..Ccm haina culture ya kujadiliana hoja kwa hoja mpaka hoja iliyobora ishinde.
..mara nyingi hoja na mitizamo ya mwenyekiti ndiyo hupitishwa harakaharaka.
..wanaoonekana kutofautiana na mwenyekiti huitwa majina mabaya na kumalizwa kisiasa.
..utamaduni huo umekuwepo tangu enzi za Mwalimu Nyerere ambapo wengi waliotofautiana naye waliitwa majina mabaya kama wasaliti, vibaraka, etc etc.
..kwa mfano, wakati hali yetu ya uchumi ni mbaya miaka ya 1980 kuna baadhi ya viongozi walianza kudai marekebisho ya sera zetu za uchumi. viongozi hao walipewa majina mabaya na wenzao ikiwemo kuitwa wasaliti na baadhi yao walianguka ktk chaguzi mbalimbali za Ccm.
..Udini, ukabila, ukanda, uzushi, ukatili, ni baadhi ya mbinu zinazotumiwa ndani ya Ccm kuwakabili wale wanaotofautiana na mwenyekiti, au walioko nje lakini wanakitishia chama chao.