CCM na "sizitaki mbivu hizi"


H

Henry Samwel

Member
Joined
Oct 11, 2008
Messages
5
Likes
0
Points
0
H

Henry Samwel

Member
Joined Oct 11, 2008
5 0 0
“CCM NA SIZITAKI MBIVU HIZI”.

Hivi karibuni vyombo vya habari hasa magazeti vimekuwa vikiripoti juu ya mchakato wa uchaguzi mdogo wa Igunga.Binafsi nimevutiwa na mkakati wa CCM kumtumia Raisi mstaafu Benjamini Mkapa pamoja na Mh Rostam Aziz Mbunge wa Igunga aliyejiuzulu.Nianze na hili la kumtumia Rostam Aziz.
Kiukweli bado sijajua kwa nini CCM kimeamua kumtumia huyu bwana mkubwa ambaye jina lake limechafuka kupindukia na hata yeye mwenyewe uchafu huo ulimtikisa kiasi kwamba aliamua kwa hiyari yake mwenyewe kujitoa ndani ya CCM na kubaki mwanachama wa kawaida.Akitangaza uamuzi wake wa kuachia nyadhifa alizokuwa nazo ndani ya CCM,Mh Rostam alisema ameamua kuchukua uamuzi huo ili kuachana na siasa uchwara zilizokuwa zikiendeshwa ndani ya chama chake.Sasa leo hii CCM imemwangukia awasaidie katika kampeni kule Igunga naye amekubali ina maana ataendeleza siasa hizo uchwara ambazo aliamua kuachana nazo?.Huyu bwana pamoja na chama chake wamekosa uelekeo na ndio maana wameonyesha siasa za kinafiki kabisa.Rostam mwenyewe alishasoma alama za nyakati na kuona hatari iliyokuwa ikimnyemelea ndani ya chama chake na kuamua kujitoa,iweje leo chama hicho hicho kilichokuwa kikimpiga vta kuwa yeye ni tatizo ndani ya chama leo kimuone anafaa kama si unafiki ni nini?ina maana thamani yake walikuwa hawaitambui kipindi alivyokuwa gamba na au gamba lishavuka?.Mbona ni muda mfupi sana CCM imesahau kile ilichokuwa ikihubiri kwa mapacha watatu akiwemo Rostam kujivua gamba?.Sasa mmoja ametoka,leo hii hao hao CCM wanampigia magoti awasaidie Igunga kama si unafiki ni nini?.CCM wamethibitisha kuwa huyu bwana hakuwa gamba ma kama angekuwa gamba angeachwa kilichokuwa kikisemwa dhidi yake ilikuwa ni chuki tu binafsi dhidi yake.Hivi inawezekana vipi gamba gamba lililokuwa halitakiwi leo lionekane linafaa?.Rostam naye anashangaza sana na ameonyesha unafiki wa ajabu sana,alisema hataki siasa uchwara leo hii anarudi jukwaani ndani ya sias hizi hizi uchwara alizo ziponda au anataka kusema kuwa hizo siasa uchwara zimeisha?Sasa kwa sababu amerudi katika siasa hizi uchwara atueleze uhusika katika kashfa tajwa ya Kagoda.
CCM pia wameamua kumtumia Raisi Mstaafu Benjamini Mkapa ambaye katika utawala wake tulisikia ufisadi mkubwa hasa wa EPA,Kiwira,Ticts pamoja na uuzaji wa nyumba za serikali..CCM hawa hawa na serikali hii hii ya awamu ya nne ndio waliokuwa wakivujisha siri za ufisadi uliofanywa na Mkapa ili aonekane kuwa yeye si kitu,lakini leo hii viongozi hao hao wa serikali ya awamu hii waliokuwa wakimchafua ndio hao wanataka kuuaminisha umma kuwa Mkapa ni mfano wa kigwa kama si unafiki ni nini?.CCM na serikali yake leo hii wamethibitisha pasipo shaka yoyote kuwa ni viongozi vigeugeu wasio na kauli thabiti zinazosimamia kwa vitendo kile wanaamini.Hakika katika kuwateuwa watu hawa wameonyesha dhahiri kuwa viongozi walionao hawafai na si bora kuliko hawa waliokuwa wakiwachafua.Kikwete kama mwenyekiti wa chama angekwenda kule ili awaeleze wananchi juu ya maisha boro aliyowaahidi lakini kwa kuogopa kivuli chake mwenyewe ameona kuwa ataumbuka.Kumbe udenda unawatoka kwa Rostam AMA KWELI SIZITAKI MBIVU HIZI.
 
S

SEAL Team 6

JF-Expert Member
Joined
Jun 10, 2011
Messages
655
Likes
0
Points
0
Age
40
S

SEAL Team 6

JF-Expert Member
Joined Jun 10, 2011
655 0 0
Kabla ya Mkapa kwenda igunga, CCM kupitia serikali wamemtumia mwanaharakati KAINERUGABA Msemakweli ili amsafishe Mkapa na RA. lakini wamesahau kwamba Mkapa huyo huyo ndiye aliyeuza madini yetu hivi sasa tunapokea asilimia 3%-4% kwa kila mrabaha wa dhahabu, wamelitia Taifa kwenye umasikini wa kutisha. Kichekesho kingine ni pale CCM imemteua yule anayejiita mtaalamu wa madini kugombea Igunga ili aendekuficha madudu waliofanya kwenye secta ya madini. Wana Igunga msipokuwa makini mmeliwa.
 
mashikolomageni

mashikolomageni

JF-Expert Member
Joined
Jan 5, 2010
Messages
1,566
Likes
11
Points
135
mashikolomageni

mashikolomageni

JF-Expert Member
Joined Jan 5, 2010
1,566 11 135
Maji yamewafika shingoni hawana option ila kubeba kila anayefikiriwa kuwa atawasaidia
 

Forum statistics

Threads 1,250,952
Members 481,523
Posts 29,752,169