CCM na project mfu zilizochanganyikiwa

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
374,221
Reaction score
866,534
Siku hizi kuna press conference karibia kila siku za mikoa mbalimbali za viongozi wa CHADEMA mikoani kukikimbia chama cha CHADEMA...

Jamani hata kama chama hakipendwi mbona huu utaratibu umenyooka sana na uko so systimastically!? Yaani unaona kabisa ni script za kuandaliwaπŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚

Halafu sasa sababu wanazotoa ni full vichekesho.. Yaani CCM imeishiwa... I me hang any I kiss mpaka mambo inayofanya Nata mtoto mdogo anawashangaa na kuwacheka

Hizi script za sasa ni baada ya ile ya G55 kufemea vibaya sana. Haikuchelewa kujulikana kwamba asilimia 95 ni watani zangu wachaga. Hili lilikuwa bonge moja la kosa la kimkakati

Sasa wakaja na plan B ya kurekebisha kosa la kwanza.. Viongozi wa mikoa mbalimbali kuhama chama
Cha kujiuliza ni hiki.

Mbona wanahama viongozi tu bila wanachama wowote!?πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ halafu wote kwa press conference mahususi? Zinazorushwa na chombo kilekileπŸ€”πŸ€£

CCM maji ya shingo na mfa maji haachi kutapatapa
 
Na mimi nimejiuliza na pesa zinazotumika kuchezea sasa hivi ni nyingi.
Wakijua wewe una nguvu ya watu hata kama sio mwanasiasa wanakufata na kukupa pesa yoyote unayotaka
 


Ninaitwa Grace Kiwelu ni Mwenyekiti wa Bawacha Mkoa wa Kilimanjaro, Mwenyekiti kamati ya Fedha wa kanda ya Kaskazini na ni Mjumbe wa kamati tendaji ya Bawacha Taifa. Leo nimesimama mbele yenu kwanza kusema ahsante kwa Chama changu Chadema, kimenipa heshima, nimekuwa Mbunge, nimekuwa Mjumbe wa Kamati kuu na nimejiunga na Chama hiki tangu mwaka 1992 nikiwa Binti na leo nazeeka ndani ya Chama lakini leo nimesimama mbele yenu kwa maumivu makubwa kwasababu nitasema mwishoni ninaenda wapi.

Chama changu nilikipenda sana na nilikitumikia kwa moyo wa dhati, tulizunguka nchi nzima hii kuijenga Chadema, tulikuwa tunazunguka na Mbowe kuhakikisha Chama chetu kinaenea Tanzania nzima, tulifanya ziara wakati huo tukiwa wabunge watano tu, mimi nikiwa Mbunge pekee mwanamke kuzunguka nchi hii tukiwa na fuso, tunaweka viti, meza, spika. Tunazunguka na hatuna mwanachama hata mmoja huko tunapoenda. Tukifika tunashusha viti, tunafunga Spika, tunahutubia miti na watoto. Leo namshukuru Mungu tumefika

hapa lakini badala ya kuvuna heshima, tunavuna matusi. Tulishauri chama kwa nia njema kwamba tunahitaji reforms ndio lakini tusizuie uchaguzi. Unawezaje kuzuia uchaguzi wakati wewe sio mshirika wa uchaguzi? Tunafanyaje mikutano wakati tumeshasema tunaenda kuzuia uchaguzi? Tunauzuiaje uchaguzi?, wakasema tutazuia kwa maandamano. Leo wananchi wangu wa Vunjo niwaambie tunaandamana kuzuia uchaguzi, tunaanzia wapi tunaishi wapi? Wazee wangu wa Vunjo na vijana,tunaanzia wapi? Maandamano tunayofanya ama vijana wanaoandika leo kutukana baba na mama zao kwenye mitandao hutowaona kwenye maandamano. Na niwaombe sana wananchi wangu wa Vunjo, nilikuwa mmoja wa G55 kwasababu ninawajali, ninawaheshimu na ninawapenda.

Uamuzi ninaouchukua leo mnisamehe nakipenda, na niliipenda sana Chadema kwasababu ilinipa heshima sana, kufika hapa nilipofika nilijengwa na Chadema lakini sasa itoshe kusema kuanzia leo Tarehe 11 Mei, 2025 ninajiondoa rasmi Chadema, ninakwenda nyumbani- bado nina nguvu, sisemi ninaacha siasa lakini acha kwanza nikapumzike, na ninamshukuru Mungu sana kwamba Aprili 27, mwaka huu Mungu alinipa Mjukuu, nakwenda kulea Mjukuu wangu. Nimechoka na matusi ya mitandaoni kila siku.
 
Na mimi nimejiuliza na pesa zinazotumika kuchezea sasa hivi ni nyingi.
Wakijua wewe una nguvu ya watu hata kama sio mwanasiasa wanakufata na kukupa pesa yoyote unayotaka
hawa viongozi wa chini nao wanavuna pesa kiasi chao mtu anahama chama kirahisi tu
 
Ninaitwa Grace Kiwelu ni Mwenyekiti wa Bawacha Mkoa wa Kilimanjaro,
 
sisemi ninaacha siasa lakini acha kwanza nikapumzike, πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
CCM inahusikaje hapa? Hizo ndio siasa mpya za upinzani CHADEMA. Umesahau timu Lissu ilivyokuwa ikiitisha mikutano kila siku wakati wa kampeni za uchaguzi wa Januari 21, kutishia kujitoa endapo Mbowe angeshinda?

Ingia YouTube. Ni kweli Mbowe angeshinda hii kimbikimbia ya sasa ungeiona siyo tu kwa wanachama bali Lissu mwenyewe na Heche wangetoka CDM na kundi lake. Watu wa Mbowe nao wanafanya kama walichokusudia kufanya watu wa Lissu. Tuachane na CCM haihusiki na upuuzi huu, mchawi wa CDM ni wao wenyewe.πŸ™πŸ™πŸ™
 
Ikiwa ni kwa hiari wala hakuna shida kabisa... Lakini kama ni kwa shinikizo na ushawishi wa pesa wa ccm hapo ndio msingi wa mada ulipojikita
 
Your browser is not able to display this video.
 
Ebu fikiria WAJINGA kama hawa eti ndiyo tegemeo la kuipa maendeleo Tanzania..... CCM Wana laana kabisaa
 
Ikiwa ni kwa hiari wala hakuna shida kabisa... Lakini kama ni kwa shinikizo na ushawishi wa pesa wa ccm hapo ndio msingi wa mada ulipojikita
Nakuelewa. Ila kwa kuwa huja establish kama wanapewa pesa au la..ungehoji na kuchambua internal na external factors zinazoyumbisha CHADEMA. Tena nakushauri jikite kwenye masuala ya ndani ya CHADEMA kwa kuangalia trend tangu uchanguzi wa Januari. The issue is; watu wa Mbowe hawaaniwi na watu wa Lissu. Vivyo hivyo watu wa Lissu wangeshindwa wangejitoa. Siioni CCM popote katika mgogoro huu.πŸ™πŸ™πŸ™
 
ccm ina mkono wake mkubwa kwenye hili kwakuwa bila CHADEMA kuyumba hatimq yake iko shakani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…