LUS0MYA
JF-Expert Member
- Aug 4, 2011
- 862
- 1,097
Nimejaribu kufuatilia siasa za Zanzibar na kubaini mambo yafuatayo;
1.Wazanzibari wengi wanahitaji Muundo wa serikali ya mkataba na sio serikali mbili au tatu.Wazanzibari hawa wapo ndani ya CCM na CUF.
2.Baada ya kuunda SUK wazanzibari wamekuwa wamoja katika kudai masilahi yao ndani ya Muungano na sio siri tena Wazanzibari wakiwemo wanaccm wanaamini kwa kupitia CUF maslahi yao katika muungano yatatatuliwa kwa haraka zaidi hasa kwa kuzingatia kuwa CCM kama chama kikongwe kuna mahafidhina wasiohitaji mabadiliko kwa kutumia mgongo wa mapinduzi ili kulinda masilahi yao.
3.Wazanzibari wengi wamegundua kuwa uhasama wa kisiasa baina ya vyama vikuu(CCM na CUF)ulirudisha nyuma kasi ya kudai haki katika Muungano na ilipoundwa SUK mahitaji yao mengi yametekelezwa katika kipindi kifupi sana na hata masuala ya haki ya mafuta yametatuliwa pamoja ilikuwa ni kilio cha wazanzibari miaka mingi.
4.Wazanzibari wengi hawaguswi na chama kipi kitaongoza serikali lakini wanafikiri ilani ya CUF imebeba mahitaji ya wazanzibari bila kuchujwa kulinganisha na ile ya CCM
5.Mgawanyo wa kura zilizotangazwa zilionyesha waziwazi mwelekeo wa mahitaji ya wazanzibari kwani CUF ilipata kura nyingi za wanaccm katika maeneo yote ya unguja na Pemba.