CCM na mwelekeo wa kufa 2015

CCM na mwelekeo wa kufa 2015

robert deusi

JF-Expert Member
Joined
Dec 3, 2014
Posts
399
Reaction score
69
Kuna vitu ambavyo naona kabisa vinaiangusha serikali na chama chetu cha CCM.

1.Huduma za jamii zimesahaulika kuanzia elimu,afya na nyinginezo nyingi tu.

Kwa kujua au kwa makusudi viongozi wote wamekimbilia kwenye ufisadi na kufisidi mali za umma.

Nchi imepata uhuru zaidi ya miaka 50 lakini mpaka leo hakuna maendeleo ya kujivunia.Inatia aibu kuona kwamba mpaka leo wanafunzi wanakaa chini,wajawazito wanajazwa chumba kimoja hii ni aibu iliyoje?

Cha kutia aibu zaidi viongozi wanaongozana kila uchwao kwenda nje kuomba msaada wakati nchi ina uwezo wa kujiendesha endapo kama rasilimali zitasimamiwa ipasavyo.

Kwa mtindo huu ikatokea UKAWA ikapewa nchi mwakani kutakuwa na lawama kweli? Hapana ili ni kosa la sisi wenyewe wanaccm kwa kuacha mambo ya msingi na kuzingatia mambo yasiyo na faida.

Sasa hivi chama kimeanzisha tabia chafu ambayo naona inaenda kukizika chama kabisa bila msosi na malori ya kuwaleta watu kwenye mikutano ya chama watu awaji hii ni dalili mbaya sana katika chama.

Ningeshauri kama inawezekana CCM ikae pembeni ili wengine nao waongoze na sisi tupate muda wa kujipanga na kurekebisha makosa yote kuepuka aibu ambayo inaweza ikatukuta 2015 au 2020.
 
Back
Top Bottom