CCM ni Ngangari

CCM ni Ngangari

kisugujira

JF-Expert Member
Joined
Aug 13, 2012
Posts
774
Reaction score
200
Leo hii huko mjini Sumbawanga Chama Cha Mapindunzi (CCM) kimeendelea kujiimarisha kwa kutimiza moja ya ahadi zake kwa kuwakopesha vijana ambao ni nguvu kazi ya Taifa hili pikipiki mia moja (100) bila riba! Kila mtu aliyepewa mkopo huo wa pikipiki yenye thamani ya shilingi milioni moja laki saba na sitini elfu (1,760,000/-) anatakiwa kulipa mkopo huo kila wiki kwa muda wa miezi saba!

Nchi hii ni yetu sote. Pikipiki hizo zikopeshwe kwa vijana nchi nzima kwa utaribu mzuri bila upendeleo. Ni vyema kuwawezesha vijana wasio na ajira kuliko kwenda kufanya harambee za ujenzi wa makanisa ambayo kama watu hawana ajira hawataweza kwenda kusali wala kutoa sadaka.

Mwaka 2015 si mbali. Hivyo basi ni vyema CCM ikaanza kutubu dhambi zake kwa kutoa misaada kwa vijana watakaofunga na kupeperusha bendera za kijani (CCM) kampeni halali zitakapoanza mwaka 2015 na kujitengenezea mapito mema kuelekea nchi ya ahadi.
 
acha kukurupuka which CCM are you talking about, CCM ya kinana, Nape,Mchemba you ought to be joking
 
Pitia sheria ya Takukuru uangalie maana ya rushwa, hiyo ni rushwa
 
Dawa ya ukosefu wa ajira siyo kukopeshana pikipiki, viwanda mlivyoua vifufuliwe na kufanya jitihada ya kutumia kodi zetu vizuri kwa kutengeneza mazingira safi ya uwekezaji wa viwanda!
 
Tunduruboy where are you? I'm very sorry that you're the only one that you've not heard these good news. It's true and not a joke buddy.
 
Dawa ya ukosefu wa ajira siyo kukopeshana pikipiki, viwanda mlivyoua vifufuliwe na kufanya jitihada ya kutumia kodi zetu vizuri kwa kutengeneza mazingira safi ya uwekezaji wa viwanda!

Mikakati iliyopo ni mingi na siyo kutoa mikopo ya pikipiki tu. Kodi zenu zitaendelea kutumika isivyo kama ilivyotumika kwa kununua mapikipiki. Hiki ni kirusi kimojawapo kati ya vile vilivyopo cha kuwafanya mwache chokochoko kisha msinzie na kusahau yaliyopita.
 
Mbona vijana tumeshajua kuelekea 2015 mutatugawia sana pesa na mali nyingi! Ila kwa taarifa tu mbaya kwenu kwamba tunajua hizo pesa ni zile ambazo mumezipata kupitia vyanzo haramu hususani UJANGILI,RUSHWA YA MIKATABA na UFISADI MIGODINI n.k. Na tumejipanga kiukweli kwa moyo mmoja kuwalia hizo hongo zenu,Na mulivyo na akili mbovu bado munaelekeza akili yenu kwenye kutafuta pesa zaidi na kibaya zaidi kwa mbinu na vyanzo haramu! Mukijidanganya ndizo zitakazowasaidia kuwarudisha madarakani kwenye uchaguzi ujao!,Niwakumbushe tu kwamba kupitia wasamalia wema tumeshaelimishwa hivyo tunatambua madhara ya kiongozi anayetumia pesa ambazo awezi kuelezea amezipataje kuja kununua madaraka! Na wasamalia hawa wameenda mbali zaidi kwa kutuambia;Kwa kuwa pesa hizi kwa namna yoyote zimetokana na rasilimali za taifa letu sote na nyie wasaliti wachache kutumia nafasi ya ukarimu,upole na ujinga wetu muliowekeza vichwani mwetu kwa takribani zaidi ya miaka 50 na kujinufaisha nyie wachache.Hivyo basi tumeshauriwa tuipokee hiyo RUZUKU yetu ambayo ni haki yetu,Kwani wahenga unena "HAKI HAIPOTEA JAPO INAWEZA KUCHELEWESHWA KWA MUDA MCHACHE TU".Hivyo hizi pesa munazotusambazia kuanzia sasa na kuendelea hata mukagawa magunia ya pesa bado heshima yenu haiwezi kurejea kwani hz ni haki yetu mulichokifanya nikuichelewesha tu! Na tutaendelea kuwachukia kwa sababu kuna wenzetu wamepoteza maisha na kupata vilema vya maisha ktk kipindi chote ambacho mumetucheleweshea hizi haki zetu.NB;Kuna watu wakichomwa na maneno haya makali na yenye kuwagusa watajifanya hawajui ninachokimaanisha! Sasa nawaambia namaanisha KULA ccm KURA cdm.
 
CHADEMA wakisikia hivi roho zao zinawauma sana. CHADEMA wanapenda kusikia meli imezama, ghorofa limeanguka, kanisa limelipuliwa na mambo kama hayo.

Shame on you CHADEMA. CCM inazidi kusonga mbele nyie endeleeni kusubiri matukio ili mpate la kuongea.
 
Ama kweli ukisikia kenge wewe ndiye mwenyewe; Rais wako kila siku yuko hapo magogoni anauliza wapi kuna msiba ama tukio la ajali ili apate nafasi ya kuwahi kwaajili ya kupiga picha na kujichekesha lakini kwa akili yako finyu unasema CDM ndiyo wanafurahia.

Pole sana, SUMU imekuwa diluted.
 
Leo hii huko mjini Sumbawanga Chama Cha Mapindunzi (CCM) kimeendelea kujiimarisha kwa kutimiza moja ya ahadi zake kwa kuwakopesha vijana ambao ni nguvu kazi ya Taifa hili pikipiki mia moja (100) bila riba! Kila mtu aliyepewa mkopo huo wa pikipiki yenye thamani ya shilingi milioni moja laki saba na sitini elfu (1,760,000/-) anatakiwa kulipa mkopo huo kila wiki kwa muda wa miezi saba!

Nchi hii ni yetu sote. Pikipiki hizo zikopeshwe kwa vijana nchi nzima kwa utaribu mzuri bila upendeleo. Ni vyema kuwawezesha vijana wasio na ajira kuliko kwenda kufanya harambee za ujenzi wa makanisa ambayo kama watu hawana ajira hawataweza kwenda kusali wala kutoa sadaka.

Mwaka 2015 si mbali. Hivyo basi ni vyema CCM ikaanza kutubu dhambi zake kwa kutoa misaada kwa vijana watakaofunga na kupeperusha bendera za kijani (CCM) kampeni halali zitakapoanza mwaka 2015 na kujitengenezea mapito mema kuelekea nchi ya ahadi.
Nilikuwa naamini ni panya tu wenye ubongo mdogo, kumbe hata baadhi ya binadamu wana ubongo mdogo. Hivi karne hii kuna watu ati wenye akili timamu wanaamini kabisa kwamba ukiwapa bodaboda vijana wote utakuwa umetatua tatizo la ajira nchini!!!!! Siwalaumu maana hata mafanikio mnayopigia debe kila siku ni ujenzi wa barabara.
 
Pitia sheria ya Takukuru uangalie maana ya rushwa, hiyo ni rushwa

Kama Takukuru wameshindwa kuchukua hatua kali za kisheria katika matukio mengine makubwa ya wizi,rushwa na kifisadi, katika tukio hili dogo lenye mwonekano wa mikopo nafuu ya pikipiki sidhani kama hata watafuatilia!
 
Kifupi huwezi kwenda sokoni na debe la maharage ukabadilisha kwa debe la maharage.
 
Kwa hiyo mmeona bodaboda ndio suluhisho la ukosefu wa ajira?...
 
Nilikuwa naamini ni panya tu wenye ubongo mdogo, kumbe hata baadhi ya binadamu wana ubongo mdogo. Hivi karne hii kuna watu ati wenye akili timamu wanaamini kabisa kwamba ukiwapa bodaboda vijana wote utakuwa umetatua tatizo la ajira nchini!!!!! Siwalaumu maana hata mafanikio mnayopigia debe kila siku ni ujenzi wa barabara.

Atanyelite bhukomu, kujugha koni jama? Mbona nasikia miundo mbinu huko Undali (ILEJE) imetengenezwa kiasi kwamba siku hizi hambebi tena nyugo vichwani kuzipeleka sokoni? Nani katengeneza?
 
Mbona vijana tumeshajua kuelekea 2015 mutatugawia sana pesa na mali nyingi! Ila kwa taarifa tu mbaya kwenu kwamba tunajua hizo pesa ni zile ambazo mumezipata kupitia vyanzo haramu hususani UJANGILI,RUSHWA YA MIKATABA na UFISADI MIGODINI n.k. Na tumejipanga kiukweli kwa moyo mmoja kuwalia hizo hongo zenu,Na mulivyo na akili mbovu bado munaelekeza akili yenu kwenye kutafuta pesa zaidi na kibaya zaidi kwa mbinu na vyanzo haramu! Mukijidanganya ndizo zitakazowasaidia kuwarudisha madarakani kwenye uchaguzi ujao!,Niwakumbushe tu kwamba kupitia wasamalia wema tumeshaelimishwa hivyo tunatambua madhara ya kiongozi anayetumia pesa ambazo awezi kuelezea amezipataje kuja kununua madaraka! Na wasamalia hawa wameenda mbali zaidi kwa kutuambia;Kwa kuwa pesa hizi kwa namna yoyote zimetokana na rasilimali za taifa letu sote na nyie wasaliti wachache kutumia nafasi ya ukarimu,upole na ujinga wetu muliowekeza vichwani mwetu kwa takribani zaidi ya miaka 50 na kujinufaisha nyie wachache.Hivyo basi tumeshauriwa tuipokee hiyo RUZUKU yetu ambayo ni haki yetu,Kwani wahenga unena "HAKI HAIPOTEA JAPO INAWEZA KUCHELEWESHWA KWA MUDA MCHACHE TU".Hivyo hizi pesa munazotusambazia kuanzia sasa na kuendelea hata mukagawa magunia ya pesa bado heshima yenu haiwezi kurejea kwani hz ni haki yetu mulichokifanya nikuichelewesha tu! Na tutaendelea kuwachukia kwa sababu kuna wenzetu wamepoteza maisha na kupata vilema vya maisha ktk kipindi chote ambacho mumetucheleweshea hizi haki zetu.NB;Kuna watu wakichomwa na maneno haya makali na yenye kuwagusa watajifanya hawajui ninachokimaanisha! Sasa nawaambia namaanisha KULA ccm KURA cdm.

Bwana Mudogo,maneno hayo yanachoma moyo. Mwenye masikio na asikie. Lakini next time utakapokuwa unakandamiza makombora usisahau kuweka aya. Usipofanya hivyo tutageuka mijusi kwa kutoa macho wakati tukisoma makomobora yako.
 
CHADEMA wakisikia hivi roho zao zinawauma sana. CHADEMA wanapenda kusikia meli imezama, ghorofa limeanguka, kanisa limelipuliwa na mambo kama hayo.

Shame on you CHADEMA. CCM inazidi kusonga mbele nyie endeleeni kusubiri matukio ili mpate la kuongea.

Napenda kuelewa tu, Kwamba CCM ni BENK, SACCOs au VIKOBA? Maana hivyo vyombo ndivyo vinavyoweza kukopesha wananchi. Je sheria ya nchi inaelezaji kuhusiana na Vyama vya siasa kukopesha wananchi? Bila shaka anaangukia Takukuru ambayo kitendo hicho ni rushwa.
 
Leo hii huko mjini Sumbawanga Chama Cha Mapindunzi (CCM) kimeendelea kujiimarisha kwa kutimiza moja ya ahadi zake kwa kuwakopesha vijana ambao ni nguvu kazi ya Taifa hili pikipiki mia moja (100) bila riba! Kila mtu aliyepewa mkopo huo wa pikipiki yenye thamani ya shilingi milioni moja laki saba na sitini elfu (1,760,000/-) anatakiwa kulipa mkopo huo kila wiki kwa muda wa miezi saba!.

1,760,00/= kwa Miezi saba .
embu tujaribu hesabu za Primary.

Kwa mwezi ni wiki NNE then kwa miezi saba ni 7 x 4 = 28 wiki.
kwahiyo kuna marejesho 28.

1760000/28 = 62857.14

sawa na 62,857/= ukigawa kwa siku saba ni 8,979/=

Kwa biashara ya Boda boda nayo ijua mimi sijuhiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii!
 
Back
Top Bottom