martyr2012
JF-Expert Member
- Jul 18, 2012
- 603
- 245
Wanajamvi, ninasikitishwa na mambo yanayoendelea hapa TZ na hasa kwenye vyama vya siasa. CCM ikiwa ni chama dola kimeonyesha kuchoka kabisa katika kuisimamia serikali. Matokeo yake:
Njia mojawapo ya kuiondoa hali hii ni kubadilisha serikali kwa kuiweka madarakani serikali ya chama mbadala. Tatizo nilinalo sasa na nina imani si mimi tu ni wengi ni chama gani au kiongozi gani? Wakati wengi wakifikiria kuipa nafasi CHADEMA, logic zote zinakataa kutokana na ukweli ufuatao:
Wanajamvi tuyajadili mambo haya si kwa jazba bali kwa kupata mustakbali nzuri wa nchi yetu. Mimi si mwanachama wa CCM wala CDM wala chama chochote. ni Mtanzania ambaye nitaathirika kutokana na sera za chama kitakacho shika dola. Tusilete MATUSI tujadili hoja. Wakatabahu
- Ufisadi mkubwa wa fedha za walipa kodi wa TZ,
- Usimamizi mbovu wa raslimali za nchi
- Kugawa raslimali za nchi kwa wageni ambao wanavuna bila kuacha faida kwa wenye raslimali
- Kukua kwa tabaka la viongozi matajiri walioifisidi nchi na kujitajirisha wenyewe na familia zao.
- Nchi kukosa muelekeo kabisa pamoja na utajiri aliotuajaalia Mungu na hatimaye waTZ kukata tamaa.
Njia mojawapo ya kuiondoa hali hii ni kubadilisha serikali kwa kuiweka madarakani serikali ya chama mbadala. Tatizo nilinalo sasa na nina imani si mimi tu ni wengi ni chama gani au kiongozi gani? Wakati wengi wakifikiria kuipa nafasi CHADEMA, logic zote zinakataa kutokana na ukweli ufuatao:
- CHADEMA ni chama cha kimla
- Haina demokrasia
- Viongozi wa CHADEMA kwenye ngazi ya Taifa hawana uweledi wa kuiongoza nchi.
- Hawana mpango mkakati wa kuiendeleza nchi na raslimali zake bali wanaishi kwa matukio tu. hivyo watakapoingia madarakani watatumia crisis management strategy ili kukabili tukio moja la msimu tu. Likiisha watasubiri jingine au serikali itakuwa 'mfu'
- Ni watu wasiotii sheria na wangependa kupindisha sheria kwa manufaa yao.
- Wana tuhuma za ubadhirifu wakiwa wana 'kifuko' kidogo cha ruzuku ya chama vipi tukiwapa HAZINA ya Taifa?