawala kimetekeleza mangapi pamoja na kukopa ilani kutoka vyama pinzani yani inamaanisha wamejitwisha mizigo mingine pasipo kutambua kua hiyohiyo ilani ya chama chao wameshindwa kuitendea haki na kubaki kufanya danganya toto kwa watu wazima, wamesahau kua taifa walilokua wakiliongoza hapo mwanzo lilikua la watu wengi wasio kua na mwanga (namaana wasomi walikua wachache) lakini hilo tu pia halitoshi ni kwamba uozo uliokua ukifanyika haukua unaonekana kama sasa ambapo watu wengi wanapata taarifa na kuchangamanua yanayotendeka, kwa kiwango hiki ilicho fikia sasa ni kweli bado hawajajua nini cha kufanya na kutafuta njia ya kutokea ambapo nasikitika kua milango yake nayo teari imefungwa kwa maana watu wanatambua nini kinaendelea.
 
Huwa ccm hajitambui kuwa ni chama tawala imeishia kuikosoa CDM ambayo haina serikali ccm inajilinganisha na TLP
 
Mimi nadhani sasa niwakati wa wananchi kutambua nini maana ya maendeleo katika nchi na mtu mmoja mmoja kwa ujumla, pia kwa kulitambua hilo ni hakikaka wanaweza kuangalia chama tawala kimetekeleza mangapi pamoja na kukopa ilani kutoka vyama pinzani yani inamaanisha wamejitwisha mizigo mingine pasipo kutambua kua hiyohiyo ilani ya chama chao wameshindwa kuitendea haki na kubaki kufanya danganya toto kwa watu wazima, wamesahau kua taifa walilokua wakiliongoza hapo mwanzo lilikua la watu wengi wasio kua na mwanga (namaana wasomi walikua wachache) lakini hilo tu pia halitoshi ni kwamba uozo uliokua ukifanyika haukua unaonekana kama sasa ambapo watu wengi wanapata taarifa na kuchangamanua yanayotendeka, kwa kiwango hiki ilicho fikia sasa ni kweli bado hawajajua nini cha kufanya na kutafuta njia ya kutokea ambapo nasikitika kua milango yake nayo teari imefungwa kwa maana watu wanatambua nini kinaendelea.

I agree
 
Back
Top Bottom