Hivi mimi na wewe nani mpotoshoji? Jenerali Imran Kombe hakuwahi, hata kwa kukaimu, kuwa Katibu Mkuu wa CCM! Sijui uzushi wako umeutoa wapi? Maneno "CCM imepoteza dira" ni kweli yaliwahi kutamkwa na Katibu Mkuu wa CCM aliyekuwa akiitwa Horace Kolimba na alifariki miezi michache baada ya kuwekwa kiti moto na wenye chama lakini sio kwa kuuwawa na Polisi au kwa risasi.