CCM njia panda | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM njia panda

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mungi, Nov 27, 2011.

 1. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #1
  Nov 27, 2011
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 441
  Trophy Points: 180
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"] Saturday, 26 November 2011 20:11
  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]
  CHADAIWA KILIKURUPUKA KUJIVUA GAMBA, SASA KIMEKWAMA

  Claud Mshana

  WAKATI CCM imemaliza vikao vyake vikuu vya maamuzi mjini Dodoma juzi bila kufikia kikomo cha dhana yake ya kujivua gamba, wasomi, wanaharakati nchini wamedai chama hicho tawala kilikurupuka ndiyo maana imeshindwa kutekelezeka.


  Wakizungumza na gazeti hili kwa nyakati tofauti jana, wasomi, wanaharakati na wanasiasa hao walisema kuwa, chama hicho hakikufanya utafiti wa kina kujua madhara ya mkakati wake wa kujivua gamba kabla ya kuutangaza, matokeo kimeshindwa kufikia mwafaka na Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM wameuacha kiporo kwa Kamati Kuu ya chama hicho.

  Walisema kuwa, kama chombo kikubwa cha maamuzi cha chama (NEC) kimeshindwa kulimaliza jambo hilo na kulirudisha kwenye vikao vya chini badala ya kulipelekea kwenye kikao cha juu (Mkutano Mkuu) maana yake uhusiano wa chama na wanachama wake umekufa na kuna mgogoro mkubwa wa kidemokrasia ndani ya chama.


  Kauli za wasomi

  Mhadhiri wa Sayansi ya Siasa na Uongozi wa Umma katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam UDSM), Bashiru Ally alisema suala la kujivua gamba limetoa picha mbili ndani ya CCM.

  Mosi, Dk Ally alisema inawezekana jambo hilo limerudishwa kwenye Kamati Kuu ili lipotee ‘kiaina' kwa madai ya kukosekana ushahidi wa kuwatia hatiani watuhumiwa wa ufisadi wanaodaiwa kukipunguzia umaarufu chama hicho miongoni mwa umma.

  Picha ya pili alisema ni kufa kwa uhusiano wa chama na wanachama wake, kwa sababu chombo kikubwa cha maamuzi kama NEC kinaposhindwa kuamua, ni dhahiri kuna tatizo kubwa ndani ya chama.


  "Kama kujivua gamba ni mageuzi makubwa, basi yangepelekwa kwa wanachama halafu hatua zingeendelea hadi kufikia Mkutano Mkuu. Kama hili halifanyiki basi kuna mgogoro wa demokrasia ndani ya chama," alisema Bashiru.


  Aliongeza kuwa tatizo lingine ndani ya CCM ni kufa kwa utamaduni wa mijadala na kwamba, matatizo ndani ya chama hayawezi kumalizwa ndani ya vikao viwili pekee.


  Bashiru alibainisha kuwa kilichotokea juzi Dodoma ilikuwa ni shughuli za makundi, lakini utendaji wa chama kwa upana na marefu yake.


  Naye Mhadhiri wa Sayansi ya Siasa na Uongozi wa Umma wa UDSM, Dk Benson Bana aliweka wazi kwamba, kujivua gamba haukuwa mkakati wala kauli mbiu stahiki kwa chama hicho.

  Dk Bana alifafanua kuwa dhana hiyo, haikuchambua maana halisi ya gamba lenyewe, ndio maana utekelezaji wake umekwama.

  "Mimi naona kujivua gamba kama kauli mbiu ambayo haikustahili, kwa vile maana yake ni pana sana. Magamba ni yapi au ni nani? Jambo hili walishindwa kuliweka bayana tangu awali na sasa linawashinda," alisema Dk Bana.


  Alieleza kuwa kujivua gamba kuliwahusu watu wachache ndani ya chama na sasa watu hao wamejisafisha na badala ya kuwa magamba, wanaonekana kupata nguvu zaidi ndani na nje ya chama hicho.


  "Zile zilikuwa tuhuma tu, hatuwezi kumhukumu mtu kwa kumtuhumu," alisema Dk Bana.

  Aliishauri CCM kujiimarisha kwenye ngazi ya matawi na kubadilisha mkakati wa kujivua gamba haraka kwa kuwa hauna tija kwa chama hicho.

  Mhadhiri mwingine wa Sayansi ya Siasa na Uongozi wa Umma wa UDSM, Dk Bakari Mohamed, alisema dhana ya kujivua gamba haikupaswa kuwalenga baadhi ya watu, bali ilipaswa kuangalia mfumo mzima wa chama kuanzia ngazi ya matawi hadi taifa.


  Alisema anaamini kuwa wakati CCM inakuja na mkakati huo hawakujua tatizo lilikuwa wapi na pengine hata dhana hiyo imekuja kwa shinikizo tu bila maono ya mbali.


  "Ni suala gumu, watawafukuza wangapi? Ndio maana wameona mchezo huu utawapeleka pabaya," alisema Dk Mohamed.


  Wanaharakati

  Mkurugenzi Mtendaji wa Chama Cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (Tamwa), Ananelia Nkya, alisema dhana ya kujivua gamba, imekosa mwelekeo kwa kuwa haikupata tafsiri sahihi tangu awali.
  "Dhana haikuwa haikufafanuliwa mapema kuwa nani ana gamba na nani hana, Mwanzo haukuwa mzuri ni kama walikurupuka," alisema Nkya na kuongeza;

  "Kama ni kusafisha chama, wangeweka wazi uchafu ni huu na ule, ili watu wajue wana gamba au hawana. Lazima wakae kama chama wafafanue gamba ni nini"


  Kwa mujibu wa Nkya, bila mambo hayo kufanyika, CCM kitaendelea kuwa chama kifisadi na mwisho wake hautakuwa mzuri.


  Kauli za wanasiasa


  Kwa upande wake Mbunge wa Wawi (CUF), Hamad Rashid, alisema kinachowasumbua CCM ni kushindwa kufanya maamuzi magumu.


  Rashindi alifafanua kuwa kitendo cha agenda kufikishwa ngazi za juu kwa ajili ya kutolewa maamuzi na kurudishwa tena ngazi za chini, huko ni kutetereka kwa chama.

  "Jambo kama hilo la mageuzi ni kubwa. Kama mmefikia hatua ya kufanya maamuzi ni busara yafanyike haraka, kuchelewa ni kuendeleza matatizo ndani ya chama na yatahamia hata katika utendaji wa serikali," alionya mwanasiasa huyo ambaye pia aliwahi kuwa Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni


  Nape Nnauye


  Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Nape Nnauye alipozungumza na gazeti hili kuhusu utata wa dhana ya kujivua gamba alisema: "Suala hili lilikuwa na pande mbili ambazo zote zilipitia hatua stahiki. Upande wa kwanza ulikuwa ni kwa watuhumiwa kujipima wenyewe na kuchukua hatua au chama kiwachukulie hatua."


  Aliongeza kuwa baada ya miezi saba kupita, wamewasilisha taarifa yao NEC kwamba , upande wa kwanza wa watuhumiwa kujipima na kuchukua hatua, haujatekelezwa.


  "Tumewasilisha ripoti yetu kuwa mwitikio wa kujipima haukuwa mkubwa mbali na yule mmoja aliyejiuzulu na Halmashauri Kuu imetuambia tukatekeleze awamu ya pili ambayo ni chama kuwachukulia hatua," alisema Nape.


  Naye Mkurugenzi wa Mambo ya Nje na Uhusiano wa Kimataifa wa Chadema, John Mnyika, alisema sakata hilo linaonyesha wazi kuwa NEC ya CCM haina uwezo wa kuchukua hatua.


  Mnyika alifafanua kuwa mtu anapotuhumiwa, kwanza anapaswa kuandikiwa barua ya kuelezwa makosa yake ili ajitetee, kisha kuhukumiwa.


  "Tangu Aprili hawajafanya hivyo suala hili limerudi kwenye Kamati Kuu kwa sababu halikuchukuliwa hatua mapema," alisema Mnyika ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Ubungo.


  Mnyika aliendelea kueleza kuwa CCM inachofanya ni sawa na kuwatapeli wananchi kwani waliwakumbatia mafisadi tangu mwanzo na sasa wanadai kuwa wanataka kupambana nao.


  Naye Mwenyekiti wa Chama cha NCCR-Mageuzi, James Mbatia alisema suala la kujivua gamba ni danganya toto ya CCM, lakini mwisho wa mchezo huo ni upatikanaji wa Katiba mpya.


  Katika kikao chake cha Aprili mwaka huu, Halmashauri Kuu ya CCM ilitangaza mkakati wa kujivua gamba kwa kuwaagiza wanachama wake wote wanaotuhumiwa kwa ufisadi wawajibike.  Mkakati huo ulioridhiwa na Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Kikwete, ulilenga kukisafisha chama hicho, kukipa sura mpya, hata hivyo haujatekelezwa hadi sasa kwani kinyume na matarajio ya wengi kuwa NEC iliyomalizika wiki iliyopita Dodoma ingetumia panga lake kuengua makada wanaoandamwa na tuhuma mbalimbali za ufisadi, suala hilo limerudishwa Kamati Kuu, kwa hatua zaidi.

  Hadi sasa ni aliyekuwa Mbunge wa Igunga, Rostam Aziz peke yake aliyetangaza kujivua gamba kwa kuachia kiti hicho na nyadhifa zingine zote ndani ya chama hicho, miongoni mwa viongozi na wanachama wanaotuhumiwa kwa masuala mbalimbali ya ufisadi.

  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. m

  matawi JF-Expert Member

  #2
  Nov 27, 2011
  Joined: Mar 29, 2010
  Messages: 2,055
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Naenda church kuiombea CCM ife kabisa na isizikwe tanzania maana ni mbegu mbaya sana
   
 3. m

  mopaomokonzi JF-Expert Member

  #3
  Nov 27, 2011
  Joined: Aug 2, 2011
  Messages: 312
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ukichaa sio lazime uokote makopo kuombea twiga awe na shingo fupi ni ukichaa nao, wahi kaombee
   
 4. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #4
  Nov 27, 2011
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 441
  Trophy Points: 180
  Kichaa wakati mwingine anawaona watu wengine vichaa. Wewe unaweza kuwa kichaa kweli!
   
 5. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #5
  Nov 27, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  waandishi wa habari wanahangaika na nadharia, kila siku ccm njia panda miaka nenda miaka rudi... waache nadharia waandike yanayotuhusu kwenye maisha ya kila siku, yaani nimechoka kabisa na siasa zinazoendelea zisizo na maamuzi wala nini zaidi ya chakula na yunifomu

  i think waandishi wakiamua ku-ignore siasa na kuelekeza nguvu zao kwenye ujenzi wa taifa basi tutaendelea.... lakini naona wako bize na siasa kupita kiasi wakati pesa zetu haziibiwi vyamani zinaibiwa serikalini

  speed in a wrong direction is irrelevant
   
 6. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #6
  Nov 27, 2011
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 441
  Trophy Points: 180
  Heshima kwako Mkuu,

  Mkuu uliyoyasema ni ya kweli na ya msingi sana. Lakini tambua kwamba maendeleo ya wananchi wa nchi hii yanategemea sana siasa safi na uongozi bora. kama mambo haya hayajakaa vizuri na maendeleo ya wananchi hayatakuwa katika chain nzuri.
  Maendeleo ya nchi hii yatapatikana kama CCM na serikali yake wataondoka madarakani.
  CCM wamesababisha mkanganyiko mkubwa kwenye uchumi wa nchi hii, wamesababisha nchi yetu iwe taifa tegemezi kwa zaidi ya asilimia 80 huku tukiwa na rasilimali za kutosha.
   
 7. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #7
  Nov 27, 2011
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,324
  Likes Received: 1,790
  Trophy Points: 280
  Nakubaliana nawe kabisa...nashauri sasa tuandike vitu vitakavyoweza kusaidia wengi,especially wakulima na wafugaji vijijini. Tulime na kuuza bidhaa kwenye masoko ya uhakika. Tujenge institutions ambazo zitatuwezesha kumiliki sehemu kubwa ya uchumi. Tufungue makampuni yenye nia ya dhati ya kutufanya tuwe wamiliki wa urithi wetu sisi kama watanzaniam
  Tuwaachie CCM balaa zao maana wafu watazika wafu wenzao, period!
   
 8. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #8
  Nov 27, 2011
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 441
  Trophy Points: 180

  Mkuu wakulima washachakachuliwa siku nyingi! Masoko yameingiliwa na Walanguzi kutoka Sirikalini, wanapanga bei kulingana na mahitaji yao, siyo kulingana na uzalishaji!
   
 9. Rweye

  Rweye JF-Expert Member

  #9
  Nov 27, 2011
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 15,047
  Likes Received: 3,080
  Trophy Points: 280
  mkuu japokuwa umenikaa mbali na sikuoni hata uso wako ila nimekupata na umeweza kueleweka japo siasa ndo kila kitu pia

  tatzo pekee hapa ni kwamba waandishi wetu hawajaenda shule na bado hawataki kwenda darasani,wamekaa na tuvyeti na tudiploma twao huku bado wanajiita waandishi,wataalamu mara watafiti...yaani upuuzi mtupu
   
 10. LOWE89

  LOWE89 Senior Member

  #10
  Nov 27, 2011
  Joined: Nov 18, 2011
  Messages: 149
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Nao wanahangaika ili waweze kuboresha hayo mahitaji muhimu ya watanzania, lakini hizo siasa zao za kifisadi ndizo zinakwamisha hata wengine waandike nini ili kiwe kipaumbele kwa maisha ya watanzania. Yanaibwa na kupotea mengi na tuyaonayo pia yanakatisha tamaa, mbaya zaidi hata inapodhihirika hatua stahiki hazichukuliwi. Basi tena tusome hizo siasa kwenye maandishi yao.
   
 11. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #11
  Nov 27, 2011
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 441
  Trophy Points: 180
  Tatizo kubwa haliko kwa waandishi wa habari, lipo kwa wasomaji wa habari. lazima tukubali kwamba waandishi wa habari wanafanya kazi yao ili kuuza habari. sasa wasomaji wengi wameshaathirika kisaikolojia, bila habari kuwa na siasa gazeti haliuziki.
  La msingi ni kuwaelimisha wananchi hasa wasomaji wa habari kujikita kusoma habari za maendeleo.
  Hata humu Jf endapo Member atapost habari ya Kilimo kwanza sidhani kama itapata wachangiaji wa kutosha. Lakini habari za siasa mara Chadema hivi au ccm hivi, watu watachangia kwa kiwango cha kutosha.
   
 12. Nicksixyo

  Nicksixyo JF-Expert Member

  #12
  Nov 27, 2011
  Joined: Jan 11, 2011
  Messages: 949
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Hata watoto wadogo waliopo shule ya msingi na majumbani hawataki tena kusikia neno ccm....Nilitembelea shule mmoja ambapo wanangu wanasoma nikiwa kama mzazi kwenye kamati ya shule nikawasalimu wakiwa morning parade...Wanafunzi hamjamboo hatujambo shikamoo baba,Marahaba..Nikauliza mwaweza imba wimbo wa Taifaaa? wakajibu tuliacha kuuimba maana sikuhizi hatupati uji..Nikajikuta mwenyewe nasema duuh..!! Nikachokoza zaidi kwa kusema CCM OOOYEEE.....Wakanijibu poweeeer..Waalimu na mimi binafsi tukabaki tunaangaliana..Nikawaambia haya jamani masomo mema..Kweli ccm imenuka hata mtaani...Nawapa pole na mashati yao ya kijani yaliyodariziwa kisanii kama walivyo wasanii kwa kauli zao.:embarassed2:
   
 13. i

  ibange JF-Expert Member

  #13
  Nov 27, 2011
  Joined: Dec 31, 2010
  Messages: 1,545
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Kwa sisi waandishi a habari, usipoandika siasa huuzi gazeti.
   
Loading...