CCM: Seif ajiandae kuanguka tena Oktoba | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM: Seif ajiandae kuanguka tena Oktoba

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by MziziMkavu, Jun 9, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Jun 9, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,617
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad  Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar kimesema Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad, anaota ndoto ya mchana kujitabiria kuingia Ikulu kwa kuwa hatashinda katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 31, mwaka huu.
  Hayo yameelezwa na Katibu wa Idara ya Itikadi na Uenezi wa Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM Zanzibar, Vuai Ali Vuai, alipokuwa akifunga mafunzo kwa makatibu wa CCM wilaya na makatibu wa uenezi wa chama hicho mjini hapa. Alisema CCM inaamini itashinda kwa kishindo kutokana na kazi kubwa ya utekelezaji wa ilani yake kuwasogezea maendeleo wananchi, hasa kisiwani Pemba.
  Alisema kauli za Maalim Seif kudai kwamba CCM itaanguka katika uchaguzi haina maana kwa vile CCM ushindi wake umekuwa ukiongezeka kila uchaguzi. Vuai alitoa kauli hiyo kufuatia matamshi ya Maalim Seif alipokuwa akichukua fomu ya kugombea Urais wa Zanzibar, ambapo alisema maridhiano ya kisiasa yaliyofikiwa kati yake na Rais Karume inaipa nafasi CUF kushinda katika uchaguzi huo.
  Hata hivyo, Vuai alisema CCM imepata moyo kuona Maalim Seif amesifia maandalizi mazuri ya uchaguzi huo na kumsihi asijekubadilika na kuyakataa matokeo baada ya kushindwa.
  Vuai alisema CCM ina matumaini makubwa ya kuongeza viti katika nafasi za ubunge na uwakilishi kisiwani Pemba kutokana na mafanikio makubwa yaliyopatikana katika utekelezaji ilani yake ya uchaguzi.  CHANZO: NIPASHE
   
Loading...