CCM polepole mnapoteza grip ya nchi -- kwa nini hamtaki kuamini?

Zak Malang

JF-Expert Member
Dec 30, 2008
5,404
233

Sawa CCM wameshinda Igunga, lakini siyo kwa kishindo kama vile wangependa au kawaida yao ya zamani. Kwa lugha yoyote ile CDM ndiyo chama kinachokuwa kwa kasi na kinaonekana ni unstoppable (hakizuiliki).Ni wachache ndani ya CCM wanakubali kama CCM inaanza kupoteza grip ya nchi.

Angalia, miezi 12 iliyopita katika uchaguzi huo wa Igunga CCM 35,000, CDM 0 na CUF 11,000.
Sawa CDM hawakuweka mgombea. Lakini leo hii CCM wamepoteza kura 9,000 kwenda CDM na pia kuchukuwa zile 11,000 za CUF na pia kukwangua yingine zaidi.

Nawauliza CCM: Kupoteza kura 9,000 maana yake nini? Jinsi tunavyokwenda hali hii itakuwa inajnirudia kama vile ilivyojitokeza katika uchaguzi wmkuu wa mwaka jana -- CCM kazi yao kubwa ni kupoteza kura tu -- hata kama wanafanikiwa kuchukuwa viti. Na kwa vile CCM wanashindwa kujirekebisha, basi hakuna njia ila mwisho wake ni kutokomea huko kwenye kaburi la sahau. Bashe aliwaambia hivyo bila kutafuna maneneno akiwa Geita.

Kwa hiyo wakati CCM inasherehekea ushindi wake huo, watu wenye akili ndani ya chama hicho wanaliona hilo -- maana liko waaaazi kabisa. Watch out.

Aidha fikiria ni fedha ngapi CCM wametumia katika kuhangaika kulibakisha jimbo hilo -- na hata hivyo bado kwa kupoteza kura 9,000!

Ila kinacholeta wasiwasi ni kwamba inaweza kufika mahala CCM wakaanza kukataa kuporomoka kwao na hivyo kutumia njia za kinguvu kubakia madarakani huku wananchi wanakipa mgongo.
 
Nakubaliana na wewe Mkuu: Hata kwa wale wanaosema ushindi ni ushindi hata kama ni mdogo wafahamu kwamba chama chochote cha siasa duniani huanza kupotea polepole na jinsi kinavyozidi kupotea ndiyo jinsi kinavyoleta matatizo makubwa kwa wananchi.

Ningependa JK, Mkuu wa CCM alitambue hilo kwani imesemwa sana kwamba chama kitamfia mikonono mwake. Kama hatki hilo kutokea, basi afanye maamuzi mazito kurekebisha hali.

Sioni hilo kufanyika. Hebu ona -- imebidi CCM imwangukie Rostam fisadi mkuu asiyependwa na wananchi wengi ili asaidie kampeni kwa kutoa helkopta. Yaani CCM haiwezi kujitutumua kutoa helkopta yenyewe hadi itoke kwa huyo huyo fisadi? IKO KAZI KWELI KWELI.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom