CCM na Serikali ya Mama Samia ni ilele

DIZZO MTAWALA

JF-Expert Member
Aug 22, 2015
240
767
Nimeona watu wakiona ahueni baada ya Mama kukalia kiti kwangu mimi CCM na serikali yake ni ileile tofauti ni namana mkalia kiti anavyoimbisha wasikilizaji.

Mama Samia kapokea ripoti ya TAKUKURU na ya CAG kamsimamisha kiongozi wa bandari, watu wameshangilia balaa katikati ya kushangilia tuoneshwa madola yamekutwa kwa mzee wa bandari hapa ndio nilielewa CCM ni ileile wanapita njia zilezile kuaminishana hatua zimechukuliwa rejea wakati Hayati JPM alipoingia madarakani yakaanza maigizo mara ohhh pesa zimefichwa mara bwana mmoja anaitwa Masamaki kakutwa na mihela ohh ana nyumba mara Dkt. Dau yaaani sarakasi kibao ndani ya maigizo yao na mbuzi wa kafara kama huyu wa bandari yananogesha lakini ni picha la kutuaminisha CCM imebadilika lakini.

CCM hiii ndo imeminya uhuru wa habari, imeruhusu watu kuporwa fedha zao kwa kisingizio cha kodi.

CCM hii ndo imeruhusu wakosoaji kugeuzwa wahaini, CCM hii ndo imefanya mtoto wa kike akipata mimba asirudi shule, CCM hii ndio matukio ya utekaji sio kwa JPM hata utawala JK, Mwangosi aliuwawa mbele ya Kamanda wa Jeshi la Polisi kina Kibanda, Kubenea na kina Ulimboka.

Tofauti ni matumizi ya kufanyia kazi malengo ya CCM, JK alitumia mfumo wa CCM kupitia green gurd wakati JPM alitumia vyombo vya dola kuhalalisha ukandamizaji wa demokrasia.

Mwisho sioni mabadiliko yoyote kutokea ndani ya CCM na zaidi ni maigizo kupooza alichofanya JPM.

Leo kamteua Philipo Mpango kuwa Makamo wake huyu aliyekuwa akipika data za uongo aliyezulumu pesa ya korosho.

Matatizo ya nchi yataondolewa siku dubwana CCM litapopelekwa makumbusho ibaki historia tu.
 
Uko sahihi! Nchi hii itapata maendeleo ya kweli tu, CCM itakapo toka/tolewa madarakani. Zaidi ya hapo, tutaendelea tu kupumbazwa miaka nenda na porojo zao.
Ni mjingatu Anae Amini wapinzani wakichukua dola nchi itapata maendeleo, maendeleo yanapatikana kwa kutegemea wazungu?

Bora. Chama cha Mapinduzi kimejipambanua kuondokana na utegemezi ndani ya miaka 5 na nchi imekimbia kimaendeleo.
 
Ni mjingatu Anae Amini wapinzani wakichukua dola nchi itapata maendeleo, maendeleo yanapatikana kwa kutegemea wazungu?

Bora. Chama cha Mapinduzi kimejipambanua kuondokana na utegemezi ndani ya miaka 5 na nchi imekimbia kimaendeleo.
Wewe utakuwa ni mtoto wa juzi. Hivyo hufahamu chochote kuhusu CCM! Uwe na utaratibu wa kuwasikiliza wakubwa zako. CCM ni zaidi ya hivyo unavyo ifahamu.
 
Ni mjingatu Anae Amini wapinzani wakichukua dola nchi itapata maendeleo, maendeleo yanapatikana kwa kutegemea wazungu?

Bora. Chama cha Mapinduzi kimejipambanua kuondokana na utegemezi ndani ya miaka 5 na nchi imekimbia kimaendeleo.
Ungeijua CCM ungeanzia 1977 ilipozaliwa na ilipofungamanishwa na dola mwaka 1984 na ilipokataa mfumo wa vyama vingi.
 
Sasa si mlikubaliana mama atasafisha nchi ndugu zangu?

Mlikubaliana twende na mama asafishe Sukuma gang, sasa mbona mnarudi nyuma Wakigogo?
 
CCM haiwezi kutuletea maendeleo ya kweli ndiyo maana tunamuomba mama atumie sheria na busara zake kuendesha nchi.

Maendeleo tutapambana wenyewe kujiletea maendeleo ya kweli kwenye familia zetu.
 
Uko sahihi! Nchi hii itapata maendeleo ya kweli tu, ccm itakapo toka/tolewa madarakani. Zaidi ya hapo, tutaendelea tu kupumbazwa miaka nenda na porojo zao.
Yamekuwa haya tena, jana si mlikuwa mnamshangilia Rais. Leo kosa lake ni kumchangua Mpango? Nchi hii ngumu sana.
 
Back
Top Bottom