CCM na Njaa kwa Watanzania.

CCM na Njaa kwa Watanzania.

M.L.

Senior Member
Joined
Feb 11, 2012
Posts
185
Reaction score
120
Ni hakika nchi inakabiliwa na mabadiliko ya hali ya hewa ambayo si rafiki kwa shughuli za kilimo na ufugaji. Lakini, CCM-mafisadi wamechochea njaa na ufukara kwa watanzania.
Mathalan, bodi na mamlaka za mazao ni za kifisadi. Makampuni ya pembejeo ni yao mafisadi -vigogo wa ccm. Makampuni ya ununuzi wa mazao ni ya hao hao vigogo mafisadi wa ccm. Mafisadi hawa, huwalazimisha wakulima kukopa pembejeo kwenye makampuni yao; pembejeo hizo huwa feki. Wamefanya hivyo Shinyanga kwa wasukuma wakulima wa pamba; wamefanya hivyo kwa wakulima wa mpunga Kyela; wamefanya hivyo kwa wakulima wa korosho mikoa ya kusini.

Tenda zote za kilimo na ufugaji huamuliwa na wao wenyewe. Wakigawana tenda hizo.

Wanajulikana, wanafahamika, wanajulikana na wapi hukutana kupanga hujuma na ufisadi huo. Lakini hakuna hatua zinazochukuliwa dhidi yao.

Kisha, hurudi majukwaani, kusema eti wanataka kuleta maendeleo kwa wananchi. Huu ni unafiki. HIYO NI ROHO KAMILI YA KICHAWI. Haya, yote wanayafanya kwa kuwa ni waabudu mizimu na majini. Hawa ni mashetani, maana shetani haji isipokuwa ana misheni tatu: kuharibu, kuiba na kuchinja. Hiyo, ndiyo CCM ya mafisadi waleta njaa na ufukara wa watanzania.
 
hatua madhubuti dhidi yao nikuwatoa madarakani na kuweka chama kingine especially pipooos! hahaha 2015 kitaeleweka.
 
Back
Top Bottom