choga mkuu
JF-Expert Member
- Apr 11, 2016
- 283
- 110
Chama chetu ccm kimekuwa kikifanya siasa chafu sana ambazo kama vyama vya upinza vingeamua kufuata mfumo huo pasingelikuwapo aman na uelewano katika jamii. Chama chetu ccm kimekuwa kikiasisi kila mpango mwovu anaolenga kufuta vyama vya upinza na si kuvishinda katika uchaguzi kutokana na kukosa Sera na mipango inayokubalika kwa wananchi.
Aidha ccm yetu imekua ikiasisi matusi ( malofa , wapumbavu, ) na mwaka 2012 kwenye uchaguz mdogo Wa Arumeru mashariki kilisikika maneno machafu yaliyotamkwa mchana kweupe na Mbunge Wa mtera bila vyombo vya dola kuchukua hatua.
Mwaka 2000 kwenye uchaguzi zilienezwa propaganda za kufuta CUF ikielezwa ni chama cha UGAIDI, & UISLAM ili kuaminisha watu na kuwafanya watu wakihame, lakin siasa hizo zikalelewa na vyombo vya dola na wengine wakiogopa kufukuzwa kazi na kushushwa vyeo. Ccm yetu ukitaka kuijibu mapigo unaishia korokoron
Mwaka 2013 ukatengenezwa mkakati Wa UGAIDI dhidi ya CHADEMA ( LWAKATARE) Ushahid Wa uongo ukaandaliwa ili kufuta chama hicho , na tukumbuke tayari kulikuwepo kauli kutoka ndan ya ccm yetu zikisema " CHADEMA HAITAFIKA 2015"maana mimakakati michafu tayari ilikuwa imeshaandaliwa na pengine kuanza kutekelezwa. Lakin tunaumia sana tunapoona chama tulichokitabiria kutokufika 2015 kikiwa imara na salama.
Ccm yetu imetengeneza mfumo mgumu unaowashinda hata watumishi Wa umma, pia vyombo vya dola kutofautisha lipi ni jambo LA siasa za chama na lipi LA kiserikali ambalo halipaswi kutekelezwa kihaki bila kujali vyama ambapo sheria zimekua zikipindishwa makusudi kwa maagizo ya ama katibu au m/ kiti Wa chama. Mfano Mikutano ya hadhara kwa vyama vya upinzan imekuwa ikipigwa marufuku kinyume na sheria ya vyama vya siasa.
Ccm ni kama mtoto kiherehere ambaye ameambiwa na Baba yake kufanya lolote yaan kutukana, kupiga ,kuchoma nyumba za watu, na kutapele baba akiwa anamlinda ikitokea kakamatwa, au kurudishiwa.
Ccm yetu imekuwa ikijenga uadui mkubwa kwa vyama vinavyoonekana kuwa na nguvu ktk jamii na hujenga urafiki Wa karibu na vyama visivyo na nguvu lengo ni kuuaminisha umma kuwa inapenda na kuthamin vyama vingine kumbe ni uongo. Mfano Ccm yetu leo ikotayari kushirikiana na CHADEMA huko Zanzibar maana hakion uwezekano Wa CDM kushinda . Hakijui kufanya siasa safi maana kinaogopa kutokuaminika kabisa
Leo kinaonekana kuwa tayari kushirikiana na ACT WAZALENDO maana hawana madhara kwacho NAAMIN ACT WAZALENDO kipata nguvu leo Uadui na uhasama utaanza na kukua kwa haraka.
Wapinzani kuweni makini sana muda huu, maana ccm yetu inapika mikakati ambayo ni mibaya zaidi ya ile iliyowahi kutumika, mjiandae tu kwa kesi . Na WAFUASI WENU msipojipanga kuwatetea katika kesi SISI CCM tutawasaidia halafu tunawaambia nyie humuwajali wanapopatwa matatizo. Jipange sana tena sana
TUNACHEZA RAFU , UKITURUDISHIA REFA KAONA ,KADI NYEKUNDU UTAIONA