CCM, Rais Samia, maslahi na makundi mnajiua Kisiasa kuelekea 2025

voicer

JF-Expert Member
Jul 13, 2020
5,553
11,885
Habari Member's JamiiForums

Tuyasemayo ni yale tunayoyaona.
Tuyasikiayo ni yale Yasemwayo na Jamii.

Mnautumia muda mwingi sana mkicheza rafu kwa wenzenu.

Wakati nyie mkitumia misafara na mikutano ya kiserikali kwa kampeni kupitia sifa kwa Mama tena kwa nguvu ya 5G.

Wenzenu mmewalazimisha kuweka mpira kwapani muda woote.
Na hata wanapotumia sebuleni kwao kujadili ya kwao inakuwa ni kwa bahati- bahati tu. kutegemeana na uelewa wa Kamanda wa Machozi wa eneo husika.

Hiyo si hoja kuu kwa leo .

Leo tuongee jinsi CCM-Samia mlivyokazana kuwekeza kwa mtu mmoja na kwa nguvu zoote.

Yeyote atakaeonekana kuwa na maoni tofauti na mwenyekiti anageuka kuwa adui wa chama kizima.
Wahuni wanaita wenzao viroboto bila chama kukemea!

Uko wapi uhuru wa kujieleza na kutoa maoni kwa maslahi mapana ya chama?

Sasa hivi Dira ya chama imekuwa ni kusifia mwenyekiti tu.

Je kufikia 2025 wananchi watawezaje kuwapembua wagombea wenu na kuwajua umahiri wao kiuongozi,Weledi,Ubunifu nk.

Nasema hivyo kwa sababu zifuatazo.

Moja ni kwamba kuanzia bungeni kwa wabunge.
Hasa baada ya @Ndugai kufurushwa!

Hatuoni wakitumia uwezo na elimu zao kuwajibika kuibana serikali ipasavyo ili kuwatatulia kero wananchi wao majimboni.

Na wao ni kama wametishika!

Badala yake ni mapambio na kuunga mkono hoja tu.

Huku nje ya bunge kwa mawaziri, ma-RC,ma-DC kote kauli ni moja tu...Nimetumwa na
Mh Samia Suluhu Hassan.

Hakuna mahali tunaposikia waziri au mkuu wa mkoa akitumia uwezo wake na uelewa wake kutoa maamuzi bila kusema anatimiza maelekezo ya Samia.

Walau kidogo kwa wakuu wa wilaya baadhi wanajitahidi kujituma wao binafsi.

Sasa basi niwaulize....wakati wa kampeni huko majimboni mtapita mkituambia kwamba Samia amewatuma mje kugombea na tuwape kura?

Bila kujali mmejituma na kutumia uwezo wenu binafsi kutupigania kiasi gani sisi wapiga kura wenu.
Katika kutatua kero zetu majimboni?

Kumbukeni kuwa ujenzi wa madarasa na maboma ya hospitali bila walimu wenye ubora kutufundishia maarifa mazuri watoto wetu bado halijatatuliwa tatizo sugu.

Mahospitali kuwepo bila kurekebisha bei ghali kwa mwananchi kuhakikisha hafi kwa kukosa pesa bado tatizo la msingi halijatatuliwa.

Kuna kero nyingi huko mitaani,kote mijini na vijijini ambazo zinahusu maisha ya siku kwa siku na "hand to the mouth" hususani mifumko ya bei hata kwa vitu ambavyo havihusiki na uagizwaji nje ya nchi.

Lakini serikali,wabunge na chama chote CCM hamuonekani kuguswa na hili ila kwenu muhimu ni ...nani kama Mama!

La pili ni kuzima ndoto za wanachama wote wanaoonekana kuwa na mawazo tofauti na tishio kwa uraisi wa Mama.

Tumeona wakifukuzwa makatibu zaidi ya mia tatu kote nchini na kwa wakati mmoja.kisa tu mwenyekiti anajenga himaya yake mpya.

Tumeona wakiteuliwa makatibu wenezi waliokwishakuwa na kashfa za rushwa huko awali.
Lakini kwa upendo wa mama wao wanapeta kwa sasa.

Tumeona nguvu ya mwenyekiti kwa kuondoa watendaji wakuu wa chama bila kujali mchango wao kutokana na uchaguzi uliopita.kisa tu ni hofu ya kuelekea 2025.

Tumeona pia Wakiibuka wana CCM maslahi wenye kashfa zao kibao huko nyuma,tena waliostahili kuwa jela kwa sasa.

Lakini wanajitokeza na kuwakejeli wale waadilifu kuwa CCM ina wenyewe na sasa ni zamu yao kupeta.Chama hakijitokezi kukemea na kujitenga na kauli hizo.

Tumeona mawaziri wasio na rekodi za uadilifu huko tulikotoka,wakirudishwa na kutamba kwa kuendelea na visasi badala ya kazi na maendeleo.

Tumeona mawaziri wazuri wenye rekodi nzuri wakiwapisha wahuni kuingia kufanya uhuni na huku hawa wengine wakivutwa bench Ikulu kufungwa midomo.
Kisa uchaguzi 2025.

Tumeona wale wanaopinga Uhuni kwenye chama wakiondolewa bungeni na kutupwa nje ya nchi.

Je CCM mnategemea kutoboa kwa ngongo wa mapambio tu?

Je tukisema sasa wahuni wamekiteka chama kweli tutakuwa na makosa?

commonmwananchi
10101.
2022.
 
Umeandika Ukweli mtupu.Ninashauri Kiongozi aliyepo madarakani sasa ajiuzulu tu ili kupisha uchaguzi utakaoondoa makundi na kurudisha umoja,uzalendo na mshkamano miongoni mwa watanzania
 
Umeandika Ukweli mtupu.Ninashauri Kiongozi aliyepo madarakani sasa ajiuzulu tu ili kupisha uchaguzi utakaoondoa makundi na kurudisha umoja,uzalendo na mshkamano miongoni mwa watanzania
Mkuu
Vema kusema kile unachokiamini na kuiweka roho Huru.
Ujumbe uwafikie huko lumumba!
 
Umeandika Ukweli mtupu.Ninashauri Kiongozi aliyepo madarakani sasa ajiuzulu tu ili kupisha uchaguzi utakaoondoa makundi na kurudisha umoja,uzalendo na mshkamano miongoni mwa watanzania
Haitokaa itokee. Unajua why?
Ccm yenyewe inayapenda hayo makundi kwa ajili ya mtaji wa kisiasa.
And you think akiuzulu rais ndio umoja utapatikana? Damage goes deeper beyond that.
 
Umendika ujinga mwingi afu walio "Like" na ku "comment" ni wachache. Ndugu harakati zina wenyew humu, usione bavicha akiandika utumbo wake anapongezwa na walevi wenzake afu na ww ukafikiri itakuwa hivyo kwa upande wako.

Unaona sasa uzi wako ulivyododa? Bavicha wote wanaupita kama hawauoni, kisa ni kwa sababu ww pamoj na kujipendekeza kwao lkn sio mmoja wao. Hili liwe funzo kwako na kwa wajinga wenzako, kabla ya kuandika uzi unatakiwa ujitafakari kwanza.

Bora data zako ulizopoteza kwa uzi huu ungezitumia kuangalia udaku huko YouTube.
 
Umendika ujinga mwingi afu walio "Like" na ku "comment" ni wachache. Ndugu harakati zina wenyew humu, usione bavicha akiandika utumbo wake anapongezwa na walevi wenzake afu na ww ukafikiri itakuwa hivyo kwa upande wako. Unaona sasa uzi wako ulivyododa? Bavicha wote wanaupita kama hawauoni, kisa ni kwa sababu ww pamoj na kujipendekeza kwao lkn sio mmoja wao. Hili liwe funzo kwako na kwa wajinga wenzako, kabla ya kuandika uzi unatakiwa ujitafakari kwanza. Bora data zako ulizopoteza kwa uzi huu ungezitumia kuangalia udaku huko YouTube.
Siandiki ili kupata followers bali ninayatoa yote ya moyoni bila kuegemea upande wowote

Kwangu ukweli ndio muhimu.

Mimi si mfuasi mahaba bali msumeno speaker

The voice of the voiceless
Nashukuru kwa Kuitwa mjinga na "MHUNI"

Mimi sina budget ya bundle na niko online muda wowote ninaohitaji katika maisha yangu.

Usinipangie cha kusema!
Usinipangie Cha kuongea!
Usinipangie cha kuandika!

Inatumika akili na Pesa yangu binafsi.

Kamwe mfuasi wa wezi hawezi kubaliana na ukweli halisi.
commonmwananchi
10101.
2022.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom