ccm ni chama cha kisultani?

kibajaj

Senior Member
Joined
Apr 12, 2011
Posts
106
Reaction score
26
Ni siku chache tangu Chama Cha Mapinduzu (CCM)kifanye kile ilichokiita kujivua gamba kule mjini Dodoma.Suala la msingi hapa la kujiuliza ni kwamba je ccm inaendeshwa kisultani? Inakuwaje watoto wa waliokuwa vigogo wa chama hicho kuchukua nafasi za juu za chama? Nape Mnawie ni mtoto wa Moses Mnawie ambaye alishakuwa katibu kuu wa ccm enzi hizo. January .Y.Makamba ni mtoto wa Januari makamba ambaye amelazimishwa kujiuzulu hivi majuzi,angalia akina Dr HUSSEIN MWINYI ni mawaziri,RIDHIWANI .J.MRISHO yuko katika kada ya juu ya ongozi wa vijana wa chama cha mapinduzi. Hebu hapa nisaidieni kuwa huku kurithishana ndiyo usultani au ni kitu gani. Manake kesho kutwa mtawaona wangombea urais na wanapata na hili limeshatokea huko zanzibari. Hii system tuiiteje?
Au chama hicho hakina watu wengine wenye uwezo wa kushika nafasi hizo isipokuwa watotot wa viongozi wastaafu.

Januari ataweza kuhoji nini ua kumuwajibisha Makamba kwa namna gani au atachangia nini kumdhuru baba yake wa kumzaa!
 
Ndio maana sisi vijana tumeamua kuwaachia chama lao! Kijana wa leo mtoto wa mkulima ana nafasi gani humo? Siku zao zinahesabika, TIME WILL TELL.
 
Mbona inajulikana wazi kuwa ccm ni chama cha viongozi wa toka uhuru na familia zao. Tangu niwe mdogo namsikia Moses Mnaye, Msekwa,Malecela,Mwinyi,Makamba,Kikwete,Karume, Malima, n.k kila siku majina hayo hayo tu! Mimi langu la litasikika lini? Ni kwa sababu sisi watoto wa masikini hatuna nafasi humo..bora tujiunge cdm!
 
Kwa nini usiulize pia iwapo vyama vya Democratic na Republican vya US ni vya kisultani?
Bush baba na mtoto wametawala karibuni tu.
Mama Hillary Clinton ni mke wa Rais mstaafu Clinton.
Usisahau pia familia ya marehemu Rais Kenedy ilivyoshiriki siasa za huko.

Huko India kuna hadithi ya familia ya Gandhi walivyotawala.

Kwa ujumla hutokea familia fulani fulani zikawa na kipaji cha uongozi.

Aidha, usidhani kuwa CDM iko salama ktk hili, usultani ulianza siku nyingi kukitafuna chama hiki.

Dr Slaa: mke wake aliyetelekezwa ni mhe Diwani.
Familia za Mhe Mbowe na Ndesamburo: ndio waliojaa kwenye uongozi wa juu wa CDM.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…