CCM njia panda mjadala wa Katiba | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM njia panda mjadala wa Katiba

Discussion in 'KATIBA Mpya' started by Rutashubanyuma, Dec 30, 2010.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Dec 30, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,528
  Likes Received: 415,716
  Trophy Points: 280
  CCM njia panda mjadala wa Katiba Wednesday, 29 December 2010 20:50

  Hussein Issa
  WAKATI joto la madai ya katiba mpya likizidi kupanda, Chama Cha Mapinduzi (CCM), kimesema kinaweza kuitisha kikao maalumu kwa ajili ya kujadili suala hilo kama kitaona kuna umuhimu wa kufanya hivyo.

  Katibu Mkuu wa CCM Yussuf Makamba aliliambia gazeti hili jana kuwa kwa mazingira ya sasa, CCM haijaona haja ya kuzungumzia suala hilo kwani misimamo ya serikali ni ya CCM, lakini kama kuna haja kamati Kuu ya Chama hicho itaketi kulizungumzia.

  "Mimi kama Makamba siwezi kusema lolote ila Kamati Kuu ya CCM ndio pekee inayoweza kukaa na kujadili mapungufu yaliyopo katika katiba na kutoa ushauri kwa serikali,''alisema na kuongeza: "Lakini Serikali ni CCM na CCM ndio Serikali, hivyo kukiwa na lolote, lazima chama kijadili kwanza kiundani na baadaye kupeleka mapendekezo serikalini kwa ajili ya utekelezaji.

  " Makamba alitoa kauli hiyo kujibu hoja la Mdhamini wa CCM, Peter Kisumo ambaye alitaka CCM itolee kauli suala hilo na isiogope kuongoza mjadala wa katiba kwani suala hilo sasa limeshakuwa la jamii.

  "Tunaheshimu mawazo ya mzee wetu Kisumo kwani ikilazimika CCM tutakaa na kujadili hili suala kiundani na kama vipi ndugu yangu tutatoa tamko kama tulivyoshauriwa "alisema Makamba. Juzi mwenyekiti wa Baraza la Wadhamini la Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kisumo, alikitaka chama hicho kutoa tamko linaloonyesha msimamo wake kuhusu mjadala huo.
  Kisumo alisema CCM haipaswi kuogopa kuongoza mchakato wa mabadiliko ya Katiba kwa kuwa mabadiliko ya kiuchumi na kisiasa yaliyotokea nchini tangu mwaka 1977, yanalazimisha kuwapo kwa Katiba mpya.

  Kisumo, aliitahadharisha CCM na kuitaka iitazame vizuri agenda ya mabadiliko ya Katiba vinginevyo itaonekana ni agenda ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na kukipa umaarufu wa bure chama hicho.

  “Tusiogope suala la kuleta mabadiliko ya Katiba na mimi naitahadharisha CCM kama haitakuwa msitari wa mbele kuongoza agenda hii basi itaonekana ni agenda ya Chadema kama ilivyotokea katika suala la vita ya ufisadi,”alisema Kisumo.

  Mwanasiasa huyo ambaye alikuwa Makamu Mwenyekiti wa mabadiliko ya Katiba mwaka 1977, alifafanua kuwa mabadiliko ya katiba ya mwaka 1977 yalisukumwa na kuungana kwa vyama vya TANU na Afro Shiraz Party (ASP).
   
 2. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #2
  Dec 30, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,528
  Likes Received: 415,716
  Trophy Points: 280
  Kamati Kuu ya CCM imekwisha pitwa na hili vuguvugu la katiba Mpya na wapigakura wengi wanawaona ni kikwazo cha maewndeleo hapa nchini............CCM wanajua vyema katiba mpya itawaondoa madarakani kwa sababu hawana jipya zaidi ya kujenga mazingira ya ufisadi na dhuluma dhidi ya raia wanyonge.............................................Their game plan is up and it is for good...............
   
 3. s

  smz JF-Expert Member

  #3
  Dec 30, 2010
  Joined: Dec 18, 2010
  Messages: 251
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kwenye ngaszi ya CCM hili limepita, liko kweny level ya wananchi kupitia wawakilishi wao yaani Mabunge. Makamba anasema ccm ni serikali!! wapi mawazo mgando hayo.

  Mh. Mnyika keshawasilisha hoja hiyo tayari kwa katibu wa bunge, Makamba kaa kimya issue iko bungeni Februari. Kama na kipindi hiki utateuliwa tena utakutana nayo mjengoni. otherwise CCM imeshachelewa kushughulikia hii issue, subirini umma uamue, maana tukiwaachia nyie mtaanza kuweka viraka juu ya vingine
   
 4. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #4
  Dec 30, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,528
  Likes Received: 415,716
  Trophy Points: 280
  Katiba mpya moto CCM
  • Vigogo waendelea kupima upepo kimyakimya

  na Mwandishi wetu


  [​IMG] CHAMA cha Mapinduzi (CCM) kimeogopa kuzungumzia suala la Katiba mpya kikisema kuwa kinangoja kupata msimamo huo toka kwa Rais Jakaya Kikwete. Akizungumza na Tanzania Daima jana, Katibu Mkuu wa CCM, Yusuf Makamba, alisema wao kama chama hawawezi kuzungumzia suala hilo na kwamba msimamo utakaotolewa na mwenyekiti wao ambaye ni Rais ndio utakaokuwa wa chama.
  'Mimi nasema wahariri si walikaa na Waziri Mkuu'¦akasemaje...akasema atamshauri Rais sasa ukinitaka mimi niseme, nasema Katiba ipo lakini ninataka iwe na maudhui gani?
  'Lakini ukitaka msimamo wa chama mimi kama Katibu Mkuu nangoja yale ambayo mwenyekiti wetu wa chama ambaye ni Rais atasema na ndio utakuwa msimamo wetu wa chama,'� alisema Makamba.
  Alipotakiwa kuzungumzia suala hilo wao kama chama na kama taasisi wana msimamo gani, Makamba alisema serikali iliyoko madarakani ni ya Chama cha Mapinduzi (CCM) hivyo inasimamia ilani ya chama hicho.
  Alisema kama serikali inasimamia ilani ya chama chao hawawezi kutoa msimamo tofauti; hivyo kauli itakayotolewa na Rais ndiyo itakayokuwa ya chama.
  Mjadala wa kutaka Katiba mpya iandikwe umeshika kasi na Rais Kikwete bado hajazungumzia lolote kuhusu suala hilo hata baada ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, kuahidi kuwa atamshauri juu ya hatua ya kuundwa kwa jopo la wataalamu kuliangalia suala hilo.
  Madai ya Katiba mpya yameungwa mkono na wanasiasa wa kada mbalimbali, viongozi wa vyama vya upinzani, viongozi wastaafu, wanaharakati na wananchi wengine wakidai kuwa Katiba ya sasa ina upungufu mkubwa ambao hauwezi kumalizwa kwa marekebisho.
  Hata hivyo suala la kuandika ama kutoandika Katiba mpya limeonekana kuwagawa viongozi wa serikali kila mmoja akitoa kauli zinazompinga mwingine.
  Waziri wa Katiba na Sheria, Celina Kombani, yeye aliibuka akisema kuwa hajui wanaodai Katiba wanadai nini kwani hawajampelekea mapendekezo mezani.
  Kauli hiyo ya Kombani iliibua mjadala mkali, lakini kauli ya Waziri Mkuu Mizengo Pinda wakati akizungumza na wahariri kwamba atamshauri Rais liundwe jopo la wataalamu waangalie suala hilo ilionekana kuwatuliza wengi.
  Hata hivyo, hivi juzi Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Fredirick Werema, naye aliibuka kupinga madai ya kuandikwa kwa Katiba mpya, akidai kuwa iliyopo inafaa na kama kuna matatizo ifanyiwe marekebisho.
  Kauli ya Werema imetafsiriwa na baadhi ya wachambuzi kuwa ni hatua ya kumpinga bosi wake ambaye ni Waziri Mkuu, Pinda.
  Kadhalika wapo waliohoji wapi alikopata mamlaka Mwanasheria Mkuu huyo ya kuwaamulia wananchi wakati suala lenyewe hawajapelekewa kuliamua.
  Wakati hali ikiwa hivyo, Chama cha Wananchi (CUF) jana kiliitambulisha rasimu sifuri ya Katiba yao mpya kwa waandishi wa habari huku ikibeba vifungu mbalimbali vinavyopunguza nguvu na mamlaka ya Rais ikiwa ni pamoja kutaka Rais ashtakiwe pindi anapomaliza muda wake iwapo itabainika alifanya makosa yanayostahili kushtakiwa wakati akiwa madarakani.
  Akiitambulisha rasimu hiyo Naibu Katibu Mkuu Tanzania Bara wa chama hicho, Julius Mtatiro, alisema rasimu iliyowasilishwa juzi kwa Waziri wa Sheria na Katiba, Celina Kombani, ina Sura 16, ibara 131 na nyongeza 3 na ina kurasa 88.
  Aidha, rasimu hiyo pia imetoa mapendekezo ya kuwepo kwa serikali tatu ambapo Zanzibar iwe na serikali yake inayojitegemea na Tanzania Bara serikali yake huku serikali moja ya shirikisho ikiunganisha serikali hizo.
  Kutokana na mapendekezo ya muundo huo hata jina la nchi limependekezwa kuitwa Jamhuri ya Shirikisho la Tanzania ambapo pia itatoa haki na kwa magavana wa shirikisho.
  Aliendelea kutaja mapendekezo mengine kuwa ni pamoja na kuwepo kwa maadili kwa viongozi huku akisisitiza viongozi hao kuacha kujilimbikizia mali na kuwaheshimu wananchi wanaowaongoza.
  Alisema rasimu hiyo imependekeza kuwepo kwa muundo wa viongozi wanaochaguliwa na kupitishwa na Bunge huku akiwataja kuwa ni pamoja na Gavana, Mwanasheria Mkuu, makamishna wa serikali na mkurugenzi wa Takukuru.
  'Viongozi niliowataja ni wa mfano tu ili kuepuka kitendo cha Rais kuweza kuwapachika watu wake ambao ni marafiki katika vyeo mbalimbali jambo ambalo litaweza kusababisha hatari katika jamii mfano mzuri uliotokea sasa kwa Mkurugenzi wa Takukuru Edward Hosea anavyowasafisha wala rushwa na kushindwa kuwachukuliwa hatua za kisheria,'� alisema Mtatiro.
  Mtatiro alisema mabadiliko mengine ni pamoja na kuwepo kwa muundo wa baraza dogo la mawaziri 15 ambao watatumia fedha ndogo za walipa kodi na kupunguza ununuzi ya magari ya anasa kama ilivyo sasa.
  Alisema Katiba hiyo imeandikwa kwa kuzingatia mifano ya Katiba za nchi 30 katika bara la Amerika na Ulaya.
   
 5. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #5
  Dec 30, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,528
  Likes Received: 415,716
  Trophy Points: 280
  Jk sisi hatukumchagua kuwa Raisi wetu yupo kwa ridhaa ya JWTZ. TISS na NEC.....................kwa hiyo Makamba na CCM yao waendelee kumsubiria JK wao awape mwongozo wake lakini sisi tutatafuta viongozi wetu wapya wakutupeleka Nchi ya Ahadi..................................The Promised Land....................
   
 6. F

  Fanfa JF-Expert Member

  #6
  Dec 30, 2010
  Joined: Sep 25, 2009
  Messages: 538
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Mikamba ni taahira, hivyo si vyema kubishana na taahira. Wananchi ndo tutaamua na tulishaamua kuwa tunataka katiba mpya.
   
Loading...